Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
1. Mh Rais, sitisha hili zoezi la bomoa bomoa kwa makazi na nyumba za wanadamu. Hakuna mtu anayependa kuishi kwa tabu na shida. Watu wamepoteza maisha tayari kwa kihoro, na mashinikizo ya damu; hasa wazee. Watanzania wasiku-reflect tena kuwa wewe ni muharibu wa makazi ya Watanzania.
Zoezi la bomoabomoa ni lazima liendelee ili kila MTANZANIA Ajifunze kuheshimu sheria za nchi.Linapaswa kudumu ili limalizike kabisa na mtu yeyote asiruhusiwe kujenga hata kibanda cha muda maana MBONGO UKIMRUHUSU KUKAA HATA KWA WIKI 2 SIKU UKIMWAMBIA ATOKE-ATAONA UNAMWONEA.BOMOAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

2.
Tengeneza mazingira ya kuwalipa wazee wetu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika mashariki, malipo yao. Kumbuka unapowahehimu wazee, unamgusa Mungu moja-kwa-moja.
Nakubari,ila kwa kuwa serikali inakusanya mapato nadhani tumpe muda

3.
Nyumba za ibada (za dini zote) zisibughudhiwe kwa namna yoyote ndani ya utawala wako, ndipo baraka zitakapoendelea kukujilia na kukupata. Barikiwa JPM.
Kila mtu akaguliwe,TATIZO KUBWA LATU WENYE WAFUASI WENGI NI KWAMBA WAO HUWA HAWAKOSEI HATA KAMA WAKIUWA MTU HADHARANI.UKIWADEAL UTAONEKANA UMEWADEAL KWASABABU YA AIDHA VYAMA VYAO,AU DINI ZAO.......................
 
Hii mifuko ni kero kwa mazingira haswa mijini... Unakuta mifuko hadi juu ya miti, kwenye mito.. Halafu ni hatari kwa afya pale inapotumika kuweka chakula cha moto kama chips.

Nchi kama Rwanda hairuhusiwi na ukikutwa nayo faini ya nguvu inakuhusu..
 
Hili umeliona sawasawa hii mifuko ya plas ndo mchafuzi mkubwa wa mazingira na sijui hivi wiwanda vipo humu nchini na kama vipo basi ni vya wakubwa fulani.

Asante kukumbusaha mkuu..
 
Hili umeliona sawasawa hii mifuko ya plas ndo mchafuzi mkubwa wa mazingira na sijui hivi wiwanda vipo humu nchini na kama vipo basi ni vya wakubwa fulani
asante kukumbusaha mkuu

Kikwete alipiga marufuku huku akichekacheka na akaweka vi_condition vya kijinga mwishowe akashindwa
 
Watz tulishakuwa na kasumba ya kuvunja sheria na kila alovunja alionekana mjanja.

Leo amekuja Farao osomjua Yusuph so hakuma namna. Kama wew ulibebwa na fulani kwa kuvunja sheria sasa ukae ukijua hakuna wa kukubeba leo maana kila alovunja sheria atashughulikiwa kwa namna yake.

Siku zote sheria iko kimya unapoifuata ama kutenda haki lakn ikifika hatua unaivunja ipo cku au saa utaijua tu sheria nin inasema.
 
1. Mh Rais, sitisha hili zoezi la bomoa bomoa kwa makazi na nyumba za wanadamu. Hakuna mtu anayependa kuishi kwa tabu na shida. Watu wamepoteza maisha tayari kwa kihoro, na mashinikizo ya damu; hasa wazee. Watanzania wasiku-reflect tena kuwa wewe ni muharibu wa makazi ya Watanzania.

2. Tengeneza mazingira ya kuwalipa wazee wetu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika mashariki, malipo yao. Kumbuka unapowahehimu wazee, unamgusa Mungu moja-kwa-moja.

3. Nyumba za ibada (za dini zote) zisibughudhiwe kwa namna yoyote ndani ya utawala wako, ndipo baraka zitakapoendelea kukujilia na kukupata. Barikiwa JPM.
Kwani wewe ndiye Mungu?
 
Magufuli anafikiri nchi ni vipesa tu.Sio na afya mzee.Plastic ni sumu.Hivi waziri husika ni nani hapa?
 
Ubavu anao na atapiga marufuku na wenye viwanda vifungwe hata kama wana produce mifuko kuuza nje hatuitaki.
Mifugo inakufa kila kukicha, mitaro inaziba, mbali na uchafu mifuko hii hata ikiwa na viwango kiasi gani bado inaharibu ardhi.
Na diapers ziangaliwe pia
 
Hao wote wa bonde la msimbazi walishapewa viwanja,cement mifuko 500 na mabati kila mmoja ktk lile eneo la Mabwe pande wamejengewa hospital,shule,umeme na mabomba ya maji lakini wao walimuona JK mpumbavu na lofa vile viwanja waliuza cement pamoja na mabati wakarudi hapo hapo, na hata Magufuli anayajua yote haya ndio maana apati kigugumizi kulitekeleza hilo japo walishavunja sheria lakini serikali kwa huruma yake ikafanya hisani hiyo.
 
PIGA MARUFUKU UKIWA NA MBADALA WAKE kwa bei nafuu kama hiyo mifuko, mfano mifuko midogo ya kitambaa iuzwa mia itawezekana?
 
Hii mifuko ni kero kwa mazingira haswa mijini...unakuta mifuko hadi juu ya miti,kwenye mito..halafu ni hatari kwa afya pale inapotumika kuweka chakula cha moto kama chips..Nchi kama rwanda hairuhusiwi na ukikutwa nayo faini ya nguvu inakuhusu

Ebwana tulia na soma maelezo ndani ya katiba. Mazingira ipo chini ya makamu wa rais. Yeye ndo wakufanya hao. Mh. Magufuli afanye mangapi? Yeye kama rais ataingilia pale patakuwepo uzembe kama utekelezaji wake utakua wakusua sua.
 
Kama Unaona Unampa Cheo Kikubwa Kutomhita Rais ; Hivyo Rais wetu Siyo Mr. Magufuli Bali Dr. Magufuli
 
PIGA MARUFUKU UKIWA NA MBADALA WAKE kwa bei nafuu kama hiyo mifuko, mfano mifuko midogo ya kitambaa iuzwa mia itawezekana?

Kwani nchi zilizozopiga marufuku wanatumia nn...au miaka kadhaa kabla ya hivyo vifuko tulitumia nini?
 
Mh. rais, hawa SUMATRA wanatesa sana wananchi maskini. Wanapokea rushwa toka kwa wamiliki wa mabasi ili kupanga nauli zinazowatesa wananchi. Sehemu ya kutumia nauli elfu tatu mtu unatumia elfu tano hadi sita.

Bei elekezi zinafahamika kabisa; njia ya lami kilomita moja ni Tsh. 25 hadi 35. na njia ya vumbi kilomita moja ni kati ya Tsh 50 hadi 60. Lakini watu wanalipa njia za lami hadi sh. 100 kwa kilomita, sehemu ya kutumia elfu 15 mtu analipa 20. Huku ni kumwibia mwananchi.
 
Sumatra ni jipu jingine linalohitaji kutumbuliwa na mtumbua majipu. Hakika ukitumbua jipu hili watu watafurahi sana
 
tunataka tujue nani aliempa uda ruti ya feri mnazi mmoja alafu ana chaji 400..... na mabasi mengine hayaruhusiwi kupita iyo ruti nani katengeneza hii monopoly
 
Kuwa mkweli,SUMATRA wanafanyakazi nzuri anzia nsuli za train,bus na meli.
Mfano daladala toka simu 2000 hadi mbezi shs 400,hapa kuna km 8.usilaumu tuu toa mifano na ushahidi ueleweke
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom