Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
wenye ndoto na mitandao ya urais hawafai uwaziri. wataishia kupanga mitandao na biashara ya kununua watu. weka mawaziri wachapa kazi. urais wananchi wataibua mchapakazi kama walivyokuibua wewe.
EXCELLENT!!! Yaani aitaka kufanikiwa na watanzania tufanikwe afuate ushauri HUU!!!!

EXCELL!!!!
 
Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mughwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.

Fox kwa hili nakuunga mkono,ile nondo aliyoitema siku pombe anapokea cheti cha ushindi na kushangiliwa na magamba hakika inafaa.nukuu"wananchi wanataka mabadiliko na mojawapo ni katiba ya wananchi"by Anna!
 
Karibu nusu ya wabunge wa CCM either wapo kwenye kashfa ya ufisadi au wana kaufisadi ndani mwao.
 
Mawazo mazuri. Ila Prof. Muhongo asimsahau. Madeni makubwa yanayozungumziwa TANESCO waliyoyaleta ndo hao mliokuwa mnazimia wakija kuomba kura.

Akikosa Prof. Muhongo tutajua yale yale. Mwakyembe big up.

Nafasi ya waziri wa Fedha ni nyeti sana. Ingekuwa tunaweka utanzania Mbele badala ya vyama Prof. Lipumba angetusaidia. Vinginevyo, nafikiri Mhe. Rais ateue mtu mwenye uwezo kutoka nje ya wabunge waliotajwa mpaka sasa.

Kihusu Elimu, sote tumemsikia Rais Mstaafu Mkapa ameeleza wazi kwamba kiwango cha elimu kimeshuka kwa miaka hii 10. Sasa, Kawambwa tusimwone hata tone kwenye baraza la mawaziri. Narudia, Kawambwa asionekane hata tone kwa ushauri wangu.
 
Pamoja na kwamba sina imani na chama chako, ila naomba unishawishi wewe binafsi katika serikali yako.
Kama ulivyojinaji kuwa serikali yako, yani Tanzania ya Magufuli itakuwa KAZI TU, basi naomba udhihirishe hivyo katika baraza lako la mawaziri.

Kabla hata sijataka kujua waziri mkuu ambaye ataendana na sura ya kauli mbiu yako, lakini nataka usituletee watu hawa ambao walikuwa mzigo kwa taifa na waliolifikisha nchi hapa ilipo chini ya aliyekutangulia pamoja na waziri mkuu wake.

1. Sopteter Muhongo.
Huyu pamoja na kwamba tunaambiwa hakuhusika moja kwa moja kwenye kashfa xa escrow lakini alikuwa kinara wa utetezi katika sakata hili. Pia ni miongoni mwa waziri wenye elimu kubwa lkn hakuwa na mkakati bunifu wa kutatua tatizo la umeme nchini zaidi ya kuiacha tanesco kwenye deni kubwa. Pia ni miongoni mwa viongozi ambao hawathamini wawekezaji wa ndani, anaamini nchi itajengwa na wazungu au wachina.

2. Lazaro Nyalandu.
Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao tumeshuhudia tembo wakiuliwa kwa wingi, na twiga wetu wakisafirishwa kwenda nje, hafai katika serikali yako, kwani atafanya kazi ya mazoeaa ya serikali ya awamu ya 4.

3. Mwigulu Nchemba.
Pamoja na kwamba hakukaa kwenye wizara ya fedha kwa mda mrefu, lkn ni miongoni mwa vijana ambao hawana adabu katika taifa hili. Ni mmoja wa wanasiasa wachanga ambao hajali matamshi yake mbele ya umma, haangalii baada ya hapa athari zake zitanipeleka wapi, sio mstaarabu.

4. Willium Lukuvi.
Huyu kwa mwendo wa kasi inayohitajika nchini hatufai, utendaji wake hauto tofautiana na wa awamu ya 4, hana jipya ndani ya serikali yako.

5. Shukuru Kawambwa
Huyu ni moja ya mawaziri walioshusha thamani ya elimu yetu. Sio mbunifu. Fedha za fidia za rada mpaka leo hatujui matumizi yake yalienda wapi, hatufai kabisaa.

6.Hawa Ghasia.
Huyu mama bado uchama umemkaa kichwani kuliko maslai ya taifa. Hayupo active katika utendaji wake.

7. Jumanne Maghembe.
Huyu ni moja ya mawaziri ambao ndio chanzo cha huduma mbovu za elimu na maji. Elimu yake ni kubwa lkn haina msaada kwetu.

8.Harrison Mwakyembe.
Huyu kinachompa sifa ni lile sakata la richmond ambalo tunamwona kama shujaa. Lakini kiukweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji. Sijaona mafanikio yake katika wizara alizozisimamia, ni mzigo ana asili ya mtandao ambao ni chanzo cha utendaji mbovu nchini. Ni mafya wa kisiasa

9. Magreth Sitta
Mama huyu tangu zama ni outdated, haendani na kasi ya dunia, yupo nyuma na mda, hafai katika serikali yako.

10. Sofia Simba
Hana tofauti na Mama sitta, tena huyu uchama na mtandao wa uongozi umemjaa kichwani, hafai katika serikali yako.

11. Andwer Chenge
Najua huyu unamfahamu vema

12. Anna Tibaijuka
Najua unamfahamu vizur

13. Willium Ngeleja
Najua wamfahamu vzr

NB.
1. Mheshimiwa Rais kuna vijana wengi ambao naamini katika utendaji wao lkn siamini kundi lake, na mmoja wao ni Januari Makamba. Huyu binafsi namwamini kiutendaji, ubunifu lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka makubwa, kundi lake lililo nyuma yake, Huyu badala ya kuchapa kazi atakuwa anawaza urais baada yako kustaafu. Kwa mtazamo wangu ungemweka kando kwa mda baada ya miaka miwili ndo uumpe majukumu.

2. Kwa kukusaidia mh Rais ni vema ukachagua mawaziri wachache ambao wengi wao hawakuwa mawaziri, sio viongozi katika chama, vijana, wenye elimu isiyo na shaka. Hawa ndio wataileta tanzania mpya ya HAPA KAZI TU.

Mh Rais ukikosea kwenye baraza la mawaziri basi jua umeuwa nchi, na hapo tutadhibitisha kuwa hakuna cha Magufuli 4 change itakuwa ccm ni ile ile.

Asantee.

Kamanda achana na Prof Muhongo.ile ni namba nyingine. Ni mashine ya uhakika nadhani rais asimuache kwenye baraza lake. Yule ni kati ya mawaziri ambao wakiwepo tuna uhakika wa kwenda kwenye uchumi wa kati.jembe lile baba! Ni muadilifu, mchapakazi, ni result oriented, ni type ya Magufuli. Hana ufisadi na wala hatamani na wala sio mfanyabiashara.
Angalia sifa kubwa ya waziri afaaye kuingia katika cabinet hii ni kwamba asiwe mfanyabiashara. Walau hapo pa kuanzia. Sio anakuwa waziri nayeye humohumo .anataka kuchomeka tenda zake kama walivyokuwa wanafanya kina Lowasa! Tafadhali badilikeni
 
Imekuwa kawaida kila serikali ikiingia madarakani au wizara kupata waziri mpya, lazima wanunue magari mapya ya mawaziri wakati yaliyopo ni mazima.Magufuli komesha tabia hii kuepeuka matumizi yasiyo ya lazima. Waziri asiyetaka kutumia gari la zamani ampishe mwingine mwenye uzalendo. Kuna tetesi mawaziri huogopa kutumia magari waliyoyakuta kwa imani za kishirikina. Kwamba waliotangulia walienda nayo Bagamoyo nk.Tabia hii ife kabisa. Tena Magufuli aweke "wanted" kabisa hakuna kununua gari mpya ndani ya miaka miwili.

Mawaziri watumie magari yao binafsi, wapewe mafuta na service ya serikali.
Au hayo mashangingi mapya wapewe kama mkopo, ndani ya muda wahakikishe wanailipa.
 
Hao uliowataja ndio nguzo ya ccm , ukiwaondoa ccm imebomoka .
 
Ubarikiwe Mkuu!
Maendeleo ni hatua, kusiwe na 2 kama hakuna 1 na 1, wala 3 kama hakuna 2 na 2.
Anaita sasa.
 
Shost kama walivyo wa-Tz wengine,ana uhuru wa kutoa maoni yake.Kwa hiyo tusimbeze bali tutoe maoni yetu kwa vile tunavyoona ni sahihi zaidi.
 
Wakitutembelea hapa atumie kiswahili. Akitembea kwa wenzetu waarabu, wachina, warusi Nk atumie kiswahili

Akitembea ktk nchi za kiingereza kama uingereza, baadhi ya nchi za ulaya na marekani hana budi kutumia kiingereza.

Akihutubia mikutano ya kimataifa kama ya afrika mashariki, sadc, AU na UN atumie kiswahili
 
pamoja na kwamba sina imani na chama chako, ila naomba unishawishi wewe binafsi katika serikali yako.
Kama ulivyojinaji kuwa serikali yako, yani tanzania ya magufuli itakuwa kazi tu, basi naomba udhihirishe hivyo katika baraza lako la mawaziri.

Kabla hata sijataka kujua waziri mkuu ambaye ataendana na sura ya kauli mbiu yako, lakini nataka usituletee watu hawa ambao walikuwa mzigo kwa taifa na waliolifikisha nchi hapa ilipo chini ya aliyekutangulia pamoja na waziri mkuu wake.

1. Sopteter muhongo.
Huyu pamoja na kwamba tunaambiwa hakuhusika moja kwa moja kwenye kashfa xa escrow lakini alikuwa kinara wa utetezi katika sakata hili. Pia ni miongoni mwa waziri wenye elimu kubwa lkn hakuwa na mkakati bunifu wa kutatua tatizo la umeme nchini zaidi ya kuiacha tanesco kwenye deni kubwa. Pia ni miongoni mwa viongozi ambao hawathamini wawekezaji wa ndani, anaamini nchi itajengwa na wazungu au wachina.

2. Lazaro nyalandu.
Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao tumeshuhudia tembo wakiuliwa kwa wingi, na twiga wetu wakisafirishwa kwenda nje, hafai katika serikali yako, kwani atafanya kazi ya mazoeaa ya serikali ya awamu ya 4.

3. Mwigulu nchemba.
Pamoja na kwamba hakukaa kwenye wizara ya fedha kwa mda mrefu, lkn ni miongoni mwa vijana ambao hawana adabu katika taifa hili. Ni mmoja wa wanasiasa wachanga ambao hajali matamshi yake mbele ya umma, haangalii baada ya hapa athari zake zitanipeleka wapi, sio mstaarabu.

4. Willium lukuvi.
Huyu kwa mwendo wa kasi inayohitajika nchini hatufai, utendaji wake hauto tofautiana na wa awamu ya 4, hana jipya ndani ya serikali yako.

5. Shukuru kawambwa
huyu ni moja ya mawaziri walioshusha thamani ya elimu yetu. Sio mbunifu. Fedha za fidia za rada mpaka leo hatujui matumizi yake yalienda wapi, hatufai kabisaa.

6.hawa ghasia.
Huyu mama bado uchama umemkaa kichwani kuliko maslai ya taifa. Hayupo active katika utendaji wake.

7. Jumanne maghembe.
Huyu ni moja ya mawaziri ambao ndio chanzo cha huduma mbovu za elimu na maji. Elimu yake ni kubwa lkn haina msaada kwetu.

8.harrison mwakyembe.
Huyu kinachompa sifa ni lile sakata la richmond ambalo tunamwona kama shujaa. Lakini kiukweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji. Sijaona mafanikio yake katika wizara alizozisimamia, ni mzigo ana asili ya mtandao ambao ni chanzo cha utendaji mbovu nchini. Ni mafya wa kisiasa

9. Magreth sitta
mama huyu tangu zama ni outdated, haendani na kasi ya dunia, yupo nyuma na mda, hafai katika serikali yako.

10. Sofia simba
hana tofauti na mama sitta, tena huyu uchama na mtandao wa uongozi umemjaa kichwani, hafai katika serikali yako.

11. Andwer chenge
najua huyu unamfahamu vema

12. Anna tibaijuka
najua unamfahamu vizur

13. Willium ngeleja
najua wamfahamu vzr

nb.
1. Mheshimiwa rais kuna vijana wengi ambao naamini katika utendaji wao lkn siamini kundi lake, na mmoja wao ni januari makamba. Huyu binafsi namwamini kiutendaji, ubunifu lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka makubwa, kundi lake lililo nyuma yake, huyu badala ya kuchapa kazi atakuwa anawaza urais baada yako kustaafu. Kwa mtazamo wangu ungemweka kando kwa mda baada ya miaka miwili ndo uumpe majukumu.

2. Kwa kukusaidia mh rais ni vema ukachagua mawaziri wachache ambao wengi wao hawakuwa mawaziri, sio viongozi katika chama, vijana, wenye elimu isiyo na shaka. Hawa ndio wataileta tanzania mpya ya hapa kazi tu.

Mh rais ukikosea kwenye baraza la mawaziri basi jua umeuwa nchi, na hapo tutadhibitisha kuwa hakuna cha magufuli 4 change itakuwa ccm ni ile ile.

asantee.

tanzania kila mtu
kocha
mwalimu
waziri \
mbunge

naona mpka

uraisi
 
Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mughwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.
Hii thread ilinipita pembeni.

Unachokifikiri ndicho ninachokifikiria kuhusu huyu Dada/Mama yetu.

Ninatumaini Rais Magufuli atamkumbuka katika safu za wabunge/viongozi wa kisiasa bungeni.

Ninashukuru kwa mchango wako unaoakisi fikra zangu.
 
Ili kuipa hadhi na kuitangaza lugha yetu ya taifa, nashauri rais wetu mpya atumie Kiswahili katika shughuli zote rasmi za kitaifa na kimataifa. Cha msingi ni kuwa na wakalimani mahiri katika shughuli za kimataifa. Hii itainua hadhi na heshima ya nchi yetu badala ya kuendelea kuthamini lugha za kigeni. Tumekuwa watumwa mno wa lugha ya kiingereza mpaka kufikia hatua kudhani kuwa mtu anayeongea kiingereza vizuri ndiye aliye elimika wakati si kweli. Elimu ni uwezo siyo kuongea kiingereza. Hiki kiingereza cha "izi, wozi, wea, kongrugesheni, ameizingi, wati?, yu no, no problemu hakitusaidii kitu. Na kwa ujinga wetu tunafundishana kwa lugha tusiyoijua vizuri matokeo yake watoto wanafeli halafu tunawaona wajinga kumbe sera zetu ndio mbovu. Wachina, wakorea, wajerumani, wareno, wafaransa mbona wanatumia lugha zao na wanapiga hatua kubwa sana katika uchumi na sayansi. Sisi na kiingereza chetu cha kuombea maji tumefika wapi zaidi ya kutudhalilisha?

Maoni yangu haya hayana maana kuwa sitambui uwezo mkubwa wa kiingereza alio nao dr. Nataka aendeleze pale mwenzake alipoachia mwenzake, kwani alianza kwa kuhutubia kwa kiswahili kwenye mkutano wa AU lakini baadaye akaacha. Mimi nashauri Dr. sasa ajikite pamoja na mambo mengi kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa kwa yeye mwenyewe kuitumia badala ya kiingereza. Huwa naona viongozi wa nchi nyingine kama za kiarabu pamoja na kuwa wanajua kiingereza lakini utakuta wanazaunguza kiarabu na kisha wasiojua kutafsiriwa. Wakalimani sasa hivi tunao wengi, ni vizuri wakatumika vizuri kuikuza lugha yetu ya taifa. Ukweli ni kuwa unapotumia lugha mama au lugha ya taifa una kuwa na uhuru na uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuelezea kuliko unapotumia lugha za kigeni. Kwa watanzania wengi lugha yetu ya mama ni kiswahili.

Kwani kuna lugha nyingine mbadala ambayo angeweza kuitumia zaidi ya kiswahili?
 
Sawa nitamwambia... Ila ujue kwamba mimi simpigii chapuo mtu yeyote yule ila nimetoa mchango kutokana na mtoa mada alivyowasilisha. Ningekua nimeyasema haya mbele ya rais hapo ningejiona nimempigia chapuo.

We kamwambie tu uache porojo, hapa jf RAIS ana watu wake wanaokusanya maoni na mitazamo ya watu. ndio maana ukiwachokonoa wakubwa hapa jf watakujia juu.Nashauri Akisharudisha hizo pesa achunguzwe ili serikali ikjiridhisha 2020 ndo apewe huo uwaziri
 
No 1,3,4 na 8 ni watu makini sana na wanahitaji sana ....hivyo nasikitika kukutangazia kuwa maombi yako katika namba tajwa hayatozingatiwa kabisa! Hao ni wachapakazi wazuri na wana hitajika...

watanzania kama wewe wapimwe akili kuona kama iko sawa kabla ya kuwalaumu ( Muhongo?)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom