Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Yaani kama kuna kitu kinauma maofisini ni kupewa watu vitengo wasio na tija katika taifa yaani kuna siku yule mwingine aliekuwa anapiga pasi ikulu akaacha pasi ina moto sijui alichukuliwa hatua gani aliposababisha moto
 
Rais anasimama kama figure ya Serikali, lakini Serikali ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Anabeba upanga, anakukata.
Warumi 13:1, 3-4 (SUV) Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;

kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.
 
Watumishi wa Mungu hawazawadii mahawara mali za umma:shetani::shetani::shetani:
 
Rais anasimama kama figure ya Serikali, lakini Serikali ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Anabeba upanga, anakukata.
Warumi 13:1, 3-4 (SUV) Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;

kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.

Unamjua Magufuli?
 
Mtumishi wa Mungu gani wakati Lowasa anatukanwa na wapambe wake alikuwa anashangilia,,Labda mtumishi wa lucifer
 
Rais wangu Magufuli jiweke mbali na siasa za Nyerere ambazo ndio liliolifikisha Taifa hili lilipo na kupitwa kimaendeleo na mataifa yote tulioyatangulia kupata uhuru

1.Azimio la Arusha: Epuka misururu ya maazimio. Nyeree alipolibuni Azimio hili alipingwa vikali na mwasisi mwenziwe Sheikh Abeid Amani Karume kuwa ni bovu na linapingana hata na imani za watu. Kwa ukaidi wa kutouona ukweli Sheikh Karume aliporudi tu Zanzibar aliitisha mkutano mkubwa wa hadhara na kuwaeleza wananchi ubaya uliojaa kwenye Azimio hilo. Karume siku hiyo alilipiga marufuku Azimio hili na kusema "MWISHO CHUMBE"

2.Rais Nyerere hakun'gatuka uongozi bali ulimshinda baada ya kulifikisha Taifa hili hatima ya kulifisika. Rais Mwinyi alipochukua madaraka nusunusu(chama kimeshika hatamu) alioweka bayana hayo na nchi ikaja kuokolewa na Rais Mugabe kwa kuipatia fedha za kuanza upya.

3. Mwalimu Nyerere alikuwa muoga wa upinzani na maisha yake ya uchaguzi alikuwa mgombea pekee. Hakuthubutu mtu kujitokeza. Mara pekee alipojitokeza na mpinzani ni pale alipokuwa akiwania kuwa mwenyekitI wa OAU. HAKUSHINDA

4. Siasa za Zanzibar: alikuwa haipendi Zanzibar na wakati mwingi aliiipa kisogo. Hata ile slogan maarufu inayotajwa sana "hatutoi dola kwa vipande vya karatasi (kura)" mfinyanzi alikuwa yeye.

5. Wazanzibari kindakindaki ni watu wastaarabu, wapenda amani na watulivu lakini werevu. Nii rahisi kutawalika lakini ni ghali wa kulighilibika

6. KILA LA HERI RAIS WANGU
 
Magufuli anafuata nyayo za mtangulizi wake JK.. ndio maana mpaka leo JK hachezi mbali na Ikulu
 
Aaagghhh sijaona ukweli wowote zaidi ya maelezo marefu,labda hapo kwenye azimio
 
Rais anasimama kama figure ya Serikali, lakini Serikali ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Anabeba upanga, anakukata.
Warumi 13:1, 3-4 (SUV) Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;

kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.
Huu msemo kwamba itii mamlaka kwa kuwa imewekwa na Mungu iachwe kwa wanaoamini lakini ziko mamlaka za kishetani duniani. mamlaka nyingi hutumia mpango wa siri kuangamiza wote wanaopinga mamlaka hizo.
 
Habari Tumeshuhudia Serikali ya raisi wetu mpendwa Mstaafu ikiongozwa na wakinamama wengi Je kwenye serikali ya Mzee wa kazi ataendeleza huo utaratibu?. Nimeuliza hili swali huku niangalia tamaduni ya Kisukuma inayotoa kipaumbele kidogo kwa kinamama na Safu ya Mameneja wa TANROAD ambako mzee alikuwa anahusika. #HAPANIKAZITU
 
Atajua yeye hakuna ubaguzi kama si legelege nivizuri kuwachagua tu
 
Habari Tumeshuhudia Serikali ya raisi wetu mpendwa Mstaafu ikiongozwa na wakinamama wengi Je kwenye serikali ya Mzee wa kazi ataendeleza huo utaratibu?. Nimeuliza hili swali huku niangalia tamaduni ya Kisukuma inayotoa kipaumbele kidogo kwa kinamama na Safu ya Mameneja wa TANROAD ambako mzee alikuwa anahusika. #HAPANIKAZITU

Hayo mambo yamebaki kwa JK na udhaifu wake kwa akina ... mda wa kazi wanaume wanatangulia daima na hizi ishu za wanawake kwangu ni upuuzi tu, wapewe wachache wenye uwezo haswa
 
Hivi ilaani ni nini.Si mikakati tu ambayo inabidi itumiwe ili kuwaletea wananchi maendelea yao.Mbona hamna akili zinazofikiri kwa mapana na marefu?CCM au CDM wote wana mikatikati mizuri tu.Si anachukua mkakati wowote depending on priorities.
mbatia alipewa ubunge na mwenyekiti wa ccm alikuwa anatekeleza ilani ipi?
 
Mh Rais,

Kuna kero nyingi zinasosababisha usumbufu mkubwa na hata kupelekea watu kuvunja sheria pasipo sababu kutokana na usumbufu huo.

MAMLAKA ZA USIMAMIZI

Tanzania ina mamlaka za usimamizi karibu kila sekta nyeti. Kuna EWURA, TCRA, TIRA, SUMATRA, etc zote zinalenga kusimamia sera, usawa na ustawi wa Taifa katika sekta husika. kati ya mamlaka zote mbili zina kero kubwa sana kwa wadau ambazo ni EWURA nA SUMATRA.

EWURA
Kila unit moja ya umeme watanzania wanayotumia kuna EWURA 1% plus REA 3% na VAT 18% (22% ni kodi tu) vivyo hivyo kwenye mafuta (petrol Diesel, mafuta ya taa) lakini tukirudi kwenye kazi za Ewura hatuoni ni namna gani mwananchi anafaidika nayo. Madhalani Budget ya serikali ya mwaka huu imeongezwa TZS 150 kwenye kila lita ya mafuta ya taa tukaambiwa ni kuongeza gharama za mafuta ya taa ili wasichachue petrol.
Swali Kama ewura wameshindwa kusimamia vituo vya mafuta visichakachue kwa nini wamuongezee mzigo mwananchi"
Kama EWURA wameshindwa kukagua vituo kwa namna yeyote ile na kuamua kuongeza gharama kwa mwananchi i wazi wameshindwa kuwahudumia wananchi na hawana uhalali wa kudai 1% au tozo yeyote badala yake waondoe hizo tozo waongeze adhabu kwa wakosaji. Kwa kuondoa tozo itawapa ahueni wananchi Mh Rais liangalie hilo kwa upana kama unataka kuboresha maisha ya kila mtanzania maana unagusa familia zote.

Kwa mwezi Tanesco inapata mapato zaidi ya 100billion (hivyo EWURA inapata 1% ni sawa na 1,000,000,000), EWURA hiyo hiyo yenye mapato makubwa kiivyo kwenye sector ya umeme tu imeshindwa kuwa na ofcn nchi nzima, imeshindwa kusimamia makampuni na vituo vya mafuta visivyozidi 6000 nchi nzima, Hivyo haina mandate ya kuendelea kuwatoza wananchi tozo kubwa kiivya.

Mbona hatuchajiwi TCRA kwenye simu? Mbona Hatuchajiwi SUMATRA kwenye ticket? Mbona hatuchajiwi TIRA kwenye Insurance? etc. Mh. Magufuli ondoa hizi TOZO zisizo na TIJA.

REA nayo ni kero maana ni 3% naamini price ya umeme imeangalia kila kitu (gharama ya kufua umeme, kusafirisha, kuusambaza na kukarababiti miundominu yake pamoja na maendelea ama upanuzi wa huduma). Hakuna kampuni inaweza kuendeleza huduma zake bila upanuzi na Huduma hivyo umeme Vijijini (REA) uwe ni mkakati wa serikali kuu na fedha zitolewe na serikali kuu kwenye budget zake na sio kuwanyonya wanunua umeme wachache. TANESCO ifanye review ya tariffs zake iachane na REA.

Mh. Magufuli Tuliambiwa na kuaminishwa pindi mitambo ya kinyerezi itakapowashwa umeme utashuka kwa zaidi ya asilimia 40 (40%) lakini hadi leo hatujaona hiyo ahadi ikitekelezwa sisi watanzania tupo kwenye Dilema hii itatekelezwa?

Ili taifa liendelee umeme ni jambo la msingi sana hivyo kuwa na umeme wa uhakika na wa bei nafuu ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hasa uchumi wa viwanda (kama ilivyo kwenye ilani ya chama chako) angalia upya ahadi hii iliyowekwa na watangulizi wako na chama chako kwa ujumla.

Itaendelea
 
  • Thanks
Reactions: 999
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom