Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Huwa nashindwa kuelewa kwann had leo lugha yetu mama (kiswahili) haijaanza kutumika kufundishia ktk ngazi zote za elimu hapa TZ kuanzia shule ya msingi had ngazi ya chuo, na si kutumika sule ya msingi pekee km ilivyo hv sasa
 
Haya ni wazo mazuri sana ambayo hata mimi nayaunga mkono asilimia mia moja.
 
Huwa nashindwa kuelewa kwann had leo lugha yetu mama (kiswahili) haijaanza kutumika kufundishia ktk ngazi zote za elimu hapa TZ kuanzia shule ya msingi had ngazi ya chuo, na si kutumika sule ya msingi pekee km ilivyo hv sasa

Matumizi ya kiswahili katika kufundishia toka shule ya msingi ni baadhi ya sababu elimu yetu kuwa duni. Viongozi wote unaowajua ww hakuna anayepeleka mtoto wake kwenye shule inayofundisha kwa kiswahili. Kupeleka mtoto wako kujifunza kwenye shule inayotumia kiswahili ni kumgeuza kuja kuwa manamba huko mbeleni. Kiswahili ni lugha inayopaswa kutumika huko mtaani na sio kufundishia. Kiswahili hakina tofauti na kigogo, kihaya, kizaramo nk.
 
sasa tuachane na reli na bombadier ili tuendelee na ushauri wako au tuchanganye vyote ?
Usikonde Tanzania ni tajiri. Tuna Diamond, Gold, chuma na Nickel na Cobolt. Tunaweza fanya projects hizo zote na nyinginezo zaidi. Tena ningemshauri Mh. Rais aongeze Standard Gauge Rail way nyingine mpaka Mtwara, Songea na Mbeya. Tuna uwezo wa kulipa. Asumed tuna wapata viongozi wenye msimmamo wa Rais Magufuli na sio kama Mkwere yule. He was a catastrophe! Sijui kama mwenyewe anajitambua huko aliko?

Projects kubwa kama hizi zitatoa ajira kubwa kwa wananchi na kutufaidisha katika kupata utaalam kwa vizazi vyetu vijavyo. Ila tu tusichukue mikopo China. Mikopo ya wachina ni matatizo makubwa sana kwa Afrika na isitoshe wachina wanawaleta watu wao kufanya kazi huku kwenye hizo projects. Nakumbuka nikiwa mtoto wakati wa ujenzi wa TAZARA, nili waona wachina watupu kwenye hiyo project. Chonde chonde Rais! Tuwatumie wajapani na wakorea kusini. Wajapan ni wazuri sana katika kutengeza "High Speed Trains" na Quality ya kazi.

Na kama Rais atapenda mimi mwenyewe ni Engineer pia. Naweza kuja isaidia serikali katika utaalam wa Mambo ya Trains. Nina ujuzi nayo mkubwa na nina wajua baadhi ya wataalam ambao sasa ni mastaafu nili kuwanao Sweeden.
 
Wote walioko serkalin walisoma shule za vingereza??
 
Wote walioko serkalin walisoma shule za vingereza??

Sifa ya kupata kazi ya serekalini ni utanzania wako sio lugha. Ingekuwa hizi kazi zina ushindani na watu wa nje unegeshangaa. Jaribu kwenda kwenye za mashirika ya kimataifa uone idadi ya watanzania na zile nchi zinazofundisha kwa kiingereza. Na usiombe hizo kazi za serekalini zikatolewa kwa wageni, ww na ndugu zako mtaishia kupika chai.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] umenena mkuu kungekuwa na ushindan na watu wa nje kweli ingekuwa balaaa
 
Ushauri wangu kwa Mhe. Mkuu wa Nchi. Nikupongeze kwanza kwamba unafanya mambo mazuri ya ujenzi wa Taifa letu ya kutuletea maendeleo na heshima. Kipekee nikupongeze kwa kuwakemea walioifanya nchi hii kuwa shamba la bibi!
Kuwa ujumla:
1. Jenga taasisi imara na huru katika kutekeleza majukumu yake. Mahakama, Bunge, Serikali na vyombo cha habari. Vyombo hivi vinalinda nchi hata kama watakuja viongozi wabovu nchi haitatetereka sana. Jenga taasisi hizo kabla hujaondoka madarakani.

2. Katiba mpya. Hii ni sheria mama inayoweka mazingira ya usawa kwa kila mwananchi. Tafadhali wateue wabobezi wachache wa katiba hata kama wengine wanachangia toka nje kuliko kuweka watu lukuki hiyo haina tija. Andaa hii kabla hujaondoka madarakani na utaiacha nchi pazuri.

Specific
Uchumi unaendeshwa na sekta binafsi. Serikali isijiingize kufanya jambo lolote ambalo linaweza kufanya na sekta binafsi. Ni hatari kufanya hivyo kwa sababu hasara ni kubwa. Kwanza Serikali inatoa sera na kisha kusimamia na haiwezi kujisimamia na kwa sababu hiyo haitalipa kodi, itatoa huduma kwa kiwango cha chini cha ubora na kwa gharama kubwa zaidi, ajira zitapotea nk. Ni disaster kwa Serikali kuingia huko. Kwa maana hiyo hata ndege tungewaachia sekta binafsi.

2. SGR. Nikupongeze kwa ujenzi wa reli. Tulichelewa sana. Hiyo ni pesa. Ni vyema tutafute pesa tujenge kipande vyote concurrently. Tuboreshe pia TAZARA. Ufike mahali tuone barabara zetu kwa kuongeza ushuru katika usafirishaji wa barabara. Hiyo inawezekana baada ya reli zetu kuwavutia wasafirishaji.

Uvuvi:
Hakuna nchi ulivyozungukwa na maji mengi, na hivyo rasilimali ya samaki kama sisi. Lea sasa bahari yetu wanajua wengine. Rujenge bandari ya uvuvi hata wanaovua huko walete samaki hapo na mapato na ajira tuyapatie hapo.
Sambamba na hilo, kuwa na bandari kunahitaji pia kuwa na meli zetu.

Kilimo kijikite kulima mazao yanayoweza kuuza kwa wingi the ili kufuta pesa kutoka nje. Hivyo kilimo inatakiwa kuhamishiwa kutoka hicho cha kujikimu kuwa cha kibiasha zaidi Ile kukidhi mahitaji ya ubora na wingi kwa soko la kimataifa.

Mchuchuma + Liganga
Peleka Umeme kule, au tumia makaa ya mawe kuzalisha umeme kwa ajili ya kufua chuma pale au watumie huo huo mkaa. Wape jeshi hiyo kazi nafikiri wataiweza. Hata kama wataajiri mtaalamu wa kuwasaidia. Hata reli zilizobaki tutumie hiyo chuma kujengea.

Elimu yetu imo vibaya. Anza na walimu. Bariki sera inayoweka muhimu wa elimu katika jamii. Walimu watokane na wale waliofaulu zaidi kuliko ulivyo sasa. Mishahara mizuri zaidi. Waliopo wanolewe zaidi, wasiofundishika waondolewe.

Tufanye nchi yetu ivutie wawekezaji zaidi. Tuweke sera zinazolenga kukuza uzalishaji siyo jodi, hizo zitakuja zenyewe. Kodi tupunguze ili faida iwekezwe kukuza biashara na mitaji. Tupunguze gharama za kufanya biashara, Umeme bei chini, maji nk.

Public service
Weka professionals wenye ujuzi mzuri laki you ya yote wenye maadili na uzalendo. Professionals watumiwe na wanasiasa kabla ya maamuzi.

Naomba kuwasilisha kwa leo.
 
Huyu mama nimemkubali sana na sijui kwanini sikuwahi kumsikia kabla ya uchaguzi! Naunga mkono hoja ila natamani ateuliwe kuwa mbunge tuu na asipewe uwaziri maana ndani ya serikali ya ccm anaweza akaonekana tofauti kutokana na mfumo.
Ke
Huyu mama nimemkubali sana na sijui kwanini sikuwahi kumsikia kabla ya uchaguzi! Naunga mkono hoja ila natamani ateuliwe kuwa mbunge tuu na asipewe uwaziri maana ndani ya serikali ya ccm anaweza akaonekana tofauti kutokana na mfumo.
Kelli dada
 
Huyu mama nimemkubali sana na sijui kwanini sikuwahi kumsikia kabla ya uchaguzi! Naunga mkono hoja ila natamani ateuliwe kuwa mbunge tuu na asipewe uwaziri maana ndani ya serikali ya ccm anaweza akaonekana tofauti kutokana na mfumo.
Kweli dada
 
ACHENI UJUHA!! Si Alikuwa MWANACHAMA Wa CCM Huyo!!?? Je, ALIPOKUWA Ndani Ya CCM Alikuwa Hawamjui Au Hawamuoni?? Kwanza Kwa KUWAAMBIA WATANZANIA Wanataka KATIBA MPYA Iliyotokana Na MAONI Ya WANANCHI!!! Nani Anayeukubali Msamiati Ndani Ya CCM!!??
Akupata nafasi
 
FISIEM msimu wa JIWE MALAIKAmkuu imeamua kutumia asset za CDM maana wafia chamaFISIEM wote ni mazganyanga tu. hawafai hata kuwasimamisha kugombea ujumbe wa mtaa. kwa wewe NZOGERA ndo kabsaaa hata kufuta vumbi viatu vya bwanaenu ndo utaona kwe picha tu[emoji12] [emoji574] [emoji61]
kuna jembe lingine CDM limeunga mkonokiwunomakaliomiguu ya MALAIKAJIWE juzi tu sasa tusubiri wafia FISIEM kama akiteuliwa FISIEM yeyote kugombea nafasi hiyo mnijuze na mie niwaunge makalioyenyu.
 
Ungemuomba atumie nguvu yake kusimamia haki

Mbagala wameporwa mbunge wao..

Kuna uchaguzi wa mameya wa majiji...asimamie haki walioshinda ndo wapewe

yasije rudia ya manispaa ya Arusha mjini kuhusu uchaguzi wa meya hasa hapa Dar
mmepotea[emoji12] [emoji12] [emoji574] [emoji574]
 
 
Mkuu hapa naona tunapenda kurudia rudia mambo bila kujua chanzo ni nini na utafiti wa kina kufanyika na kuelezea hizo taasisi mnazo zizungumzia zina majukumu gani na kwa vigezo vipi?

Naomba tufafanulie huo uimara na uhuru wa taasisi unavyotakiwa kuwa. Ninavyo jua mimi nchi karibu zote duniani jaji mkuu wa muhimili mahakama huteuliwa na Rais wa nchi, kuna tofauti gani na Rais wetu anavyo fanya? Ulitaka jaji mkuu ateuliwe na nani?

Muhimili mwingine ni Bunge, tuelezee unapendekeza reform gani katika kuwateua viongozi wa Bunge kama Mh. Spika na kadhalika?

Muhimili wa tatu ambao ni serikali Rais ni kiongozi wake mkuu ambaye anasimamia shughuli zote za uendeshaji wa serikali na mtendaji wake mkuu ni waziri mkuu. Unataka mabadiliko gani hapo ili serikali iwe huru na imara?

Kuna vyombo vya habari ambavyo vina milikiwa na serikali na viko vingine vingi ambavyo ni vya binafsi. Sasa hapa ulitaka mambo yaendeje?

Vyombo vya habari vya watu binafsi mbona viko huru? Swala hapa nalo liona ni kwamba vinatakiwa viwe makini katika kutoa habari ambazo zina husu serikali. Visiwe vinatoa habari za uongo ili kuipotosha umma na kuwafanya wananchi kuichukia serikali yao bila sababu na hivyo kuhatarisha usalama wa nchi.
Katiaka nchi ambazo hazina maendeleo makubwa kama Tanzania ni kitu muhimu sana kuangalia media inafanya nini. Media zinaweza zikatumiwa vibaya kama Rais mwenyewe ulivyosema. Pia tusipende kuilinganisha Tanzania na nchi zilizoendelea tunaweza pata shida kubwa, kwani wananchi wengi hawana elimu ya kuwafanya wawe na reasoning character hiyo unayo ifikiria.

Sawa, tunapo zungumzia katiba lazima pia tuzingatie uwepo wake ili kujua kuna manufaa gani kwa nchi na watu wake. Katiba ni paper work ambayo inalindwa na mihimili hiyo mitatu; serikali, Bunge na Mahakma. Kuna nchi duniani hazina katiba kwa mfano England na kuna nchi nyingine kama Kenya ambako katiba ipo na wamejaribu kui-reform kuwa kama ya Amerika, lakini je imesaidia kitu chochote? Mimi naona ukabila bado upo pamoja na katiba mpya.

Tusiwe na Illusion ya kuamini kuwa maandishi peke yake yatatusidia kuwa na viongozi bora kama watu wenyewe hawafuati kanuni zake. Nikupe mfano, CCM inakatiba nzuri sana ambayo ilitengenezwa na waanzilishi wa nchi yetu. Uliona mambo yaliyo tokea kwenye CCM ya awamu ya tatu na ya nne? Kuna mambo ya rushwa yameandikwa humo, kuna maswala ya uteuzi wa viongozi yameandikwa huko, lakini je CCM ya awamu ya tatu na ya nne iliyazingatia hayo? Mafisadi wengi walikuwemo kwenye hicho chama mpaka Rais Magufuli alipo ki-reform.
Naomba tuachane na ndoto za mchana kinacho takiwa hapa mabadiliko ya mind set na maendeleo ya mtu binafsi.

Yaani hii ni theory isiyekuwa na msingi. Of cause serikali inweza kujiingiza katika shughuli ya uzalishaji.
Sikiliza mkuu Ujerumani inamiliki kwa asilimia kubwa Railway yao ya Deutsche Bahn pia kampuni ya magari ya Vokswagen shirika la ndege la Lufthanser na kadhalika kuna hathari zipi zimetokea?

Kipindi cha nyuma serikali ya uiingereza nilisikia ilijaribu ku-privatize Railway yao na shirika la umma la kuzoa taka. Waulize waingereza mambo yaliyowakuta ni yapi? System zao za uendeshaji wa treni mbaya kupindukia. Amerika nako hivyo hivyo. Nenda Kaangalie system ya treni Germany, Sweeden, Switzerland na Ufaransa, utaona tofauti kubwa sana. Hapo ndipo utaona tofauti kati ya private na Parastatal institutions.

Msipende tu kubwabwaja vitu "just for the sake of" kubwabwaja, angalieni mifano iliyopo. Ethiopia Airline mbona ina fanya vizuri? Liko chini ya nani?

Tukija Tanzania Reli yetu ya kati na viwanda vingi ambavyo Rais wa awamu ya kwanza alivianzisha na baada ya serikali ya awamu ya tatu ku-privatize, viko wapi? Na sasa Rais Magufuli ana anza upya tena kuvifufua. Huyu jamaa sio wa kucheza naye ni mzalendo haswa. Amekaa serikalini akisoma matendo yote maovu yaliyo tokea. Anajua nini anafanya na wapi kuna udhaifu.

Hapo hata mimi nakuunga mkono. Hapa simweelewi Rais vizuri. Kitu gani kina mshinda kutawanya pipe lines ya gesi asilia Dar es salaam na miji mingine ambako kuna gesi asilia kama Mtwara, Lindi na kadahalika, watu wakawa na Energy ya kutosha kupikia badala ya kutumia mkaa? Energy sio umeme tu. Makaa ya mawe, Geothermy na kadhalika.

