Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Zanzibar hakuna mgogoro, kwani uchaguzi umeshafanyika? Subirini uchaguzi muone kama swala la Zanzibar litamsumbua JPM huyu ndie rais atakayewanyoosha wote waliokuwa wanafaidi pesa za walipa kodi bila kunawa mikono.
ha ha wew upo wap? xax huo uchaguz lin?
 
Zbar hakuna mgogoro labda km unataka kuuanzisha ww. Wenzio saivi wanajiandaa kwa uchaguzi mwingine.
 
Dar es Salaam, Tanzania. Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Mambo ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga kuanza kushughulikia
mgogoro wa Burundi na ametaka kazi hiyo afanye kwa kushirikiana na
waziri wengine kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Huu utakuwa mtihani wake wa kwanza kwa Balozi Mahiga ambaye
aliapishwa hivi karibuni kwenye wadhifa huo baada ya kuteuliwa na
Rais kuwa mbunge. Balozi Mahiga aliliambia gazeti moja akisema
kuwa, ameagizwa kushughulikia kiini cha mzozo huo na tayari wakati
wowote alitarajiwa kuwasili Bujumbura kuanza mazungumzo.
Hata hivyo, alitarajiwa kuwasili kwanza mjini Arusha kwa ajili ya
majadiliano na Katibu Mkuu wa EAC, Dk Richard Sezibera na baadaye
kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kushughulikia mzozo huo.
Tanzania ndiye mwenyekiti wa EAC.
Wakati hali ya wasiwasi ikiendelea kujitokeza Burundi, ripoti zinasema
kuwa zaidi ya raia 1O0,000 wamewasili nchini kwa ajili ya kuomba
hifadhi tangu mzozo huo ulipoanza Aprili mwaka huu.
Wakati Tanzania ikianzisha juhudi mpya kuhusiana na mzozo huo,
kuna ripoti kuwa Umoja wa Afrika (AU) umeanza kujadili uwezekano
wa kutumwa jeshi la Afrika Mashariki nchini humo kwa lengo la
kuzima ghasia na machafuko yanayotishia kuitumbukiza nchi hiyo
kwenye vita vya ndani.
Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika limesema hali ya
Burundi ni mbaya na kwamba hatua za dharura zinahitaji kuchukuliwa
ili kuepusha nchi hiyo kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa
wenyewe.
Kamishna Mkuu wa baraza hilo, Ismail Chergui ameandika kwenye
ukurasa wake wa Twitter akisema kuwa mauaji nchini Burundi ni
lazima yakomeshwe. Baraza hilo la AU limefanya kikao cha dharura
kujadili kadhia ya Burundi na pendekezo la kutumiwa kikosi maalumu
kinachojulikana kama ‘East Africa Standby Force’ kwa ajili ya kudhibiti
hali ya mambo katika nchi hiyo limetolewa. Kikosi hicho kiliundwa
mwaka 2003 na kinajumuisha nchi za Kenya, Burundi, Comoros,
Djibouti, Ethiopia, Rwanda, Ushelisheli, Somalia, Sudan na Uganda.
Huku hayo yakijiri, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja
wa Mataifa amewalaumu viongozi wa Burundi kwa kuchochea ghasia
na machafuko nchini humo na kulitaka Baraza la Usalama la umoja
huo kuwawekea vikwazo vya usafiri viongozi kama njia moja ya
kuwashinikiza wakomeshe ghasia hizo.

CHANZO: Gazeti La Mwananchi

NOTE:
SAWA! ILA ZANZIBAR MBONA UMEWAPA KISOGO? AU YAMEKUSHINDA MH.???

Kuhusu zanzibar subiri tarehe ya uchaguz
Haina haja ta utatuz
 
Mambo Ya Zanzibar Bado Yako Ndani Ya Uwezo Wa Wazanzibari Wenyewe Kuyamaliza. Watu Tunajiandaa Kurudia Uchaguzi, Mgogoro Uko Wapi Hapo?
 
Hapo ndipo naliona Neno la Mungu kuwa kweli daima. Miaka zaidi ya 2000 ilopita Bwana Yesu akamwona JPM akiwekwa wakfu kuwa rais wa Tanganyika.
Akasema hivi; Toa kwanza Boriti iliyomo jichoni mwako ndipo ukione kibansi kilichomo ndani ya jicho la mwenzako.
Mzee JPM, maliza Zenj, ndo uende Burundi. Uchokozi wote Burundi ulianza kwa kuibeza katiba ka weye unavyocheza na katiba ya Tza.
Pole sana, ukiona mwenzio ananyolewa, nawe zako tia maji
 
Zanzibar hakuna mgogoro, kinachosubiriwa ni tarehe ya kupiga kura basi.
 
Nyumbani bado hapajachafuka na pia tunasubir huo muda ulopangwa wa miez mitatu..so its still a good move kusuluhisha majirani...
 
Wana JF,
Habaru zenu

Nianze kwa kumpongeza Rais Magufuli kwa uzalendo alionao!

Tumo katika zama za kutumbua majipu. Tumemulika sana upande Wa uchumi au mapato ya serikali. Utumbuaji Wa majipu TRA, TPA, PCCB nk.... ni jambo linalotupa faraja.

Japo tumeangalia uchumi, lakini kuna jipu LA AJIRA KATIKA OFISI ZA UMMA. Naamini ni kubwa kuliko yote.

Watanzania tuna haki ya kupata ajira serikalini kwa misingi ya uadilifu. Zisiangaliwe dini, kabila, koo, eneo tunakotoka na jinsia. Cha kuangaliwa uwe uwezo Wa MTU kufanya kazi husika.

Kwa masikitiko makubwa, ajira serikalini zinazingatia dini, kabila na kanda katika wizara na mashirika mengi. Ukuu wa idara unazingatia dini, kabila na kanda. Huu mdudu umeanza kututafuna na utatupeleka pabaya sana.

Tutajikuta tuna dini fulani au kabila fulani ndiyo limeendelea kiuchumi sana kuliko dini au makabila mengine.

Kuna baadhi ya mashirika kama TRA, TPA, NSSF, baadhi ya mabenki nk...., yamelalamikiwa kuwa na ukabila na udini.

Tumefika mahali tumeanza kusema, kwa mfano, kupata kazi maliasili lazima uwe kabila fulani. Kupata kazi Tra lazima uwe kabila fulani, kupata kazi nssf lazima uwe dini fulani.....

Hii nchi ni yetu sote. Tuna haki ya kupata ajira kwa usawa bila upendeleo.

Namuomba Muh. Rais aunde tume ya kuchunguza jambo hili. Kwa mfano, Je TRA kuna zaidi ya nusu ya wafanyakazi kabila moja au dini moja! Kama ni hivyo kwa nini? Tuendelee na uchunguzi katika mashirika na wizara zote. Penye mapungufu ajira ziitishwe upya na uwiano uzingatiwe.

Bila kufanya hivi, watu wataendelea kuvutana na baadhi ya kabila, dini na kanda zitaendelea kuwa za wasindikizaji. Watoto wao hata wakisoma haitokua rahisi kupenya katika ajira serikalini. Barua za kazi lazima zitaendelea kuwekwa kapuni.

TANBIHI
Tuache mtindo Wa kukwepa kuzungumzia udini na ukabila. Tunazidi kulifanya jipu hili liwe kubwa zaidi na sugu. Kadri linavyozidi ukubwa watu wanazidi kuumia. Rais Magufuli tafadhali Pasua jipu hili.
 
Huo wimbo wa UKABILA na UDINI kaimbe na familia yako. Kama hukidhi vigezo usitake ubebwe kwa ajili ya dini ama kabila lako.
 
Ni kweli kabisa...ila asiishie kwenye makampuni tu...ende hadi kwenye vyama vya kiasa...tunashuhudia baadhi ya vyama ili kupata cheo cha uongozi ni lazima uwe umetokea ukanda flani au umeoa koo flani..
 
Hili ni nafikiri ni jipu ambalo limekomaa sana, kama ukifuatilia ofisi nyingi ajira zimekua zikitolewa kwa upendeleo ama ukabila, udini, undugu kama hivyo si sababu basi rushwa inachukua nafasi yake.
Nafikiri kutumbua jipu hili kunahitaji mkakati na dhamira ya dhati ya mtumbuaji na watumbuliwaji.
Ndio maana waliosoma wanatafuta kazi ila wenye vyeti feki wanapata kazi kiulaini.
 
Jipu la kuajiri kwa kigezo cha dini na kabila Lipo sana kwenye baadhi ya taasisi za serikali,ukienda TRA 80% ni kutoka kule na ukienda NSSF 90% ni dini Ile.
 
Kuna mdogo wangu ni Dentist mzuri sana alisomea Cuba amemaliza internship Muhimbili miezi michache iliyopita but hadi leo hii hana ajira. Baadhi ya madaktari Muhimbili walimshauri awe lecturer pale na akakubali but hadi leo hana ajira. Nashindwa kuelewa tunaelekea wapi - haya mambo ya udini na ukanda ndio yanayochangia kudumaa kwa utendaji wa serikali na huduma za jamii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom