Ushauri wangu kwa Mhe. Mkuu wa Nchi. Nikupongeze kwanza kwamba unafanya mambo mazuri ya ujenzi wa Taifa letu ya kutuletea maendeleo na heshima. Kipekee nikupongeze kwa kuwakemea walioifanya nchi hii kuwa shamba la bibi!
Kuwa ujumla:
1. Jenga taasisi imara na huru katika kutekeleza majukumu yake. Mahakama, Bunge, Serikali na vyombo cha habari. Vyombo hivi vinalinda nchi hata kama watakuja viongozi wabovu nchi haitatetereka sana. Jenga taasisi hizo kabla hujaondoka madarakani.
Mkuu hapa naona tunapenda kurudia rudia mambo bila kujua chanzo ni nini na utafiti wa kina kufanyika na kuelezea hizo taasisi mnazo zizungumzia zina majukumu gani na kwa vigezo vipi?
Naomba tufafanulie huo uimara na uhuru wa taasisi unavyotakiwa kuwa. Ninavyo jua mimi nchi karibu zote duniani jaji mkuu wa muhimili mahakama huteuliwa na Rais wa nchi, kuna tofauti gani na Rais wetu anavyo fanya? Ulitaka jaji mkuu ateuliwe na nani?
Muhimili mwingine ni Bunge, tuelezee unapendekeza reform gani katika kuwateua viongozi wa Bunge kama Mh. Spika na kadhalika?
Muhimili wa tatu ambao ni serikali Rais ni kiongozi wake mkuu ambaye anasimamia shughuli zote za uendeshaji wa serikali na mtendaji wake mkuu ni waziri mkuu. Unataka mabadiliko gani hapo ili serikali iwe huru na imara?
Kuna vyombo vya habari ambavyo vina milikiwa na serikali na viko vingine vingi ambavyo ni vya binafsi. Sasa hapa ulitaka mambo yaendeje?
Vyombo vya habari vya watu binafsi mbona viko huru? Swala hapa nalo liona ni kwamba vinatakiwa viwe makini katika kutoa habari ambazo zina husu serikali. Visiwe vinatoa habari za uongo ili kuipotosha umma na kuwafanya wananchi kuichukia serikali yao bila sababu na hivyo kuhatarisha usalama wa nchi.
Katiaka nchi ambazo hazina maendeleo makubwa kama Tanzania ni kitu muhimu sana kuangalia media inafanya nini. Media zinaweza zikatumiwa vibaya kama Rais mwenyewe ulivyosema. Pia tusipende kuilinganisha Tanzania na nchi zilizoendelea tunaweza pata shida kubwa, kwani wananchi wengi hawana elimu ya kuwafanya wawe na reasoning character hiyo unayo ifikiria.
2. Katiba mpya. Hii ni sheria mama inayoweka mazingira ya usawa kwa kila mwananchi. Tafadhali wateue wabobezi wachache wa katiba hata kama wengine wanachangia toka nje kuliko kuweka watu lukuki hiyo haina tija. Andaa hii kabla hujaondoka madarakani na utaiacha nchi pazuri.
Sawa, tunapo zungumzia katiba lazima pia tuzingatie uwepo wake ili kujua kuna manufaa gani kwa nchi na watu wake. Katiba ni paper work ambayo inalindwa na mihimili hiyo mitatu; serikali, Bunge na Mahakma. Kuna nchi duniani hazina katiba kwa mfano England na kuna nchi nyingine kama Kenya ambako katiba ipo na wamejaribu kui-reform kuwa kama ya Amerika, lakini je imesaidia kitu chochote? Mimi naona ukabila bado upo pamoja na katiba mpya.
Tusiwe na Illusion ya kuamini kuwa maandishi peke yake yatatusidia kuwa na viongozi bora kama watu wenyewe hawafuati kanuni zake. Nikupe mfano, CCM inakatiba nzuri sana ambayo ilitengenezwa na waanzilishi wa nchi yetu. Uliona mambo yaliyo tokea kwenye CCM ya awamu ya tatu na ya nne? Kuna mambo ya rushwa yameandikwa humo, kuna maswala ya uteuzi wa viongozi yameandikwa huko, lakini je CCM ya awamu ya tatu na ya nne iliyazingatia hayo? Mafisadi wengi walikuwemo kwenye hicho chama mpaka Rais Magufuli alipo ki-reform.
Naomba tuachane na ndoto za mchana kinacho takiwa hapa mabadiliko ya mind set na maendeleo ya mtu binafsi.
Specific
Uchumi unaendeshwa na sekta binafsi. Serikali isijiingize kufanya jambo lolote ambalo linaweza kufanya na sekta binafsi. Ni hatari kufanya hivyo kwa sababu hasara ni kubwa. Kwanza Serikali inatoa sera na kisha kusimamia na haiwezi kujisimamia na kwa sababu hiyo haitalipa kodi, itatoa huduma kwa kiwango cha chini cha ubora na kwa gharama kubwa zaidi, ajira zitapotea nk. Ni disaster kwa Serikali kuingia huko. Kwa maana hiyo hata ndege tungewaachia sekta binafsi.
Yaani hii ni theory isiyekuwa na msingi. Of cause serikali inweza kujiingiza katika shughuli ya uzalishaji.
Sikiliza mkuu Ujerumani inamiliki kwa asilimia kubwa Railway yao ya Deutsche Bahn pia kampuni ya magari ya Vokswagen shirika la ndege la Lufthanser na kadhalika kuna hathari zipi zimetokea?
Kipindi cha nyuma serikali ya uiingereza nilisikia ilijaribu ku-privatize Railway yao na shirika la umma la kuzoa taka. Waulize waingereza mambo yaliyowakuta ni yapi? System zao za uendeshaji wa treni mbaya kupindukia. Amerika nako hivyo hivyo. Nenda Kaangalie system ya treni Germany, Sweeden, Switzerland na Ufaransa, utaona tofauti kubwa sana. Hapo ndipo utaona tofauti kati ya private na Parastatal institutions.
Msipende tu kubwabwaja vitu "just for the sake of" kubwabwaja, angalieni mifano iliyopo. Ethiopia Airline mbona ina fanya vizuri? Liko chini ya nani?
Tukija Tanzania Reli yetu ya kati na viwanda vingi ambavyo Rais wa awamu ya kwanza alivianzisha na baada ya serikali ya awamu ya tatu ku-privatize, viko wapi? Na sasa Rais Magufuli ana anza upya tena kuvifufua. Huyu jamaa sio wa kucheza naye ni mzalendo haswa. Amekaa serikalini akisoma matendo yote maovu yaliyo tokea. Anajua nini anafanya na wapi kuna udhaifu.
Mchuchuma + Liganga
Peleka Umeme kule, au tumia makaa ya mawe kuzalisha umeme kwa ajili ya kufua chuma pale au watumie huo huo mkaa. Wape jeshi hiyo kazi nafikiri wataiweza. Hata kama wataajiri mtaalamu wa kuwasaidia. Hata reli zilizobaki tutumie hiyo chuma kujengea.
Hapo hata mimi nakuunga mkono. Hapa simweelewi Rais vizuri. Kitu gani kina mshinda kutawanya pipe lines ya gesi asilia Dar es salaam na miji mingine ambako kuna gesi asilia kama Mtwara, Lindi na kadahalika, watu wakawa na Energy ya kutosha kupikia badala ya kutumia mkaa? Energy sio umeme tu. Makaa ya mawe, Geothermy na kadhalika.
Mimi nashangaa kwa nini nchi kama Tanzania kwa hivi sasa tuna uhaba wa umeme. Tunaweza tuka tumia trilion moja TSHS kuzalisha umeme ambao tukasambaza kwenye miji mikubwa yote kwa kutumia G and S Circles. G stands for Gas Turbine na S stands for Steam Turbine. Gas turbines zinazalisha umeme na kutoa hot air ambayo inaenda kuchemsha maji. Ule mvuke unaotoka kwenye boiler unaenda ku-drive Steam Turbines ambazo zinazalisha umeme kwa Zero Tarif. Steam Turbines hapa hazitumii energy yeyote ile katika kuzalisha umeme. Kwa hali hiyo tunapata umeme zaidi kuliko matumizi ya gas. Yaani unatumia fuel ndogo kuzalisha umeme maradufu.
Mimi saa nyingine nashidwa kuelewa nchi yetu imezalisha wasomi au ma-engineers wa aina gani? Yaani vitu vidogo kama hivi vitushinde, nchi ambayo tuna Gas asilia, tuna makaa ya mawe, tuna uranium na Geothermy. Badala yake tunahangaika na vigenaratos vya wachina na wahindi kweli?
Tuna poteza mabilions na mabilions za fedha kwenye mabarabara na ma-flyovers tunashindwa ku-invest kwenye chip energy? Kwa mfano, kulingana na mahesabu yangu tuna hitaji umeme Tera Watt 10 ambazo ni Mega Watt 10,000.
Kulingana speech ya Rais mwenyewe, amesema umeme wa Stiegler utata Mega Watt 2100 yaani Tera Watt 2.1 na huu tulio nao Tera Watt 1.7, kwa pamoja utafanya Tera Watt 3.8.
Rais Amesema pia kwenye General reserve tuna kama bilioni sita hivi US Dola, katika hizo akichukua bilioni nne tuna Pata umeme wa Tera Watt 5, kwani mtambo mmoja wa G&S-Circle una cost milioni $15 nao utazalisha umeme wa Mega Watt 20. Kwa hiyo katika Tera Watt 5 tutaagiza mitambao 250 ya G&S-Circle. Tayari tuna Tera Watt 8.8. Huu umeme utatuwezesha kusambaza kwenye miji yote mikubwa na kwenye Standard gauge yetu. It is so easy. Hatuwahitaji wachina wala Wajapan. Tunafanya sisi wenyewe. Izingatiwe kuwa wauzaji watatuletea ma-specialist wao wanne au watano mengine yote ni kufuata instractions tu. Watanzania wazalendo tunaweza utaalam tunao. Serikali ituite tu kama iko tayari.
Nami ningemshauri pia kufanya Energy Mix. Asitegemee Stieglers Gorge peke yake, mito na yenyewe inakauka. Global warming inakuja japo kuwa slowly lakini ipo. Itakuja kutukumba siku. Nilivyo kuwa mdogo niliziona picha na clips za mlima Kilimajaro barafu ilijaa, nenda sasa kaone kila kitu kimebadilika! Najua ni vigumu kuuza gesi yetu nje kwa sababu kuna nchi nyingi ambazo zina produce gesi asilia kwa wingi, lakini tunaweza tuka tumia kwa ajili ya atumizi ya local.