Mimi nashangaa kwa nini nchi kama Tanzania kwa hivi sasa tuna uhaba wa umeme. Tunaweza tuka tumia trilion moja TSHS kuzalisha umeme ambao tukasambaza kwenye miji mikubwa yote kwa kutumia G and S Circles. G stands for Gas Turbine na S stands for Steam Turbine. Gas turbines zinazalisha umeme na kutoa hot air ambayo inaenda kuchemsha maji. Ule mvuke unaotoka kwenye boiler unaenda ku-drive Steam Turbines ambazo zinazalisha umeme kwa Zero Tarif. Steam Turbines hapa hazitumii energy yeyote ile katika kuzalisha umeme. Kwa hali hiyo tunapata umeme zaidi kuliko matumizi ya gas. Yaani unatumia fuel ndogo kuzalisha umeme maradufu.

Mimi saa nyingine nashidwa kuelewa nchi yetu imezalisha wasomi au ma-engineers wa aina gani? Yaani vitu vidogo kama hivi vitushinde, nchi ambayo tuna Gas asilia, tuna makaa ya mawe, tuna uranium na Geothermy. Badala yake tunahangaika na vigenaratos vya wachina na wahindi kweli?

Tuna poteza mabilions na mabilions za fedha kwenye mabarabara na ma-flyovers tunashindwa ku-invest kwenye chip energy? Kwa mfano, kulingana na mahesabu yangu tuna hitaji umeme Tera Watt 10 ambazo ni Mega Watt 10,000.
Kulingana speech ya Rais mwenyewe, amesema umeme wa Stiegler utata Mega Watt 2100 yaani Tera Watt 2.1 na huu tulio nao Tera Watt 1.7, kwa pamoja utafanya Tera Watt 3.8.
Rais Amesema pia kwenye General reserve tuna kama bilioni sita hivi US Dola, katika hizo akichukua bilioni nne tuna Pata umeme wa Tera Watt 5, kwani mtambo mmoja wa G&S-Circle una cost milioni $15 nao utazalisha umeme wa Mega Watt 20. Kwa hiyo katika Tera Watt 5 tutaagiza mitambao 250 ya G&S-Circle. Tayari tuna Tera Watt 8.8. Huu umeme utatuwezesha kusambaza kwenye miji yote mikubwa na kwenye Standard gauge yetu. It is so easy. Hatuwahitaji wachina wala Wajapan. Tunafanya sisi wenyewe. Izingatiwe kuwa wauzaji watatuletea ma-specialist wao wanne au watano mengine yote ni kufuata instractions tu. Watanzania wazalendo tunaweza utaalam tunao. Serikali ituite tu kama iko tayari.

Nami ningemshauri pia kufanya Energy Mix. Asitegemee Stieglers Gorge peke yake, mito na yenyewe inakauka. Global warming inakuja japo kuwa slowly lakini ipo. Itakuja kutukumba siku. Nilivyo kuwa mdogo niliziona picha na clips za mlima Kilimajaro barafu ilijaa, nenda sasa kaone kila kitu kimebadilika! Najua ni vigumu kuuza gesi yetu nje kwa sababu kuna nchi nyingi ambazo zina produce gesi asilia kwa wingi, lakini tunaweza tuka tumia kwa ajili ya atumizi ya local.
 
Mkuu hapa naona tunapenda kurudia rudia mambo bila kujua chanzo ni nini na utafiti wa kina kufanyika na kuelezea hizo taasisi mnazo zizungumzia zina majukumu gani na kwa vigezo vipi?
Hii ina tija gani katika mjadala huu?
 
Naomba tufafanulie huo uimara na uhuru wa taasisi unavyotakiwa kuwa. Ninavyo jua mimi nchi karibu zote duniani jaji mkuu wa muhimili mahakama huteuliwa na Rais wa nchi, kuna tofauti gani na Rais wetu anavyo fanya? Ulitaka jaji mkuu ateuliwe na nani?
Mimi kwenye wasilisho langu sijapinga au kuzungumzia uteuzi wa Jaji Mkuu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…