Urais ni Taasisi inayotakiwa kuwa na Ulinzi wa kiitifaki a.k.a Presidential Security Protocol, ili kumuwezesha anayekishika cheo hicho cha juu kabisa katika nchi awe salama na aongoze kwa muda mrefu akiwa salama.
Kuna faida kubwa Katika ziara za kushtukiza, kwamba unajionea hali halisi na kuchukua hatua Madhubuti. Hilo ni jambo jema, lakini ikumbukwe kuwa wakati unafanya hivyo, unazidi kujijengea marafiki wengi ambao ni wananchi, na wakati huo huo unajitengenezea maadui wachache waliokuwa na maslahi binafsi hapo mwanzo.
Hawa maadui wachache ndio wa hatari zaidi kwa mustakabali wa Ulinzi wa Kiongozi.
Sasa ili kuwa na Ulinzi thabiti dhidi ya hawa wachache wa hatari, inabidi ziara za Rais zile very secured kwa kuzingatia Presidential Security Protocol zote muhimu ili Kiongozi huyo wa nchi awe salama katika Uongozi wake.
HIVYO ZIARA ZA KUSHTUKIZA ZINA FAIDA KWA WANANCHI LAKINI ZINA HATARI KWA USALAMA WA KIONGOZI MKUU WA NCHI KAMA NILIVYOELEZA HAPO JUU.
NI MATUMAINI YANGU WAHUSIKA WATAUCHUKUA USHAURI HUU NA KUJIPANGA VIZURI KWA USALAMA ZAIDI.