Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Nyalandu, Kingwangala, Slaa, Nape na Makamba wote ni wasanii kama JK
 

Sawa...
Lakini kwa upande mwingine tunaangalia waziri au viongozi kwa ujumla wawe mfano kwa walio chini yao.
Wawe mfano katika kuchapa kazi lakini pia katika kubana matumizi ya fedha za umma.
Naamini kabisa sio mawaziri peke yao wana kazi nyingi, wapo watendaji wengi chini yao na pengine wengi wana kazi nyingi kuliko mawaziri.
Na naamini pia waziri mchapa kazi anaweza kuwa productive vya kutosha akiutumia mda wake akiwa ofisini vyema.
Lakini kama ni suala la kuutumia mda wa safari basi sio vibaya waziri akaonyesha mfano wa uzalendo kwa kuajiri dereva wake kama ulivyoajiri wewe...
 
Mi namuomba mh rais magufuli atembelee jeshi la police kitengo cha usalama barabara hawa jamaa wametufanya miradi huko barabarani kwa kweli utrafki ni zaidi duka la jumla
 
Reactions: nao
Magufuli tembelea mahakama kuu ukaone maajabu.

Watu wanateseka mno, jaji anaahirisha kusoma hukumu anavyotaka hata mara saba.

Hukumu ikitolewa haitekelezwi.Mwanasheria Mkuu anatumia ujanja wa kiufundi kunyima wananchi haki hasa pale taasisi za serekali zinaposhitakiwa.

Ngoja tuachie hapo ni shida, kesi inazungushwa miaka kumi na zaidi mpaka wadai haki wote wafe.
 
Sijajua kama muhimili huu nao ataukomalia, maana hata huko ndo rushwa imetamalaki! watu wamefungwa wasio na hatia!, kama huna hela ujue jela ya kwako!, kuna likiwanda la WAZO HILL LIMETIRIRISHA MAJI KWENYE MAKAZI YA WATU, KWAKUWA WANA HELA HAWASIKII! YAANI OVYO OVYO TU!
 
Sijui kwa nini wafanyakazi wengi serikalini wana njaa
 
Watu siku hizi hawendi ofisini kufanya kazi! Wanaenda kupiga dili. Mahakimu na majaji ni dili tupu!! Jaji mmoja alisikiks akisema, " Kwanini sisi hatutaki pesa? Hata kwetu wanasheria pesa ni tamu pia!!"
 
Dr. Grace Ndalichako - Elimu

Ludovic Uto - Fedha

Anne Kilango - Jinsia na watoto

Barozi Amina Salum- Mambo ya nje

Palamagamba Kabudi - Sheria
 
Sio siri kuwa CCM ni chama kilicholea na kuhifadhi ufisadi nchini.

Kupata mtu mwadilifu ndani ya CCM ni sawa na kocha kutafuta wachezaji wa kusajili MOI.

Chama kilihangaika kumpata mgombea urais mwadilifu kikakosa kikabidi kumpata mwenye nafuu kidogo,na kumnadi kwa pesa nyingi za kukufuru, na kufanikuwa kumchagulusha.

Sasa tujiulize huyo waziri mkuu na mawaziri wasio na kashfa ndani ya chama chetu watapatikanaje?

Nimesikia majina yanatajwatajwa lakini yote yana madoa ya ufisadi. Subiri wateuliwe uone jinsi watu watakavyoanza kuweka hadharani madudu yao.
 
Deo fili angekuwepo angepewa u Prime minister.....sijaona mtu mwenye committment ya magufuli
 
Dr. Grace Ndalichako - Elimu
Ludovic uto - Fedha
Anne Kilango - Jinsia na watoto
Barozi amina salum- mambo ya nje
Palamagamba kabudi - sheria

Mbona bungeni wameenea, kuna vijana kibao, mtu kashindwa kuwatumikia wananchi elfu arobaini milioni arobaini atawaweza?
 
Katibu Mkuu WIZARA YA UCHUKUZI alitoa ahadi hewa alipo kwenda kuwaona viongozi wa PPF kuhusu utekelezaji amri ya mahakama kukamata mali za ATCL ili kupata pesa kuwa lipa wastafu walio kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ndege ambao michango yao ya miaka kadhaa haikupelekwa PPF japo walikatwa toka mishahara yao. PPF walishinda kesi walioishitaki management ya ATCL kwa kutokupeleka michango ya wastaafu hao.

Kesi iliyo toa amri kukamata na kuuza mali za ATCL kupata pesa kuwa lipa wastaafu wasio kuwa na kosa ili kupata haki yao. Uongozi ATCL ulipeleka amri hiyo wizara mama na Katibu Mkuu akaenda kuwaona viongozi wa PPF ambako aliahidi kulipa kabla ya mwisho wa mwezi March, 2015. Hadi leo hii haja lipa akikaidi na kudharau amri ya mahakama.

Hii inaonyesha jinsi gani wazee wailotumikia taifa wanavyo nyanyasika punde wanapo staafu. hadi sasa wengine wamefariki na waliopo hawa jui watalipwa lini kwa kuwa wapo walio staafu mwaka 2010 na haijulikani kama watalipwa arrears kwa miaka hiyo waliyo kosa haki yao hadi leo au kesho.
Mheshimiwa Raisi wachukulie hatua viongozi wana lindana kimaslahi na kuwatesa walio staafu kwani hii inafanya baadhi ya waajiriwa wa sasa kuchukua chao mapema kukataa adha kama hii wapatayo wazee hawa walio kuwa ATCL.
 
Jamani hata Grace Ndalichako!!!?
 
Changamoto kubwa kwa Magufuli iko hapo!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…