Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hakika mkuu,mi nakiri kuwa nilikuwa nampinga sana jamaa lakina kwa sasa namkubari kwa 99.99%
Nilikuwa namkubali Magufuli toka kitambo sema CCM Ndo kichefuchefu kwangu.Na kwa vile Magufuli yupo ndani ya CCM.basi naona kama Imani yangu inazidi kuwa ndogo kwake
 
Tunaunga mkono mpango wako wa kubana matumizi ya serikali ili fedha hizo zikatumike katika kuwasaidia watanzania.
Kuna kundi ambalo ningependa serikali yako kwa kushirikiana na bunge iliangalie,hili ni la wastaafu wa ngazi za juu ambao hata baada ya kustaafu wanaendelea kulamba asilimia 75 ya mshahara wa aliyeko madarakani.Watu hawa wakiwa madarakani hugharamiwa kila kitu na serikali hivyo posho zao na mishahara hawaitumii kabisa na hawakatwi kodi.Baada ya kustaafu wanapata mafao makubwa lakini pia huendelea kulipwa asilimia 75.

Mh Rais,watu hawa ni wengi kwa sasa na hawafi mapema kiukweli,baada ya kustaafu wanaishi zaidi ya miaka 30 na hii ni kutokana na maisha mazuri na huduma bora za afya wanazopata wakiwa madarakani na baada ya kutoka.Wao wakiugua hutibiwa nje na familia zao.

Kutokana na hilo napendekeza baada ya wao kustaafu waendelee kulipwa asilimia 10 tu ya mshahara wa aliyeko madarakani kutoka asilimia 75.
in a long run tutakuwa tumeokoa pesa nyingi sana!
 
Ni kweli kabisa Okonkwo Jr,fedha hizi mpya wakati zinaingizwa ktk matumizi halali,wahusika wakuu hasa Gavana Beno Ndulu alizipamba na kuzipigia chapuo sana kwamba zina ubora wa hali ya juu,haziwezi kurudufiwa kutokana na features za kiusalama na utambuzi,kwamba kampuni iliyopewa kandarasi hiyo ni moja ya makampuni yaliyobobea ktk fani hiyo,muda mchache baada ya kuingia sokoni zilikamatwa mamilioni ya fedha bandia pale mpakani Tunduma,ghafla zikasambaa kwenye minada ya mifugo ktk mikoa mbalimbali waliko wafugaji,ilifikia baadhi ya wananchi wakawa hawazipokei tena ktk biashara hadi alipwe fedha ya Zamani@ Mikeka.Noti mpya kama za mia tano zikawa zinachuja rangi na kutepeta,ule ni Uhujumu Uchumi kabisa,wale wote waliohusika na kuidhinisha kandarasi ile walipaswa kukamatwa na kuhojiwa,iweje zile noti za Zamani za enzi ya Mzee Mkapa ziwe na ubora hadi leo?Mh rais bila kumumunya maneno hapo BoT pana Jipu linatakiwa kukamuliwa hadi Damu itoke ili kuondokana na AIBU HII YA NOTI ZILIZOPO CHINI YA KIWANGO.
 
Pole mkuu kama hujui,pesa inapochakaa huwa kunadawa zinawekwa na kuwa reprented tena,sasa hizi pesa kutokana na kuchakaa mapema ,zinahitaji gharama kubwa kuwa reprented mara kwa mara,nadhan umeelewa mkuu.

Muongooo toka na hadidhi zako za vijiwe vya bange
 
Tunaunga mkono mpango wako wa kubana matumizi ya serikali ili fedha hizo zikatumike katika kuwasaidia watanzania.
Kuna kundi ambalo ningependa serikali yako kwa kushirikiana na bunge iliangalie,hili ni la wastaafu wa ngazi za juu ambao hata baada ya kustaafu wanaendelea kulamba asilimia 75 ya mshahara wa aliyeko madarakani.Watu hawa wakiwa madarakani hugharamiwa kila kitu na serikali hivyo posho zao na mishahara hawaitumii kabisa na hawakatwi kodi.Baada ya kustaafu wanapata mafao makubwa lakini pia huendelea kulipwa asilimia 75.

Mh Rais,watu hawa ni wengi kwa sasa na hawafi mapema kiukweli,baada ya kustaafu wanaishi zaidi ya miaka 30 na hii ni kutokana na maisha mazuri na huduma bora za afya wanazopata wakiwa madarakani na baada ya kutoka.Wao wakiugua hutibiwa nje na familia zao.

Kutokana na hilo napendekeza baada ya wao kustaafu waendelee kulipwa asilimia 10 tu ya mshahara wa aliyeko madarakani kutoka asilimia 75.
in a long run tutakuwa tumeokoa pesa nyingi sana!

Good point! eti hawafi haraka he he!!
 
Wenye kufaidi hii mipesa wakikwata na Magufuli lazima watamhujumu sana hadi wamtoe ikulu uchaguzi ujao.
 
Duh kama sumaye ana uhakikika wa kuish miaka 35 ijayo kama mungu atamsaidia
 
Magufuli akiminya pesa zao lazima watamhujumu sana, ebu Magufuli komaa na hawa wazee tuone kama utaweza kuwapunguzia ulaji wao na ukaendelea kutawala bila shida.
 
wewe jamaa kwahiyo ulitaka wafe???? anyway u have good idea.
 
wewe jamaa kwahiyo ulitaka wafe???? anyway u have good idea.

Hapana,nasema tu life span yao ni kubwa kwahiyo hili suala liangaliwe upya!Wapunguziwe malipo ya baada ya kustaafu,wanakula hela nyingi sana!
 
Hata hivyo Maghufuli kama uko seriou kwa sababu hata watangulizi wako walianza hivi hivi
1.Tutajie mali zako na madeni yako sasa ili siku ukitoka utueleze umetoka na nini
2.Pia ndani ya siku sitini waliobeba fedha kwa viroba pale STANIBIC zile za ESCROW watajwe majina yao na wafunguliwe kesi haraka.
3.Singasinga wa ESROW awe wa kwanza kuhudhuria kesi ya mafisadi shahidi awe Mh Kaulila
3.Mh Kafulila alidishiwe Ubunge wake haraka
 
Mhe Rais Magufuli,
Ni mapema mno kusema lolote kwa sasa LAKINI naomba niseme in advance. Tunajua kuwa Mhe. Kafulila amefungua kesi Mahakama Kuu huko Tabora kupinga matokeo ya ubunge katika jimbo lake. Endapo hatafaulu katika rufaa hiyo, nakuomba kwa kutumia mamlaka yako ya kikatiba uturudishie kijana huyu katika Bunge letu tukufu. Kila Mtanzania anaweza akakumbuka mchango wake kwenye Bunge lililopita.
Ninakuombea mema katika nafasi yako hiyo mpya na nikupongeze kwa ulivyoanza kazi.
Mtiifu,
Oikos
 
Ni wakurugenzi wa HALMASHAURI mmekua mkiwateua ili wasaidie wananchi katika eneo husika ila unaweza kwenda una shida serious unakuta JITU LINAJIVUTA KAMA GUNDI au unamweleza shida yako anajifanya Mungu mtu, anakutukana na kukujibu hovyo, baadhi ya wakurugenzi wenye tabia hizo ni wa halmashauri ya Nzega, Bagamoyo.....ongeza wengne
 
Kumekuwa na tabia isiyopendeza ya kutokupenda kuwatumia wataalam wa Kitanzania Wazalendo kulitumikia Taifa lao na badala yake wamekuwa wakiachwa waende kuyatumikia mataifa ya nchi za nje na sisi kuishia hatuna wataalam na tunapowahitaji huwa tunawatumia wageni ambao tunawalipa mamilioni ya fedha wakati tungeweza kuokoa fedha hizo kwa kuwatumia wataalamu wazawa.

