Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mleta thread umetumwa. Lengo lenu ni namba 1,Prof Muhongo. Mzee wa Machame,Baba wawili,akisikia hilo jina,mhhh!! Kitu kigonga nguo ya ndani. Wauza juice,biashara ya nishati hamwezi
 

Hapana hizi ni chuki binafsi sasa mtu ana PhD ashindwe just kusalimia tu?
 
Kwani Maalim Seif anatekeleza ilani ipi kama Makamu wa Rais wa Zanzibar?

ile ipo kwenye katiba ya Zanzibar, je hii ya kwako ipo kwenye katiba ya muungano?hau ni maaba tu. labda ungemuombea viti maalum tu ili apeleke mchango wake bungeni na kumpa tafu kiongozi mkuu.
 
Msifananishe China na Tanzania kwa kigezo cha lugha wachina wanajiweza sisi walala hoi tu

Mkuu, kwa nini unajivunjia heshima kwa kudharau chako? Kwa tabia za namna hii mtu utajikuta unamkana mzazi wako alikuja kukutembelea kutoka kijijini. Kiswahili ni chetu tukupende, tukikuze mpaka kifike huko unakotaka wewe. Mbona mtoto wa malkia Elizabeti wa Uingereza anajifunza kiswahili na anakipenda? Heshimuni vyenu mheshimiwe...
 
Hapana hizi ni chuki binafsi sasa mtu ana PhD ashindwe just kusalimia tu?

PhD alisoma kwa ujaja ujanja wa kitanzania. Waziri Si ana mchuzi anaandikiwa na wasomi walala wima. Kiukweli tuliaminishwa kuwa anajua lugha nyingi sana kumbe anajua Kisukuma, Kizinza, Kiha, Kijita, Kikerwe,Kisubi etc. Kimataifa bado sana wote tulijionea uwanja wa Taifa. Amesoma Kemia. H20+Mg0=
 
Katika nchi yenye wanasheria waliobobea kashindwa kumpata hata mmoja kamrudisha yule yule aliyekua anashindwa kujibu maswali bungeni atawezaje kuchagua sura mpya kwenye baraza la mawaziri, ccm ni ileile.
 

Naunga mkono Hoja.
 
Ni wazo zuri,nadhani kuna haja ya kulifanyia kazi.Wenzetu katika kututawala wanatumia mbinu mbili soft power na hard power.Hard inatumika kama soft imeshindwa.Language ni soft power na imefanikiwa sana.
 
Ha ha ha! apewe nafasi kwa kipi kwa kwenda kuhudhuria jpm anapewa cheti? hana lolote! labda kama mnatafuta huruma kwa wanaccm mpate kubebwa!
 
Hii ni chuki binafsi.Ni mbaya, kwa kuwa you can never be objective..
 
Kweli kunabaadhi ya uliyo wataja hawastahili hata kidogo kuwemo ila kuna majembe hayata kosa mwakyembe mwigulu lukuvi muhongo Hawa ntasikitika sana wakikosa hapa kazi tu
 
Tanzania ya Magufuli ni ya viwanda ili vijana wengi wapate ajira, wakati ile Tanzania ya Mkapa ilikuwa ya kuviuza viwanda na kuwakosesha vijana wengi ajira. Kila nikimuangalia usoni mzee Mkapa anaonekana kama vile mwenye furaha sana kuliko zile zama za Kikwete. Wasiwasi yangu mimi asije akapeleka mkono wake kwa Rais Magufuli kwa kutumia njia ya uzoefu wake na ugeni wa Rais Magufuli kumshawishi mambo mabaya kama vile kumalizia kuyauza yale mashirika aliyoyabakiza enzi zake kama vile posta, simu, reli, umeme, ndege na DAWASA, na kuzirudisha kwa wenyewe shule za umma zilizokuwa zimetaifishwa na Nyerere kama vile Mkapa alivyofanya kwenye shule za Magamba, Mazengo, Forodhani, n.k ambazo hivi sasa zimegeuka kuwa shule za watoto wa matajiri tu wenye fedha. Kama haitoshi, Mkapa enzi zake alipunguza wafanyakazi wengi sana na kusitisha ajira mpya kiasi cha kusababisha hali ngumu sana katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Kwake mzee Mkapa "paka ni paka" bila kujali rangi yake, alithamini zaidi wageni wenye fedha kuliko wazawa wakati wa zoezi lake la ubinafsishaji wa viwanda, majengo, mahoteli, migodi, n.k. Wazawa tuliachwa tumeduwaa tunangalia mashamba yetu makubwa na viwanda vikigawiwa kwa wageni ambao walishindwa kuviendeleza na kufa hadi leo. Wageni hawa walitumia rasilimali zetu hizo kuombea mikopo mikubwa nje ya nchi ambayo hawakuiwekeza kuendeleza zile mali walizoziweka rehani ili kupata mikopo hiyo.

Dr. Magufuli akili za kuambiwa tafadhali sana uchanganye na PhD yako.
 

Hivi nani aliwapigia kura yani wasingestahili hata kurudii bungeni. Sana sana Mwingulu Nchemba .
 
Kweli kunabaadhi ya uliyo wataja hawastahili hata kidogo kuwemo ila kuna majembe hayata kosa mwakyembe mwigulu lukuvi muhongo Hawa ntasikitika sana wakikosa hapa kazi tu

tatizo nchi hii kuwa kiongozi mbovu ni mpaka uwe fisadi, kuna mengi ya kuangalia, sio uadilifu pekee
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…