Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
hapo wewe ndo umenishauri kitu ambacho ndo nilikuwa nawaza. na huu ni ujumbe au ushauri kwa taifa. ninaomba waandishi wa habar mfike sasa na huku Kilombero Kuna Mambo Mazuri Sana

sijakuelewa tena.........
 
Ni ushauri mzuri mno,hongera.Frankly hata mimi singependa kuwaona watu hao katika any position of power tena. Wametu-let down sana.Akimuweka yeyote kati ya hao tutajua kwamba hana nia ya kweli ya kuwasaidia watanzania,na infact yeyote ambaye alikuwa kwenye awamu ya nne.Haikuwa serikali makini kabisa.

ila mwigulu unamuonea jamaa kwa kazi anajua! labda ongea yake, but ni bora kuliko ata makamba
 
Pamoja na kwamba sina imani na chama chako, ila naomba unishawishi wewe binafsi katika serikali yako.
Kama ulivyojinaji kuwa serikali yako, yani Tanzania ya Magufuli itakuwa KAZI TU, basi naomba udhihirishe hivyo katika baraza lako la mawaziri.

Kabla hata sijataka kujua waziri mkuu ambaye ataendana na sura ya kauli mbiu yako, lakini nataka usituletee watu hawa ambao walikuwa mzigo kwa taifa na waliolifikisha nchi hapa ilipo chini ya aliyekutangulia pamoja na waziri mkuu wake.

1. Sopteter Muhongo.
Huyu pamoja na kwamba tunaambiwa hakuhusika moja kwa moja kwenye kashfa xa escrow lakini alikuwa kinara wa utetezi katika sakata hili. Pia ni miongoni mwa waziri wenye elimu kubwa lkn hakuwa na mkakati bunifu wa kutatua tatizo la umeme nchini zaidi ya kuiacha tanesco kwenye deni kubwa. Pia ni miongoni mwa viongozi ambao hawathamini wawekezaji wa ndani, anaamini nchi itajengwa na wazungu au wachina.

2. Lazaro Nyalandu.
Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao tumeshuhudia tembo wakiuliwa kwa wingi, na twiga wetu wakisafirishwa kwenda nje, hafai katika serikali yako, kwani atafanya kazi ya mazoeaa ya serikali ya awamu ya 4.

3. Mwigulu Nchemba.
Pamoja na kwamba hakukaa kwenye wizara ya fedha kwa mda mrefu, lkn ni miongoni mwa vijana ambao hawana adabu katika taifa hili. Ni mmoja wa wanasiasa wachanga ambao hajali matamshi yake mbele ya umma, haangalii baada ya hapa athari zake zitanipeleka wapi, sio mstaarabu.

4. Willium Lukuvi.
Huyu kwa mwendo wa kasi inayohitajika nchini hatufai, utendaji wake hauto tofautiana na wa awamu ya 4, hana jipya ndani ya serikali yako.

5. Shukuru Kawambwa
Huyu ni moja ya mawaziri walioshusha thamani ya elimu yetu. Sio mbunifu. Fedha za fidia za rada mpaka leo hatujui matumizi yake yalienda wapi, hatufai kabisaa.

6.Hawa Ghasia.
Huyu mama bado uchama umemkaa kichwani kuliko maslai ya taifa. Hayupo active katika utendaji wake.

7. Jumanne Maghembe.
Huyu ni moja ya mawaziri ambao ndio chanzo cha huduma mbovu za elimu na maji. Elimu yake ni kubwa lkn haina msaada kwetu.

8.Harrison Mwakyembe.
Huyu kinachompa sifa ni lile sakata la richmond ambalo tunamwona kama shujaa. Lakini kiukweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji. Sijaona mafanikio yake katika wizara alizozisimamia, ni mzigo ana asili ya mtandao ambao ni chanzo cha utendaji mbovu nchini. Ni mafya wa kisiasa

9. Magreth Sitta
Mama huyu tangu zama ni outdated, haendani na kasi ya dunia, yupo nyuma na mda, hafai katika serikali yako.

10. Sofia Simba
Hana tofauti na Mama sitta, tena huyu uchama na mtandao wa uongozi umemjaa kichwani, hafai katika serikali yako.

11. Andwer Chenge
Najua huyu unamfahamu vema

12. Anna Tibaijuka
Najua unamfahamu vizur

13. Willium Ngeleja
Najua wamfahamu vzr

NB.
1. Mheshimiwa Rais kuna vijana wengi ambao naamini katika utendaji wao lkn siamini kundi lake, na mmoja wao ni Januari Makamba. Huyu binafsi namwamini kiutendaji, ubunifu lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka makubwa, kundi lake lililo nyuma yake, Huyu badala ya kuchapa kazi atakuwa anawaza urais baada yako kustaafu. Kwa mtazamo wangu ungemweka kando kwa mda baada ya miaka miwili ndo uumpe majukumu.

2. Kwa kukusaidia mh Rais ni vema ukachagua mawaziri wachache ambao wengi wao hawakuwa mawaziri, sio viongozi katika chama, vijana, wenye elimu isiyo na shaka. Hawa ndio wataileta tanzania mpya ya HAPA KAZI TU.

Mh Rais ukikosea kwenye baraza la mawaziri basi jua umeuwa nchi, na hapo tutadhibitisha kuwa hakuna cha Magufuli 4 change itakuwa ccm ni ile ile.

Asantee.

Mkuu,

Mimi sitaji majina ila nataja vigezo vikuu 2: Chonde chonde Rais Magufuli usiwateue wafanyasiasa-political careerists ambao wanadhani siasa ni ajira. Kama utalazimishwa na Chama, basi wawe wachache sana ili kuondoa nuksi. Sana sana teua wapigania mabadiliko, ambao kwao siasa ni njia ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya Watanzania walio wengi-siyo kujinemesha wenyewe pamoja na familia zao, marafiki nk. Wapigania mabadiliko wawe vijana, wazee, au wanawake wanaweza kukusaidia kufikia ahadi zako!
 
ila mwigulu unamuonea jamaa kwa kazi anajua! labda ongea yake, but ni bora kuliko ata makamba

mwigulu na makamba wanajulikana kwa kusaka urais, watakuwa sehemu ya kutengeneza mitandao ya kuingia ikulu badala ya kutumikia wananchi
 
Wana Jamvi..
Namwomba rais JPM afanye mabadiliko pale kwenye ofisi yake maana kuna baadhi ya watendaji pale wakati wa JK walishaona ikulu kaa Mali yao. Mmoja wapo wa kumwondoa ni Salva Rweyemamu.
Nawasilisha.
 
Salva hawezi kuondoka nasikia ana hisa Ikulu.
 
Wana Jamvi..
Namwomba rais JPM afanye mabadiliko pale kwenye ofisi yake maana kuna baadhi ya watendaji pale wakati wa JK walishaona ikulu kaa Mali yao. Mmoja wapo wa kumwondoa ni Salva Rweyemamu.
Nawasilisha.

Huyo atafute kazi nyingine atapigwa chini tuu
 
Wanaondoka wote, mkuu usihofu ngoja kwanza baraza la Mawaziri litangazwe
 
Khaa!! Huyo mungu wako yaani anamuogopa Magufuli hadi kaona akutume wewe Illovo? 😎
 
PhD alisoma kwa ujaja ujanja wa kitanzania. Waziri Si ana mchuzi anaandikiwa na wasomi walala wima. Kiukweli tuliaminishwa kuwa anajua lugha nyingi sana kumbe anajua Kisukuma, Kizinza, Kiha, Kijita, Kikerwe,Kisubi etc. Kimataifa bado sana wote tulijionea uwanja wa Taifa. Amesoma Kemia. H20+Mg0=

Mh! Sitaki kuamini hebu nisubiri nimskie live akiongea
 
Msiwe na wasiwasi na kiingereza chake. Atapata walimu pale pale ikulu atakuwa vizuri tu. Aweke juhudi!
 
Sera ya ubinafsishaji no Sera ya CCM magufuli hana ujanja Wa kuikwepa Na kufufua viwanda au kujenga sio rahisi dunia ya Leo hakuna serikali inayojenga viwanda no wawekezaji mkuu suala la ajira sahau
 
Mwigulu atarud tena wizara ya fedha. Na apewe uwazir kamili atawanyoosha. Kasi ya Mh. Rais anaiweza na yeye yuko vizur. hzo chuki za majibu mabaya ni nyie tu. kiutendaji yuko poa.

Mwakyembe, unakosea saana kusema hajafanya kitu katka wizara zake. waulize wa uchukuzi. pale bandarin na Airpot watakufahamisha vizur. kaleta mpaka treni Dar kurahisisha usafir wa kwenda mjin. umesahau mgogoro wa wabongo kwenda kupokea wageni Jommo Kenyatta airpot?? alimalizana nalo hilo tatzo siku chache alipotua wizara ya EA.

Muhongo yuko vizur. alitoa majibu ya ukweli na Hakutaka kupundisha katika swala la gesi hasa upatikanaj wa vitalu.

hao watatu hapo juu mie sion anawaachaje katika baraza lake kwa mfano!!!...
 
... serekali miaka hii ijenge viwanda? what a dump! China na Cuba pamoja na ukomunisti wakishaacha long.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom