Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Jipu hili ukilitumbua, litasaidia Serikali yako. Jipu hili litaimarisha makazi ya watumishi wako waandamizi Serikalini. Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na wengineo hawatakaa uraiani au kwenye hoteli zinazolipiwa na Serikali. Watakaa pamoja na kuwa rahisi kupatikana kwao. Jipu hili muhimu kutumbuliwa kwasasa.

Ni jipu la nyumba za Serikali. Nyumba za Serikali zilijengwa sehemu mbalimbali hapa Dar es Salaam. Lengo lilikuwa ni kuwapa makazi viongozi waandamizi Serikalini na urahisi wa ulinzi pamoja na kupatikana kwao. Viongozi waandamizi walipokuwa wakimaliza muda wao wa kazi, walikuwa wakiwapisha wengine na maisha kuendelea. Nyumba zilibaki.

Nyumba hizo zikauzwa. Viongozi sasa wanatafuta na kutangatanga juu ya makazi. Wanakaa mbali na vituo vyao vya kazi na hata kusababisha foleni kwakuwa wanatokea mbali ya mji. Mfano, Jaji Mkuu anaishi njia ya Tegeta. Si sahihi. Si sawa. Alipaswa kuwa karibu na ilipo ofisi yake. Nyumba kwa ajili ya Jaji Mkuu iko wapi?

Tafadhali Rais, rejesha nyumba zote za Serikali serikalini. Ni jipu lililokwishaiva siku nyingi tu. Kwakuwa mtumbuaji umefika, fanya yako. Umbea: hata nyumba za Mawaziri pale Mikocheni hazikaliwi na Mawaziri waliolengwa. Viongozi wameshapazoea uraiani.

Jipu hili litumbuliwe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Usijari we Mzee, serikali inapunguza hilo lundo la viongozi ili idadi yao iendane na nyumba zilizopo ..mawaziri + makatibu wakuu.
 
Leo nimetembelea chuo St Joseph University, lakini cha kushangaza nimekuta karibia asilimia 90 ya staff wote pamoja na walimu ni raia wa India na hakuna mwenye uhakika na elimu zao maana wanapeana ajira wao kwa wao.

Dukuduku langu ni kwamba hawa jamaa wanachangia pia kuharibu taaluma na uweledi wa watanzania wanaoenda kusoma pale, na tunasahau kuwa hawa jamaa wanaomaliza hapa wanakuja kuwa mizigo kwetu aidha kwa kukosa ajira au kuwaajiri na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi unaotakiwa.

Mheshimiwa magufuli tafadhali naomba hakikisha mikataba yote ya wawekezaji wote inapitiwa upya hasahasa linapofikia suala la ajira kwa wazawa kwa sababu tunajua kuwa faida mojawapo ya wawekezaji kutoka nje ni pamoja na kutupatia ajira sisi wazawa katika hili kwa kweli St joseph wamezidi.Nchi yetu ina wataalamu wa kutosha hao hao ndo wapewe kipaumbele kwanza pale wawekezaji wanapokuja nchini mwetu.

********Nimechukia sana katika hili*******
 
Mkuu hii thread yako imenisaidia kupata picha ya kwa nini wahitimu wa hicho chuo ulichotaja wanasifika kwa kuiva kitaaluma. Hii kwa mujibu wa waajiri wachache niliopata kuonana nao personally na pia baadhi ya wahitimu wa vyuo vingine. Kwa mtazamo wangu suala la mikataba yao kama wageni na uharibifu wa taaluma ni vitu viwili tofauti. Kuna vyuo vingi sana hapa nchini ambavyo lecturers wake ni wazawa lakini bado kitaaluma viko chini mno. Kwa hiyo sishawishiki kukubaliana na wewe kwamba uwepo wa foreign lecturers pale chuoni umeharibu taaluma kwani kitaaluma chuo kiko vizuri sana. Labda hoja yako iwe ni kwanini wazawa (wenye taaluma husika, weledi na walio committed kwenye kazi) wasipewe kipaumbele kwenye ajira.
 
Ofisi za St. Joseph University ukifika kwa mara ya kwanza unaweza kudhani upo "Calcutta kwa Mama Thereza India"
 

Mkuu hapa concern zangu kuu ni mbili

1.Kutokuwa na uhakika wa taaluma za wakufunzi wa hapa maana hakuna board yeyote ya serikali inayoshughulikia kuhakikisha inakuwa na uhakika wa taaluma zao

2.Ni hili suala la ajira kwa wazawa
 
Mie nakuomba ushughilikie idara ya uhamiaji na tume ya ajira nchini,,, idara ya uhamiaji inatoa vibali kwa wahindi kwa kihidhinisha kuwa ni expperts na kuwaruhusu kufanya kazi katika makampuni kwa ajira ambazo zinaweza kufanywa na watanzania wazawa na tume ya ajira inaridhia bila kufanya ukaguzi kuwa mtu huyu ni experts kweli na nikipi ailichonacho cha kipekee ambacho hakiwezi kufanywa na watanzania wazawa. Vijana wa kitanzania wanakosa ajira huku wageni wanageuza tanzania shamba la kuchuma na kutajirisha nchi zao. Pia kiwango cha mishahara kwa makampuni ni aibu sana akiendani na masaa ambayo mtu anafanya kazi. Mfano mtu wa degree alipwa tsh. 300,000 kwa mwezi na anafanya kazi kuanzania saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni au saa 2 usiku. No overtime. Jmp liangalie na hili pia
 
Sasa hivi kumekuwa na matarajio na sifa kedekede kumwendea Magufuli katika wiki hizi tatu alizoingia ofisini. Tofauti na wengi, mi nitamkubali akifanya haya :

1) Akijenga reli ya kati, ili wenye malori yanayoharibu barabara zetu yakapaki uani

2) Akikamata wauza madawa ya kulevya wale wakubwa (mapapa)

3) Awafunge mafisadi kuanzia wa meremeta, KAGODA, ESCROW nk

4)Afute mbio za mwenge wa uhuru

5) Afute mikataba yote yenye utata ya madini na ya Gas.

Asipofanya haya, nitaona ni sanaa tu ndo zinaendelea.
 
hapo sawa kbs nakubaliana na wewe ..hayo mengine anayoyafanya ni danganya toto wenye akili tunajua ukweli
 
Kama huna uwezo wa kushukuru kwenye unacho kiona kidogo kamwe hutopata uwezo wa kushukuru kwenye unacho kiona kikubwa!

Hata akifanya unayo yasema bado utakuja na list nyingine!

Ambacho kitakuridhisha wewe nikuona ana kwama.
 

wewe nani umpangie rais kazi tunaataka utata wa richmond na capacty chage ya umeme ambayo inaendelea kutafuna wananchi
 
Mimi nitafurahi endapo atamtaja mtu aliyesafiri nje ya nchi
mara nyingi kuliko kwenda kusalimia wazazi wake.
 

Mm nataka amkamate yule aliua kiwanda cha general tyre na kuingiza yana nchin
 
Mh Rais mchapakazi hebu litazame hili suala la simu wakati wa kazi, ikiwezekana piga marufuku matumizi ya simu wakati wa kazi. Haya mambo ya kuchat wakati wa kazi yanapunguza sana ufanisi katika kazi, sekta binafsi wamefanikiwa sana katika hilo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…