Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hivi unaelewa Kiswahili?! Nimesema hawakuombea au nimesema:-
Hata wakati JK alipoenda kutumbuliwa tezi dume, sidhani kama waliokuwa wanamuombea arudi akiwa kwenye sanduku walikuwa ni wengi namna hii!
 
CHADEMA na ZITO KABWE na mafisadi ndio wanaomuombea mabaya rais, Watanzania wazalendo wote wanamuombea mema
Acha mtazamo huo ambao ni jumuishi. Hata ndani ya ccm kuna wengi hawaupendi uongozi wake.

Nakumbuka Kila ccm wakifanya mkutano ilikuwa wakirudi ni bia kwenda mbele. Siku hizi ni njaa kali.

By the way mimi ni chadema na nitampigia kura magufuli kwa sababu anatekeleza yale niliyokuwa nayataka hasa kudhibiti wizi serikalini through miradi isiyoendana na thamani (value for money)
 
Wingi unaupima na nn? Kifo cha Nyerere kiliumbua wengi, jinsi na namna Watz walivyokipokea kifo chake kwa majonzi makubwa .

Uandishi Wa waandishi wenyefursa ya kufurahia tetesi siyo kipimo cha Watz wote
Wingi upi unaohoji wewe?!
 
Hivi unaelewa Kiswahili?! Nimesema hawakuombea au nimesema:-
We jamaa bana, hawakuombea wakati kwenye uzi huo waliombea afe? Umeupitia? Yaan walitaman alivyoanguka angekufa kabisa alafu unasema eti hawajaombea
Nyie ni wasahaulifu na wajinga sana
 
We jamaa bana, hawakuombea wakati kwenye uzi huo waliombea afe? Umeupitia? Yaan walitaman alivyoanguka angekufa kabisa alafu unasema eti hawajaombea
Nyie ni wasahaulifu na wajinga sana
Bado tu huelewi!!! Soma kwa vituo uelewe kilichoandikwa!
 
Kila mtu ataonja mauti...Jiombee maisha marefu wewe na wazazi wako...na yeye ataombewa na ndugu zake




Pia ATAKAE NI QUOTE NI MPUMBAVU ..
 
Tofautisha kuchukiwa na kuombewa mauti!!
Ulimwengu na walimwengu wana mambo sana enzi za yjakaya walimuita dhaifu na kutwa kuchwa vijembe vilitawala, sasa hivi Jpm nananyoosha mambo yaende sawa mameno meeengi , hivyo walimwengu wanataka nini? Yote ni ubatili.
 
Magufuli kaanza kujiombea mabaya mwenyewe kabla mtu yeyote hajamuombea mabaya.

Alivyoanza urais, watu wengi sana walikuwa na matumaini naye, alikuwa na mtaji mkubwa sana wa kisiasa.

Ameenda kuufuja vibaya sana mtaji ule, kwa uongozi wa kiimla, matusi na kuua nzi mmoja kwa mtambo wa nyuklia.

Ukipewa heshima ya kuongoza nchi, jiheshimu.

Magufuli hajiheshimu. Anaendekeza sana shobo.

Granted, Tanzania ilifika pabaya na kulikuwa na haja ya kuisafisha. Na mambo mengine anayofanya Magufuli yanahitajika kufanyika kurudisha nchi kwenye mstari. Lakini ubovu wa Magufuli ni kwamba, hata akifanya jambo ambalo kimsingi ni zuri, atalifanya vibaya, kwa shobo, kwa ubabe usio na lazima, kwa ujinga.

Watanzania wengi wanamkubali kwa sababu hawajaona uongozi. Wana ombwe la uongozi. Hawajui kwamba Magufuli anaweza kufanya mazuri yote anayotakiwa kufanya bila kuweka mabaya anayoyafanya. Watu wana low expectations na ukimsema Magufuli kwa mabaya, kitu cha kwanza wanachoona ni kukuona wewe fisadi. Bila kujali kwamba mtu mzalendo kabisa anaweza kumkosoa Magufuli kwa mabaya anayofanya, akitaka rais wa Tanzania awe na ufanisi zaidi.

Magufuli hahitaji mtu kumuhujumu.

Mtu wa kwanza kumhujumu Magufuli ni yeye mwenyewe.
 
Issue sio kupendwa au kuchukiwa, bali kuombewa kifo! That's beyond na chuki za kawaida kwa mwanadamu! Na wala hakuna anaysema "apendwe na kila mtu" kwa sababu hata huyo Mungu hapendwi na kila mtu!
Hiyo ni kitu cha kawaida tangu zama zile , Hitler alipokufa ulaya nzima ilizizima
 
Ulimwengu na walimwengu wana mambo sana enzi za yjakaya walimuita dhaifu na kutwa kuchwa vijembe vilitawala, sasa hivi Jpm nananyoosha mambo yaende sawa mameno meeengi , hivyo walimwengu wanataka nini? Yote ni ubatili.
Rudi kwenye mada... kwanini wengi wanaonekana kumuombea mabaya zaidi?!
 
Issue sio kupendwa au kuchukiwa, bali kuombewa kifo! That's beyond na chuki za kawaida kwa mwanadamu! Na wala hakuna anaysema "apendwe na kila mtu" kwa sababu hata huyo Mungu hapendwi na kila mtu!
Kuombewa kifo/uhai hakumfanyi mtu afe/aishi. Kila mtu amekuja kwa wakati wake na ataondoka kwa mda wake. Hizi chuki unazoziona wakati mwingine watu wapo kimkumbo tu, nakumbuka hata JK aliombewa mengi ya ajabu wakati anaumwa, lakini leo anaonekana kupendwa na kila mtu.

Simamia unachoamini katika maisha yako, haijalishi ndugu, majirani, workmates nk watakuonaje.
 

Hata ukijaribu kuhamisha mada kwa kuwataja watu wengine haiondoi ukweli wa angalizo la mleta mada. Ifahamike kila mtu anasababu zake zinazompelekea kwenye hiyo chuki. Usitake kupotosha eti wanaochukiwa wanachukiwa na wanaotaka seat zao, kwani wanaotaka seat zao ni washindani wao kisiasa, na hilo ni tofauti na chuki inayoletwa na uonevu. Ukitaka kujua hapa suala sio seat ya rais, rejea idadi ndogo ya wapiga kura kwenye uchaguzi wa SM, na sababu hasa ni yeye kunajisi box la kura kupitia madaraka yake.
 
Ulimwengu na walimwengu wana mambo sana enzi za yjakaya walimuita dhaifu na kutwa kuchwa vijembe vilitawala, sasa hivi Jpm nananyoosha mambo yaende sawa mameno meeengi , hivyo walimwengu wanataka nini? Yote ni ubatili.
Hii hoja ina ukosefu wa mantiki.

Inawezekana kabisa kiongozi mmoja akawa dhaifu sana, na kiongozi mwingine akawa mbabe sana, na kwa hiyo, wote wawiki wakakosa sifa za kiongizi mzuri.

Kwa sababu kiongizi mzuri anatakiwa asiwe dhaifu wala mbabe, awe anajua ku balance mambo.

Sasa mtu kama mimi nikisema Kikwete aliowaya jwa sababu alikuwa dhaifu sana na Magufuli anaowaya kwa sababu ni mbabe sana na tunahitaji kiongozi asiye dhaifu wala mbabe, utajibu vipi?

Kuna ubaya kwa wananchi kukosoa viongozi wao nankutaka uongozi bora zaidi?
 
Mkuu Chige,nafurahi kukuona tena hapa jukwaani.

Hayo mambo uliyoandika hapo juu ni ya msingi sana,si kwa Mh. JPM pekee,bali liwe somo kwa viongozi wote waliopewa dhamana ya kuwatumikia Watanzania,katika utendaji wao wa kila siku wahakikishe hawatengenezi chuki kwa watu wanaowaongoza dhidi yao kiuonevu.

Mimi ni muumini wa "turning point" na pia muumini mzuri wa imani ya kuwa kila binadamu anastahili kupata nafasi ya pili ili aje kujirekebisha, hivyo namwombea Mh. JPM ili ajirekebishe.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…