Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.

Kwa hoja yako hiyo Tanzania haina haja ya kujiita kisiwa cha amani kama unaifananisha na nchi ulizozitaja.
 
Kama kuna kitu kinachokera wananchi wengi, hususan walalahoi ni kuona waheshimiwa wabunge wakijipangia posho na marupurupu yao kwa viwango vya kufuru.

Kazi ya mbunge ni kuwawakilisha wananchi wake bungeni,na Kwa kufanya kazi hiyo analipwa mshahara kila mwezi. Kinachostaajabisha ni kuwa wakati mbunge anafanya kazi aliyeiomba na kulipwa mshahara kila mwezi, eti analipwa malipo mengine kwa jina la posho la vikao vya kufanya kazi anayolipwa kila mwezi tena kwa kiwango cha ambacho kwa siku ni kikubwa Zaidi ya anachopata mtumishi wa umma wa ngazi ya chini kwa mwezi. Hiyo ni kufuru na Mungu anashuhudia.

Kwa vile umeanza kazi kwa gia kubwa inayowafanya wananchi waanze kujenga matumaini mapya, Rais wetu wa awamu ya tano utakumbukwa kwa vizuri katika historia ya nchi hii kama utaondoa wizi na unyonyaji wa fedha za umma kwa kudhibiti viwango vya posho hivyo ili viendane na hali halisi, na vilingane na watumishi wengine wa umma.Katika mukhtadha huo huo tupia macho pia posho za wakurugenzi wa mashirika na taasisi za serikali ili nazo zilingane na hali halisi, na utatukosha sana kama ukiridhia wabunge wasichaguliwe kuwa wajumbe wa bodi za mashirika na taasisi za umma, huku ukitafakari matakwa ya walio wengi ya kupendekeza mawaziri wasitokane na wabunge, ili kuliwezesha bunge kusimamia vizuri serikali iliyopo madarakani..
 
Nimefurahishwa sana na maamuzi yako ya mapema tu baada ya kuingia Ikulu. Kitendo cha kufuta ununuzi wa magari mapya ya mawaziri na kusimamisha safari za nje, kweli umeona mbali. Mimi ningeshauri nusu ya safari za nje uzifutilie mbali na hizo kazi zifanywe na mabalozi wanaowakilisha Tz. Pesa zitakazopatikana kwa kubana matumizi hayo zielekezwe kujenga nyumba za waalimu, kujenga madarasa, zielekezwe kwenye mikopo elimu ya juu, huduma za hospitali n.k. Pia ningeshauri magari yanayonunuliwa kwa mawaziri, makatibu wakuu na majaji yasinunuliwe ya gharama kubwa kama haya yanayonunuliwa sasa hivi, kwa nini gari ya zaidi ya Tshs. 200 hadi 300m/= na lina 4wheel drive wakati viongozi hao muda mwingi wako mjini kwenye lami?
 
Mkuu inasikitisha sana na sijui kwa nini JK aliruhusu suala hili ovu liwepo Tanzania wakati watu hawana dawa, elimu hovyo kabisa, maji shida. Naunga mkono wazo lako japo Mhe Rais keshaanza kulitekeleza tunaomba aungwe mkono.
 
Mh umekuwa ukisisitiza kwenye kampeni "hapa ni kazitu#" na kupambana na ufisadi. Ushauri wangu ni huu hapa:

1) Huduma za jamii ziboreshwe ili wenye huduma hizo binafsi ama wafuunge au washushe gharama zao ili watanzania wengi waweze kumudu. Huduma hizo ni kama vile madawa hospitali, vitabu mashuleni, nk.

2) Ufanyike utafiti kuhusu njia kuu za ufisadi ili mianya, mirija na bomba zake zifungwe. Wahusika, baada ya muda mfupi, watajifunga wenyewe badala ya kupitia njia ya mahakama ambayo ni ndefu yenye upotevu wa muda na pesa.

3) Ajira za vijana: Mikakati na juhudi zichukuliwe kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali (km kilimo, mifugo, uvuvi), kutoa huduma (km gereji, saloon, migahawa) na sanaa. Makumpuni yahamasishwe kuvisaidia hivi vikundi kwa mitaji au mashindano. Matokeo yake yatakuwa ni zaidi ya ajira kwani jamii itapata bidhaa na huduma zilizo bora na nyingi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA na UONGOZI WAKE MPYA
 
Safi sana Mungu amutanguli kwa kila njia aweze kutenda vyema
 
Salaam,
Kama tunavyofahamu kuwa mchakato wa uchaguzi umeisha na bila shaka kuna wabunge ng'ang'ari na maarufu walioangushwa.
Na kama tunavyojua Rais ana mamlaka kikatiba ya kuwateua jumla ya wabunge kumi. Kutokana na uchapakazi wao,ningeomba HURUMA ya mheshimiwa iwapitie wabunge wafuatao;
1. Aggrey Mwanry
2. Ezekiel Wenje
3. Viccent Nyerere
4. Anne Kilango
5. Fenella Mukangara
Naomba huruma iwapitie wapate walau nafasi ya kuteuliwa.

NAWASILISHA.
 
Huruma za nini?
ungesema awateue kwa kuwa ni viongozi wazuri sio suala la kuwaonea huruma.
Akishaanza kuendesha nchi kwa kuwaonea watu huruma nchi haitaenda.
 
Ongeza na David Kafulila listi ikae vizuri.Ndo mbunge aliyekuwa kinara bunge lililopita.Rais wetu kama ana nia kweli ya kupinga ufisadi amteue kafulila kuwa mbunge.Nadhani rais anamjua vizuri tu jamaa.
 
Uongoz mzur hauitaji huruma peke yake,hao uliowataja si wema..hawakutambua kuwa tupo zaidi nje tunaishi maisha magumu...wao waliona ufahari sn..kama mwisho wao hautafika...ulikuwa ukiomba kupata apointment na mmojawapo wapo hapo hata km una namba yake mkononi...hatoi ushirikiano kabisa..wanadhalau sn...hawa watu...magufur naomba usitoe huruma kabisa....km una huruma wape wapa kabisa..wengine ambao mimi binafs nimewahi kuomba appointment kupitia simu zao za mkononi na hawa kutoa ushirikiano..wao udhani kila mmoja ambae hayuko kwenye system hana akiri,ni maskini,ni hovyo..mojawapo alikuwa Kagasheki, prof.tibaigana, kamala,..na wengi wengi. Nawaombea maisha magumu sana...tufike paala tuamini kuwa nafasi uliyokalia kama cheo wapo zaidi ya milioni moja wanaoweza kukaaa vizur zaidi kiutendaji. Tuondoe hii dhana ya huruma huruma kwenye maslahi ya umma jamani.HATUTAFIKA.
 
Acheni na wengine waoneshe makucha yao. hao nao wametosha. huruma hakuna tena.
 
Ongeza na David Kafulila listi ikae vizuri.Ndo mbunge aliyekuwa kinara bunge lililopita.Rais wetu kama ana nia kweli ya kupinga ufisadi amteue kafulila kuwa mbunge.Nadhani rais anamjua vizuri tu jamaa.
Kupinga Ufisadi gani "Unafiki tu".Unapinga Ufisadi halafu unaungana na FISADI LOWASSA.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…