Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Washenga wa kafulila mwambieni akauze mawese.hakuna viti vya bure sasa
 
Mhe Rais Magufuli,
Ni mapema mno kusema lolote kwa sasa LAKINI naomba niseme in advance. Tunajua kuwa Mhe. Kafulila amefungua kesi Mahakama Kuu huko Tabora kupinga matokeo ya ubunge katika jimbo lake. Endapo hatafaulu katika rufaa hiyo, nakuomba kwa kutumia mamlaka yako ya kikatiba uturudishie kijana huyu katika Bunge letu tukufu. Kila Mtanzania anaweza akakumbuka mchango wake kwenye Bunge lililopita.
Ninakuombea mema katika nafasi yako hiyo mpya na nikupongeze kwa ulivyoanza kazi.
Mtiifu,
Oikos


Haka ka jamaa hakafai japo kalileta hoja ya msingi lkn kitendo cha kuwatukana wananchi wake.
 
Haka ka jamaa hakafai japo kalileta hoja ya msingi lkn kitendo cha kuwatukana wananchi wake.

Jaji werema ana hasira naye hadi leo huku mama Tibaijuka na mzee wa vijicent Chenge na Rugamalila na wana-Escrow wote wakihakikisha kuwa wanampa Pesa nyingi Zito awasaidie kumteketeza apotee kwenye Ulingo wa Siasa.
 
you are very right,she must be a wife of Mr, Kiyabo.Vinginevyo uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana kwa kumuona tu kiyabo ndiye anayeweza.Au ndyo ile kitabia cha kihaya haya.
 
Unataka aje wamfanyie figisufigisu uzandiki bin fitna mwishowe ajutie kurudi bongo kama yule dr mtaalam wa magonjwa ya moyo (asili kanda ya ziwa) aliyepoteza maisha yake kisa kurudi bongo
 
Hoja ina utamu ndani yake ila mbinu zake sikubaliani nazo. Nakiri kuwa Kafulila alifanya kazi nzuri sana kwa nchi ila kwa waliomtuma ama hawakumuelewa au aliwapuuza. Apatane nao. Kaenda mahakamani,akishinda uchaguzi utarudiwa na waajiri wake watathibitisha wanachotaka maana yaliyopo hamyakubali. Akishindwa sense Monduli amuulize tajiri mpya afanyeje? Magufuri atamruhusu kuomba kazi ya kiutendaji anayoiweza. Siasa muda umepita kwa JPM,hapa kazi tu.
 
Kafulila anaweza kuwa mmoja wa vijana bora katika medani za siasa kwa manufaa ya taifa, lakini ikumbukwe kuwa wanaokuchagua kurudi bungeni ni wananchi wa jimbo lako na si watanzania wote. Kibaya zaidi ni pale unapowaambia wapiga kura wako uwezo wao umeishia kuuza mawese.
 
Hongera sana kwa hatua unazochukua katika kubana matumizi.

Nakumbuka enzi za mwl Nyerere akiwa Rais alitamka kutokuongeza mikoa na wilaya kwa maana ya kuboresha huduma kwa wananchi, cha kushangaza uncle Ben akafungulia mlango na sasa mikoa na wilaya inaanzishwa kihisani tu.

Hebu tupia jicho hapo mheshimiwa.
 
Awali ya yote nitoe pongezi zangu za dhati yaani toka sakafu ya moyo wangu kwa kazi nzuri uliyoanza nayo. Kazi ya kuturudisha kwenye uzalendo na uwajibikaji. Mheshimiwa Tafadhali rekebisha tofauti ya kipato Na marupurupu ya watumishi Wa umma.

Serikali kuu Mishahara ni midogo ukilinganisha na wakala wa Serikali. Japo sifa za elimu zinafanana na hata kuwazidi lakini hawa wakala Mishahara yao inatisha. Hii imetokana na mamlaka waliyopewa ya kukusanya kodi na kujilipa wanavyotaka. Nature ya kazi ndio imetupeleka serikali kuu na wengine wakala.

Ninaomba wenye michango waboreshe hili ombi langu kwa MH Rais.
 
mkuu wenzako wanataka waongezewe then wewe unasema tena wapunguziwe??? cost of living zimepanda.
 
Kafulila kateketezwa na Zito baada ya kumwomba ahamie ACT akagoma wakatibuana wakawa maadui wakubwa ndipo Zito akala njama na ccm za kumhujumu kwa njia za kimafia ilkiwemo Goli la mkono.

unaushahidi dogo, au unadhani uko salama kubwabwaja nyuma ya keyboard?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom