Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.

You should read between the lines: kama huezi kusoma na kuelewa useme
 
Mkuu asante kwa kumtafakarisha hata kama hajui kutafakari ujumbe umefika!
 
Yani kila siku zinavyoendelea ndivyo unavyoona watu wanatambua mambo na kujua kwamba "Watanzania si wajinga" hata kama "Kuna Watanzania wajinga".

Kua na mdomo haimaniishi uongee kitu ambacho kitakufanya uonekane una mdomo: wangap wametekwa? Just it justify kusema ni lazma ni mtu flan kwa sababu tupo opposites beliefs? kwamba kanisa limechomwa moto just it justify kwamba ni waislam wanahusika? just because it happend back?
 
Ukishaanza kuongea habari za nchi kumuhumitaji mtu, mpaka hapo usha fail tayari.

Nyerere alivyokuwa katika mkutano na waandishi wa habari Kilimanjaro Hotel, kuelekea uchaguzi wa 1995, wakati huo Mrema yuko juu, waandiahi walikuwa wanawashwa sana kumjadili Mrema.

Nyerere akawapa kanuni kubwa sana waandishi wale. Akawaambia mimi sipo hapa kumjadili mtu, nipo hapa kujadili sifa za uongozi. Kama mnataka mjadala wa mtu niambieni nigeuze safari kurudi nyumbani.

Alielewa. Ingawa Mrema alikuwa juu sana kuelekea uchaguzi wa 1995, kwa sasa Mrema ni kichekesho

Nyerere alielewa kwamba unavyozidi kujadili mtu, ndivyo unavyozidi kujifunga kwenye udogo. Ukitaka kujadiki kwa uoana, jadili kanuni.

Eleanor Roosevelt alisema "Small minds discuss people, average minds discuss events, great minds discuss ideas".

Nyerere alijua hilo. Alikaa nao hao kina Roosecelt tangu Tanganyika haijapata Uhuru akajua haya mambo. .

Mwaka 1959 Nyerere alialikwa kwenye kipindi cha Roosevelt, viseo ipo Youtube hapa
Tujikite kwenye kujadili dhana, mijadala ya kuwaangalia sana watu badala ya dhana itatufilisi kisiasa na kiuchumi.
 
You should read between the lines: kama huezi kusoma na kuelewa useme
Hapa umeshindwa kujibu hoja na umekimbilia katika obfuscation.

JF hatuna daftari kenye mistari.

Sasa nisome kati ya mistari gani?
 
Hapa umeshindwa kujibu hoja na umekimbilia katika obfuscation.

JF hatuna daftari kenye mistari.

Sasa nisome kati ya mistari gani?

kama huelewi no need for me to explain anything to you zaidi:
 
Daaah jana nilikua nafanya kazi ya kuswitch mda wote from jf to twitter and vice versa aiseee haters wa boss ni wengi sana mitandaoni

Watu wanakataa bure tu, lakini hawa wa mitandaoni ndiyo reflection ya hali halisi kwa ujumla wake....

Kinachomponza Bwana Magufuli kwa ujumla ni kutawala watu kwa MAGUVU tu huku akiwa ameitupa BUSARA na HEKIMA ndani ya shimo la choo....!!

Jamaa si MVUMILIVU, hana BUSARA wala HEKIMA....

Kuna ishu zingine zinahitaji maamuzi ya HEKIMA na BUSARA tu lakini yeye utamwona anaripuka mithili ya volcano huku akidhani kuwa ametatua tatizo hilo lakini hali halisi ikiwa kinyume chake.....!!

Kuji - mwambafai siku zote hakujawahi kuishinda BUSARA na HEKIMA. Tabia hii si ASILI ya Mungu aliyetuumba bali ni tunda la roho wa shetani.....
 
Mkuu bahati mbaya sana siasa za Afrika hazitoi mwanya kwa mfumo kushika hatamu, halafu mtu anayekuwa kiongozi afuate misingi ya mfumo uliopo...

Mifano halisi ni namna wagombea wa ngazi mbalimbali za kupigiwa kura wanavyopatika sio upinzani sio chama tawala...

Kilichobaki na ambacho kimekuwa kikifanyika ni kutafuta watu wenye visions zao binafsi, wanakaimishwa uongozi...

Yaani nchi za kiafrika zimekuwa kama timu inayotegemea mchezaji fulani awepo uwanjani...

 

Kwa taarifa yako huku mitandaoni ndio pekee unaweza kuonyesha hisia zako hasi dhidi ya rais. Kwani rais wetu Kawa rais kwakuwa kachaguliwa na watanzania wote 55m? Hivi ukitaka kujua una malaria unatoa damu yote mwilini kwenda kuipima? Kwa hiyo kwa huu utetezi wako unaamaanisha wote wanaomkubali hawatumii mitandao, na wote wasiomkubali wanatumia mitandao! Rekebisha utetezi wako boss.
 

Uko sahihi sana, mahali pekee unapoweza kupata maoni na hisia halisi juu ya kukubalika kwa rais ni humu mitandaoni, maana nje ya mitandao ni kutafuta shida toka kwa wapambe wake. Uandikishaji wa daftari la uchaguzi SM umeakisi michango iliyopo mitandaoni.
 
Sasa mtu mmoja akifariki ghafla, na hakuna mfumo endelevu, itakuwaje hapo?
 
Hao unaowaita wanaelewa walishawahi kuifanyia nini nchi hii cha kustua zaidi ya kupiga?

Wanaelewa au wamelewa?

Bado tupo tupo sana...
 

Mkuu nimependa mchango wako, tatizo naliona kwa wanasiasa wenyewe, wao ni kikwazo cha kupatikana mgombea binafsi, laiti wangeachia njia hiyo kila mtu angetekeleza hisia zake binafsi. Sio huku ilani ya chama A inasema hivi, huku kiongozi anafuata anayotaka yeye.
 
Sasa mtu mmoja akifariki ghafla, na hakuna mfumo endelevu, itakuwaje hapo?
Nani kasema hakuna mfumo? Alifikaje huyo moja kama siyo mfumo uliomweka? Mmekula ya wapi?

Tupo wengi sana na bado tunaendelea mpaka generation nne zijazo kuzika kabisa nia yeyote ovu kutoka kwa yeyote...
 
Nani kasema hakuna mfumo? Alifikaje huyo moja kama siyo mfumo uliomweka? Mmekula ya wapi?

Tupo wengi sana na bado tunaendelea mpaka generation nne zijazo kuzika kabisa nia yeyote ovu kutoka kwa yeyote...
Umefuatilia mjadala au unarukia tu?

Kama katiba ya nchi inatoa haki kwa watu kufanya mikutano ya kisiasa, halafu anakuja mtu mmoja tu na kukataza mikutano ya kisiasa, kinyume na katiba, hapo mfumo uko wapi?
 
Dar, ilikikataa chama cha mapinduzi, mikoani walikikubali chama cha mapinduzi.

Mwisho Wa siku matokeo unayajua. Mijini ni ujuaji tu , vijijini ni waamuzi Wa vitendo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…