Inawezekana kabisa wataalamu hawa wazawa wamekuwa wakifichwa na wasaidizi wa Rais kwa kuhofia hatma zao eti watakuja kuwapora nafasi zao. Mawazo na fikra mfu kabisa.

Tangu Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli aingie madarakani ameonyesha kujitenga na aina ya uongozi toka kwa marais waliomtangulia jambo linamjengea heshima kubwa sana kwa jamii. Inabidi sasa avunje hii dhana ya kupuuzia kutumia wataalamu wetu wazawa wanaofanya kazi nchi za nje.

Kwa kuanzia Rais Magufuli amtumie mtaalamu Mzalendo anayewika katika mataifa ya nje aitwaye Dk. Kiyabo Mike Nghomange.

DK. KIYABO MIKE NI NANI?

Dk. Kiyabo Mike ni Mtanzania aliyezaliwa Oktoba 16, 1959 anayeishi na kufanya kazi nchini Marekani. Dk. Kiyabo alipata elimu ya msingi Nyashimo (1966-1972). Pia amesoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne (1973-1976) katika Shule ya Sekondari ya Kahororo.

Mwaka 1980 alihitimu diploma ya Clinical medicine katika chuo cha Ifakara Medical college. Alijiendeleza tena na mwaka 1993 alihitimu shahada ya Clinical medicine katika chuo cha KCMC.

Hakuishia hapo mwaka 2004 alipata masters ya Health care administration katika chuo cha Rochville University na mwaka 2008 alipata Phd ya Health Care Adminstration katika chuo cha Rochville University nchini Marekani.

UZOEFU WA KIKAZI WA DK. KIYABO MIKE

Dk. Kiyabo alishafanya kazi Clinical Officer katika hospitali ya Temeke, Dar es salaam (1980 -1991); Alishawahi Mganga mkuu msaidizi, Dar es salaam (1993-2002); Clinician wa Clear view Center (2007-2010); Program Manager wa Equinox Inc (2010-2013) New York, Marekani.

Pia ni Mhadhiri katika chuo cha Albany Medical School cha nchini Marekani kuanzia mwaka 2010 mpaka sasa.

Sasa hivi ni Quality Health Care Director wa hospitali ya Whitney M Young Health service cha nchini Marekani.

Wamarekani wanazidi kutambua kipawa, elimu, uweledi wa Dk. Kiyabo hadi kupewa ushiriki wa ushauri juu ya Obama Care.

Uwezo wake wa kiuongozi umemfanya kupata wadhifa wa juu kabisa wa Umakamu wa Rais Umoja wa Afrika Mashariki, USA. Inabidi Mtaalamu huyu Mzawa aje nchini alitumikie Taifa letu. Ila si Dk. Kiyabo tu, wapo wataalamu wengi wenye taaluma mbali mbali wakitumwiwa vizuri wataleta tija kwa Taifa.

KWANINI DK. KIYABO?

1. Elimu na uzoefu wake unashawishi kuwa ataleta tija kwa Watanzania.
2. Ni mtaalamu wa aina yake aliyesomea Tanzania na kufanya kazi Tanzania (miaka ya nyuma) na hivyo anazijua shida, changamoto zinazolikabili Taifa.

My take;-

1. Dk. Kiyabo amesomea Tanzania na hivyo anazijua changamoto za elimu Tanzania na namna ya kuzikabili.
2. Dk. Kiyabo ni mtaalamu wa masuala ya Afya na amewahi kufanya kazi ya huduma za kiafya nchini na hivyo atakuwa jawabu sahihi ya kuzikabili changamoto za sekta ya kiafya.

Rais Magufuli amtumie Dk. Kiyabo na wana taaluma wengine wazawa nikiwa na imani wataleta tija kwa maslahi mapana ya Taifa letu kwani wanatosha kuendana na kasi ya HAPA KAZI TU
 
Attachments

  • 1448419157492.jpg
    1448419157492.jpg
    72 KB · Views: 495
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom