Mhe Rais Magufuli,
Ni mapema mno kusema lolote kwa sasa LAKINI naomba niseme in advance. Tunajua kuwa Mhe. Kafulila amefungua kesi Mahakama Kuu huko Tabora kupinga matokeo ya ubunge katika jimbo lake. Endapo hatafaulu katika rufaa hiyo, nakuomba kwa kutumia mamlaka yako ya kikatiba uturudishie kijana huyu katika Bunge letu tukufu. Kila Mtanzania anaweza akakumbuka mchango wake kwenye Bunge lililopita.
Ninakuombea mema katika nafasi yako hiyo mpya na nikupongeze kwa ulivyoanza kazi.
Mtiifu,
Oikos
Washenga wa kafulila mwambieni akauze mawese.hakuna viti vya bure sasa
Haka ka jamaa hakafai japo kalileta hoja ya msingi lkn kitendo cha kuwatukana wananchi wake.
Hafai.
Mfano Rais wasitaafu kafa Nyerere tu wengine wapo wanapiga pesa kiulaini.
Duu, hawa wazee waachwe. Nao mnataka wamlikwe!!!
Wakala ndiyo nani?
Kafulila kateketezwa na Zito baada ya kumwomba ahamie ACT akagoma wakatibuana wakawa maadui wakubwa ndipo Zito akala njama na ccm za kumhujumu kwa njia za kimafia ilkiwemo Goli la mkono.