Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Wanajamvi,

Mimi ni raia wa kawaida na ninawaona watumishi wa umma jinsi wanavotumia hovyo mali za umma mfano kutumia magari ya umma kwa ajili ya manufaa yao binafsi kama kumpeleka mama/msaidizi wa nyumbani sokoni au hata wakati mwingine magari ya serikali kuwepo sehemu za starehe usiku mwingi pia uharibifu wa miundombinu ambayo inaigharaimu serikali pesa nyingi.

Nimeanza kuvutiwa sana na utendaji kazi wa mheshimiwa Rais na ningependa kutoa mchango wangu ili kusaidia kupiga vita mambo haya yanyoyoligharimu taifa je ninawezaje kupaza sauti naye akanisikia? sina uhakika sana na hawa wasaidizi wake maana baadhi ya wabadhirifu ndio hao hao ambao unatakiwa upitishie malalamiko yako.

Naomba msaada
 
Matatizo mengi ya nchi hii yapo kwenye katiba ambapo kiongozi afanye mabaya au mema hakuna pa kumbana na wanajivunia wingi wa wabunge walio nao ili kupitisha mambo ya hovyo ndy mh Magufuli anahangaika kusafisha uozo wa watu wengi waliokuwa wameridhika na yaliofanyika huko nyuma
 
Raisi wetu Magufuli tu nakuomba sana tumalizie hii kero ya umeme kwa mfano hapa Arusha umeme umekua Kero kubwa unakatwa toka asubuhi ikifika jioni unarudi baada ya nusu saa wanakata tena ikifika saa moja usiku unarudi haipiti nusu saa ghafla unakua dhaifu kama mshumaa alafu wanaukata tena yani imekua kero na vifaa kuungua kutokana na low voltage tunakuomba rais wetu uliangalie hili suala.
 
Namsihi mh.Jpm kama anataka kasi yake iendane na matakwa ya sheria basi namuomba ktk kuendeleza mchakato wa katiba mpya basi alete ile rasimu ya warioba ya tume ya mabadiliko ya katiba ili kasi yako iwe kisheria zaidi na ccm wenzako wasifhani km una bifu nao.

Kama utapitisha ya bunge la jk basi speed yako itakuwa bure na unaweza kuishia kuvunja sheria na kulaumiwa.

Yote unayotamani yaganyike yaweke kisheria uwe safeside.

Hongera km utaendelea hv unaweza angalau kutuvusha.
 
Tena aanze na huyu Engineer Mramba, siku hizi nae amegeuka mwanasiasa kama Simba cha wenyewe.

Engineer mzima anadanganya umma eti gesi inajazwa na August itakuwa mwisho wa tatzo la umeme afu hamna kitu!!

Hivi ni huyu Engineer ndie alie kuwa Mkurugenzi wa TANESCO wakati wa sakata la Jairo, la TANESCO na Idara za madini kuchangia fedha kupitisha Budget ya Nishati na Madini?

Hadi Magufuli aseme TANESCO wamefungulia maji ya Mtera, yeye yupo kimya tuu! Awajibe au awajibishwe!

Tangia Prof. Mhongo atoke nguzo wanaunganisha kwa mdebwedo sana hadi utoe laki kadhaa.
 
Namsihi mh.Jpm kama anataka kasi yake iendane na matakwa ya sheria basi namuomba ktk kuendeleza mchakato wa katiba mpya basi alete ile rasimu ya warioba ya tume ya mabadiliko ya katiba ili kasi yako iwe kisheria zaidi na ccm wenzako wasifhani km una bifu nao.

Kama utapitisha ya bunge la jk basi speed yako itakuwa bure na unaweza kuishia kuvunja sheria na kulaumiwa.

Yote unayotamani yaganyike yaweke kisheria uwe safeside.

Hongera km utaendelea hv unaweza angalau kutuvusha.

Nakubaliana na wewe kabisa.
 
Problem ni kwamba yy sio mwenyekiti wa chama so hana influence kubwa sanaa ila naunga mkono
 
Warioba mwenyewe hajielewi, eti anaenda Jangwani kuwakampenia CCM.
 
Namsihi mh.Jpm kama anataka kasi yake iendane na matakwa ya sheria basi namuomba ktk kuendeleza mchakato wa katiba mpya basi alete ile rasimu ya warioba ya tume ya mabadiliko ya katiba ili kasi yako iwe kisheria zaidi na ccm wenzako wasifhani km una bifu nao.

Kama utapitisha ya bunge la jk basi speed yako itakuwa bure na unaweza kuishia kuvunja sheria na kulaumiwa.

Yote unayotamani yaganyike yaweke kisheria uwe safeside.

Hongera km utaendelea hv unaweza angalau kutuvusha.

Kwenda huko wewe unamsihi kama nani wakati hukunpigia kura? Unaleta sera za ukawa hapa? Sisi tuliompigia kura ndo tunaweza kumsihi afanye kadri tunavyotaka...wewe endelea kumsihi EL jinsi ya kuimarisha ukiwa..
 
Hawezi, labda kama anataka kukosana na wabunge wa chama chake walioipitisha na rais mstaafu aliyesaini rasimu kwa mbwembwe
 
Achukue rasimu ya warioba ili iweje? kama mmeshindwa wakati JK yupo madarakani kwa JP ndo msahau kabisa, kile ni cha mpingo hesabuni mmeumia!
 
Hatuna uhakika kama Na wewe ulipiga kura kwa Rais ila hasa watumishi wa nishati hii ya umeme busy
 
Kwenda huko wewe unamsihi kama nani wakati hukunpigia kura? Unaleta sera za ukawa hapa? Sisi tuliompigia kura ndo tunaweza kumsihi afanye kadri tunavyotaka...wewe endelea kumsihi EL jinsi ya kuimarisha ukiwa..

Kwa hiyo yeye ni rais wa waliomchagua au wa Watz wote?
 
Kuna wahudumu wa Afya hasa members wa Regional Health Management Team (RHMT) na Council Health Management Team (CHMT) waliozoea kuzurula kwenye warsha, semina na maadhimisho ya sherehe mbalimbali za kiafya walalamika ile mbaya. Wanasema eti mh.Rais unaingilia professional za watu , wanaona kuwa unawaharibia dili zao za kunyonya mapene bila jasho.

MY TAKE: Hivi rais hakuna namna ya sisi wazalendo kuwa tunakutumia majina ya wazembe kwenye hi sekta ya Afya waliozoea kunyonya bila kutoa jasho? Tunaomba utupe namba yako ya simu tuwe tunakutumia hayo majina maana hawa watu wamezoea sana.
 
Kwa hiyo yeye ni rais wa waliomchagua au wa Watz wote?

Ni rais wa JMT, lakini kumbuka kuwa sisi tulio wengi (majority) tumempa hiyo nafasi kwa sababu ya sera zake. Watanzania wangekuwa interested na Katiba Mpya basi wangemchagua EL!
Acha kumchomekea rais afanye vitu ambavyo sio vipaumbele kwa watanzania tulio wengi
 
Wanasiasa wa nchi hii kwa Zanzibar wameshindwa kabisa jumla!
Yule bingwa Wa kutatua migogoro duniani hayati baba wa taifa Mwalimu J. K Nyerere alishindwa hapo!
Mzee Mwinyi alishindwa hapo!
Mzee wa uwazi na ukweli Mkapa hapo ndio kabisaaa!
Jk Wa Maisha bora, ndio ametoka wakati Jecha akilianzisha tibwiri huko!

Nimekuwa najiuliza sana.
Tukiacha hizi suluhu zetu tulizozoeshwa za funika kombe mwanaharamu apite.

Je katika nchi hii hakuna watu wengine wenye hekima zaidi ambao wanaweza kupelekea suruhu ya kudumu katika visiwa hivi vya karafuu hata kama ni nje ya siasa za siasa zinazoshabikia maslahi ya vyama?
Kama hakuna basi tusubiri lile tusilolijua liamue vile litakavyoamua!
Pamoja na hivyo hii itakuwa ni aibu kubwa mno ambayo inawafanya laia wa nchi hii pamoja na viongozi wao; kukosa ujasiri wa kusaidia wengine kuamua mambo yaliyowashinda!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom