Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Alafu ni bora na masifuri yapungue pia, Noti ya 10,000 ibadirike iwe 1000!!
 
This is s good proposal as much of our money in out of the banking system. It is a good option.
 
tumeshajadili hili swala hapa..na imeonekana ni gumu na linaweza lisisaidie sana..maana mafisadi yanajua ishu za uchumi kuliko sisi..maana mafisadi wengi ni wa TRA BOT n.k
 
Sadacta hata mimi nilifilia hivyo, breau de change zifungwe kwanza halafu zoezi la kubadilisha fedha lifuate , lakini uchapishaji wa note mpya ufanye kwa siri kubwa , apewe mkandarasi wenye viwango ,ikiwezekana ofisa wa BOT akajifunze Msumbuji, noti za msumbiji hasa ndizo zinazofaa
 
Alafu ni bora na masifuri yapungue pia, Noti ya 10,000 ibadirike iwe 1000!!

Mhhhh! Ingawa mie sio mchumi ila ili kuondoa hiyo sifuri ina maanisha kuongezea thamani fedha yetu na hilo halifanyiki kwa kubadiri fedha bali uzarishaji wa ndani kuuza nje.

Vinginevyo Mkwere angeisha badirisha kitambo.
 
Wana JF,

Rais wetu Dr. JPM mtu wa vipimo na viwango anaendelea kuwakonga nyoyo aliowahaidi kumwamini kuibadilisha nchi hii kutoka mzimu wa ufisadi kuwa nchi ya mfano, tiyari juhudi zake za operation OKOa pesa imetamaruki, njia mbili za kumsaidia kuokoa uchumi ni kubadilisha pesa za madafu haraka sana, hali hii itawafanya wafanyabiashara haramu waliokuwa wanaweka pesa zao kwenye mashimo na safe watakimbia kununulia vitu kama mashamba, nyumba na vitu vya thamani, watakaoshindwa kubadilisha basi ziwafie kwani kukaa nazo nyumbani hazina faida kwa uchumi wa nchi, watu hao watakimbia kuzibadilisha katika mfumo wa dola, hivyo dola zitakauka, ni vizuri kuwahi kufunga maduka yote yanayouza fedha za kigeni ili kuziba mianya ya kutorosha pesa, pesa zote zielekezwe kwenye mabenki ya serikali tu,

Jambo la pili, kwa kuwa pesa zetu zimetengenezwa kwa kiwango hafifu sana fedha hizi ziteketezwe utafutwe muundo mwingine wa fedha zetu ziongezewe ulinzi kwa kuweka halama zisizoweza kuigwa, hivyo atakuwa amewakomesha wenye mitambo ya kutakatisha fedha.

Hili Jambo nilikuwa namweleza mjasliamali mwenzangu Kama ulivyonena.

Nchi yetu itakuwa na sura mpya kiuchumi
 
Wakuu wasalam,
Baada ya Tafakari ya Kina na maumivu makali ya hivi vitu vinavyoibululiwa kila kukicha, japo naamini ni tone kati ya maji ya bahari nashauri ni Kwanini BUNGE LISIITWE KWA DHARURAa,
kwanza kabisa kujadili hali ya Ufisadi nchni hasa chini ya Serikali zilizopita,
Pili, kupitisha maazimio ya kuwapiga Risasi hadharani wahusika wote wa Ujambazi wa matrilion ya shilingi ,ikiwemo kuwafilisi kabla ya Risasi za moto na familia zao zijengewe makazi kwenye kijiji kimoja Tutakiita kijiji cha Ufisadi, ambapo hapo kwa Huruma serikali itawahudumia watoto wa Marehemu Mafisadi,
Inauma sana na Hapo ni maeneo mawili tu Bado Meng Mengi hayajafikiwa, Kama TANESCO KUPITIA LUKU, TANAPA KUPITIA UTALII NA UWINDAJI, GESI na Madini hapa ndo Balaa, Jeshi letu kupitia miradi, Makampuni ya Simu
Tatu Bunge liazimie kuitishwa kwa Bunge la Katiba ambapo hapo kwa kuwa sasa wote tu wamoja naamini maslahi ya nchi yatakuwa ya kwanza Ambapo Bunge la katiba haraka lianzie alipoishia Jaji Warioba na kuongeza na kupunguza Mengine ambapo Haitakuwa hata na haja ya kuchezea hela kupiga kura ya maoni hapo utekelezwaji wa Na uundwaji wa taasisi mpya chini ya serikal mpya Uanze, Hapa Tuungane wote bila mambo ya Vyama Na ndiposa la mwisho
La nne Bunge Liazimie Mshindi wa Uchaguz Zanzibar Atangazwe ili Tujenge Tanzania Mpya Yenye Mapya, 2020 tukienda kwenye uchaguzi tubishane mambo ya Msingi
Ni hayo Tu.
 
Mafundi cherehani mpooooo!! Jiandaeni kupunguza nguo za vigogo vitambi kwishnei
 
Wana JF,

Rais wetu Dr. JPM mtu wa vipimo na viwango anaendelea kuwakonga nyoyo aliowahaidi kumwamini kuibadilisha nchi hii kutoka mzimu wa ufisadi kuwa nchi ya mfano, tiyari juhudi zake za operation OKOa pesa imetamaruki, njia mbili za kumsaidia kuokoa uchumi ni kubadilisha pesa za madafu haraka sana, hali hii itawafanya wafanyabiashara haramu waliokuwa wanaweka pesa zao kwenye mashimo na safe watakimbia kununulia vitu kama mashamba, nyumba na vitu vya thamani, watakaoshindwa kubadilisha basi ziwafie kwani kukaa nazo nyumbani hazina faida kwa uchumi wa nchi, watu hao watakimbia kuzibadilisha katika mfumo wa dola, hivyo dola zitakauka, ni vizuri kuwahi kufunga maduka yote yanayouza fedha za kigeni ili kuziba mianya ya kutorosha pesa, pesa zote zielekezwe kwenye mabenki ya serikali tu,

Jambo la pili, kwa kuwa pesa zetu zimetengenezwa kwa kiwango hafifu sana fedha hizi ziteketezwe utafutwe muundo mwingine wa fedha zetu ziongezewe ulinzi kwa kuweka halama zisizoweza kuigwa, hivyo atakuwa amewakomesha wenye mitambo ya kutakatisha fedha.

Kwenye jambo la pili umejichanganya mkuu. Fedha kuwekewa ulinzi na fedha kutakatishwa ni mambo mawili tofauti. Security features zinazowekwa kwenye fedha au document yeyote yenye face value zinaweza kughushiwa ndio mana kuna 'super dola' (feki ) mbazo alama zake za ulinzi ni sawa na dola halisi na utambuzi wake lazima uingie maabara maalum kuweza kuzitofautisha dola halali na feki.

Utakatishaji wa fedha (money laundering ) hufanywa kwa fedha zilizopatikana kwa mfano umeuza madawa ya kulevya then fedha hiyo ukaitumia kununu kiwanja kisheria, ukajenga jengo kihalali, ukapangisha, ukakusanya kodi n.k
 
hii ni dharau sasa, with less than a week baada ya ziara ya waziri mkuu, bado madudu ya tpa na tra yako pale pale.

Hawa jamaa wanadharau.


iliyobaki ni kuvunja hizi mamlaka na kuajiri upya.

Hilo ndio suluhisho.

Otherwise madudu yataendelea.
 
tangu ipitishwe bajeti ya serikali ya mwaka 2015/16 hakuna pesa ya maendeleo imepelekwa isipokua ndani ya mwezi mmoja aliokaa madarakani amesha peleka shs bilion 122 huyu jamaa akikaa madarakani miaka 5 itakuaje?
 
Huyu mtu ndani ya miaka miwili atakuwa amekamilisha ahadi zote alizotoa, kutoa ujenzi wa daraja la Coco beach-Aga khan ambao (technically speaking) hauwezi kukamilika in 2 years
 
Alianza na wizara ya fedha (MOF) akaja MUHIMBILI na waziri mkuu wake akajibu mapigo bandari (TPA) na TRA akarudi tena TPA. Nini mtazamo wako wewe kama mtanzania au mtu wa taifa lingine lolote unaeitakia maendeleo nchi hii?

Aendelee na kasi hii ya ziara za ghafla na kuwawajibisha "live" wazembe kupitia vyombo vya habari au unamtazamo tofauti juu ya hili swala?

Lipi ni pendekezo lako la sehemu nyingine upendayo ifanyiwe ziara?

Njoo tujadili kwa mustakabali wa taifa letu.

MUNGU ibariki Tanzania MUNGU ibariki Africa
 
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana serikali mpya ya Dr.MAGUFULI NA Mh Majaliwa katika utendaji wao wa kazi.Nachoweza kusema ni kwamba hawa watu wamejitoa kwa sana kuitetea na kuilinda Tanzania yetu kwa hali na mali,na nina Imani kuwa Watanzania bila kujali itikadi,rangi,chama,ukanda nk watampa ushirkiano mkubwa raisi Magufuli katika kutekeleza yale aliyokusudia kuijenga nchi.

Ilani ya CCM ni upuuzi mtupu. Waliotufikisha hapa ni hao hao MACCM;hivyo basi naoana umuhimu wa kujitolea kumlinda raisi wetu kwaajili ya vizazi vyetu.Maadui sasa wamekuwa wengi mno,ndani ya TANZANIA.Tanzania yetu iligeuzwa nchi ya familia,shamba la bibi,sehemu ya wanyan'ganyi na washenzi huku wenye nchi wakigandamizwa na kuumizwa huku sehemu ndogo ya hawa minyoo wakifaidi keki ya nchi.

I think its time to bring back our country to where it deserves.Nchi yetu ina hadhi na sauti kama nyingine nchi kubwa duaniani.
Napenda ku-quote Dr Magufuli alipokuwa anaongea na wafanyabiashara wa watz.Alisema "Nchi hii ni tajiri,inauwezo wa kuwa a donor country".Hapa raisi alimaanisha na hakusema kwa kuchekesha au hadithi tu.

Nathani sisi sote kama watanzania inatupasa kumlinda na kumtetea raisi wetu.
Msema ukweli mpenzi wa Mungu,mim sikuichagua ccm wala Magufuli.Maana nilijua atatekeleza yale ya washenzi wa kwenye chama chake.Lakini so far raisi Magufuli amesema "TANZANIA KWANZA ". hivyo sina budi kukubaliana nae na niko nae katika kila hatua kuijenga nchi yetu.

so back to my note,kama anayefahamu ninapoweza kwenda kujitolea kumlinda mkuu,mtetezi,mzalendo wetu MAGUFULI anipe data vizuri.

IDUMU TANZANIA YETU.
 
Huyu kweli ni mtumishi wa wananchi sio yule mwingine alikuw anatutumikisha tu wanyonge!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom