Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Sipati picha watu wanavyoomba kupangiwa kazi ya ofisi ya makamu wa rais
Usishangae kwa sababu sasa ni ofisi ya Mkm/Rais ndo iliyo TOO ACTIVE na ina overshadow ofisi ya rais Magufuli.
Najua hili hatapenda kulisikia lakini huo ndo ukweli wa mambo.
 
Huyu hana tofauti na kakamega sory kagame .
alishasema hapangiwi au umesahau hii kauli yake[emoji61]
 
Kwa Mhe Rais wetu, Rais Mtukufu na wa wanyonge wote Tanzania.
Salaam.
Jana nilikuangalia na kukusikiliza kwa makini ulipokuwa wanatoa neno baada ya kuwaapisha Majaji uliowateua wiki hii. Niliona pia ulipomsimamisha CAG na kumuuliza kama kuna pesa trillioni 1.5 alizogundua kwamba zimeibiwa na akakujibu hakuna.
Pia nilikusikia ukisema umeisoma taarifa ya CAG mwanzo hadi mwisho.
Haraka nilikimbilia kitabu changu ambacho nami nimekisoma mwanzo mpaka mwisho.
Nilipofungua ukurasa wa 34 niligundua haya:-

1. CAG Anasema, kwa mwaka wa fedha 2016/17 Serikali ilipanga kukusanya mapato yenye dhamani ya Shilingi Trillioni 29.5

2. Mapato halisi yaliyokusanywa ni Shilingi Trillioni 25.3

3. Serikali ilitumia shilingi Trillion 23.8

4. Trillioni 25.3 ukitoa Trillion 23.8 ni Trillion 1.5 ambazo ndizo anazotaka apewe maelezo.

Mtukufu Rais CAG hajasema pesa zimeibiwa. Wala ktk hatua hii hawezi kusema hivyo. Anachosema fedha hizo, matumizi yake hayaonekani na hazipo popote. Inawezekana kweli zimeibiwa, zimetumika kwa uzembe bila kufuata sheria au zipo mahali fulani.

Kwa taratibu za kibunge Maafisa Masuuli(accounting officers) wanatakiwa wampelekee ushahidi wa matumizi yake au ziliko ktk Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali yaani PAC mbele ya CAG ili hoja hii ifungwe. Kama wakishindwa kuifunga PAC na CAG sasa wanaweza kuomba msaada wa Polisi na au Takukuru kutafuta wezi au wabadhirifu.

Mhe Rais bila shaka umesoma pia ktk ripoti kwamba Serikali ktk ujumla wake imepata HATI CHAFU.
Wakati ukipokea taarifa hii Ikulu uliagiza Mkurugenzi wa Mji wa Kigoma Ujiji na wa Pangani watumbuliwe kutokana na maeneo yao kupata hati chafu.

Mhe unasubiri nini kumtumbua Katibu Mkuu hazina kwa kuisababishia Serikali yako kupata Hati chafu? Mbona kila mara unaapa kuwa mtu wa haki na jana uliwaagiza Majaji wakatende haki kwa Watanzania hasa wanyonge?

Mheshimiwa Serikali yako imepata doa kubwa. Vyombo vya dola haviwezi kulizuia kwa kuwatisha wanaoandika. Hizi ni fedha za maskini wote unaowatetea wauza maandazi, mitumba, mchicha na wengine wakubwa.

Ninakushauri baadala ya kuwatisha wanaohoji, waagize watendaji wa Serikali yako, wapeleke maelezo ya kutosha yenye ushahidi kwa CAG. Vinginevyo hatutaacha kukuuliza kila mara ZIKO WAPI PESA ZETU SHILINGI TRILLION 1.5

Jana Naibu waziri wa fedha alisema uongo Bungeni akidai sehemu ya fedha hizo Billioni 200 Serikali ya Muungano iliisaidia Serikali ya Zanzibar kukusanya mapato yake huku Bara.

Wote tunajiuliza vyanzo vya mapato ya ZNZ huku bara ni vipi? Hebu atutajie tuvijue na je! utaratibu huo ulikuwa wa 2016/17 peke yake tangu uhuru au ulikuwepo Taifa lisijue?
Mheshimiwa naona nakuchosha lakini nataka kusema neno la mwisho.
Inawezekana unadanganywa sana na waliokuzunguka na kwamba hawakuambii mambo mengi kwa faida yao. Wanapenda tu kukuambia yale wanayogundua unapenda kuyasikia na wanaogipa kukukosoa kutokana na ukali wako. Panua wigo wasikilize hata wale ambao hupendi kuwasikia hutakosa jambo lenye faida. Asante.
 
Pesa Trillion 1.5 imetumika kununua ndege, kukomboa ndege Canada, kuwanunua wabunge, madiwani wa chadema, kurudia chaguzi, uchakachuaji, kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani nk pesa nyingi ya Nchi imetumika kwa mambo ya hovyo hovyo ikiwemo kumlipa Cyprian msiba na kafulila kutengeneza Uzushi na Propaganda za kishamba na kijinga jinga kuwahadaa watanzania.
 
Nchi inaongozwa na wasukuma wawili washamba toka kolomije na chato wanatumia Katiba ya kuanzia 1971- 1979 ya uganda ni katiba ya marehemu idd Amin dada, wake-copy Tabia zote za marehemu idd Amin Dada na msaidizi wake marehemu colonel Maliyamungu, ambao walikuwa watu Hatari na wakatili hakuna mfano, walichukua pesa Hazina ya uganda hata usiku na Gavana alipokataa aliawa na Tanzania ya sasa Gavana aliyepita alikuwa akigoma kutoa pesa kienyeji ndipo wakamtoa na kumpachika wao ambaye huwapa pesa mda wowote hata saa nane usiku , utawala huu wa Awamu ya Tano unaendesha Nchi kienyeji sana, Maliyamungu Bashite Naibu Rais ana nguvu kuliko waziri mkuu na makamu wa Rais hata Bunge, kwa bahati kipindi hiki watanzania wameamka hawataki kusikia Propaganda za polepole wala ujinga wa akina kafulila na Cyprian msiba.
 
Nafasi ya mshauri wa Rais inatendewa haki?
Mh.Rais kujibizana na wanamitandao/wanasiasa kwenye majukwaa yenye maudhui tofauti ni sahihi?
Je,kuna haja ya kuhutubia taifa kila mwezi?
Je,hotuba ya mh.Rais inatakiwa kuandaliwa jitaalamu zaidi?
Je,ni muhimu mh.Rais kufuata yale tu yaliyoandaliwa kwenye hotuba bila kuathiri maudhui yaliyokuudiwa?

Ushauri wa CAG usichukuliwe juu juu alimaanisha kwa kutumia lugha ya kisomi mtu mwingine angechafua hali ya hewa.
 
Kwa sasa ni zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM pekee, mshauri mkuu hana vyeti na ni Naibu Rais unategemea nini?
 
Ni heri ashauriwe na bashite atamuelewa mara moja sio wewe! Ndivyo alivyo.
Maliyamungu idd Amin Bashite ndiyo mshauri mkuu wa Mtukufu malaika toka. Kwani ulidhani kuna mshauri mwingine mkuu? wapo washauri wengine lakini ni waoga wa kumkosoa humshauri kile anachopenda kukisikia ikiwemo kudhoofisha upinzani na kurejesha mfumo wa chama kimoja kama Cuba na China .
 
Mimi nashindwa kuelewa kabisa, inaonekana hawa viongozi kwanza hawana maelewano wenyew kwa wenyew. Anachoongea Pole pole ni tofuti na Mkuru na naibu wa fedha.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…