Ni kweli kabisa Okonkwo Jr,fedha hizi mpya wakati zinaingizwa ktk matumizi halali,wahusika wakuu hasa Gavana Beno Ndulu alizipamba na kuzipigia chapuo sana kwamba zina ubora wa hali ya juu,haziwezi kurudufiwa kutokana na features za kiusalama na utambuzi,kwamba kampuni iliyopewa kandarasi hiyo ni moja ya makampuni yaliyobobea ktk fani hiyo,muda mchache baada ya kuingia sokoni zilikamatwa mamilioni ya fedha bandia pale mpakani Tunduma,ghafla zikasambaa kwenye minada ya mifugo ktk mikoa mbalimbali waliko wafugaji,ilifikia baadhi ya wananchi wakawa hawazipokei tena ktk biashara hadi alipwe fedha ya Zamani@ Mikeka.Noti mpya kama za mia tano zikawa zinachuja rangi na kutepeta,ule ni Uhujumu Uchumi kabisa,wale wote waliohusika na kuidhinisha kandarasi ile walipaswa kukamatwa na kuhojiwa,iweje zile noti za Zamani za enzi ya Mzee Mkapa ziwe na ubora hadi leo?Mh rais bila kumumunya maneno hapo BoT pana Jipu linatakiwa kukamuliwa hadi Damu itoke ili kuondokana na AIBU HII YA NOTI ZILIZOPO CHINI YA KIWANGO.