Kinachoendelea hivi sasa inabidi kiwe funzo kwa Rais J.P Magufuli!
JK alipoleta msamiati wa "kujimwambafai" tu, mitandao ikaripuka kwa vigelegele! Magazeto karibu yote yakaifanya habari hiyo kuwa ukurasa wa mbele!
Si tu kwa mstari wa mbele, lakini karibu yote yaliashiria kana kwamba huyo aliyeambiwa aache kujimwambafai ni JPM!
Hata wana-CCM wenyewe, kama vile Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ali Hapi, nae akaamini kabisa anayeambiwa aache kujimwambafai ni Rais Magufuli!
Kwanini hadi wana-CCM na wenyewe waamini JK kamsema Magufuli wakati yeye alisema Viongozi waache kujimwambafai?!
Lau kama kauli ile ingetamkwa na Mkapa wakati JK yupo rais, sidhani kama wananchi wangemshuku JK kwamba ndie anajimwambafai!!
Sasa kwanini JPM ionekenane ndie anajimwambafai?! Kumbe hata wana-CCM wenyewe wanafahamu kwamba Magufuli anajimwambafai!
Limekuja hili sasa!
Hivi sasa zinapoonea habari juu ya afya JPM, bila kujali kama ni za kweli au za uongo, kwa mata nyingine, mitandaoni kumeibuka shangwe, huku wengine wakisema wazi "...atangulie safari ya milele!"
Hata wakati JK alipoenda kutumbuliwa tezi dume, sidhani kama waliokuwa wanamuombea arudi akiwa kwenye sanduku walikuwa ni wengi namna hii!
Sasa ikiwa hadi wananchi anaowaongoza miongoni mwao kuna wanaouuombea afe, basi hilo ni tosha kumfanya ajitafakari unless!!
Generally speaking, kwa Tanzania inaonekana jamii iliyopo Mtandaoni ndio jamii yenye uelewa zaidi, hususani walio Jamiiforums na Twitter!
Kwa maana nyingine, miongoni mwa wale wanaoonekana kuwa na uelewa zaidi, watafanya sherehe wakisikia rais wao ame-rest in peace!!
Na ukweli ni kwamba, ni mpumbavu na punguani tu ndie anaweza kudiriki kusema hawa wanaomuombea JPM mabaya ni mafisadi! Hao mapunguani tayari tumeanza kuwasikia wakiongea hizi kauli za kipunguani!