Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Yote hayo usemayo ni sahihi ila ndio hivyo tena kamwe haiwezekan kwenye hik kizaz chet. Nafuu bas tungewaandaa hawa madago ambao ndio kizaz chet kichajo lakin ndio hivyo tena imetoka tumeshindwa na hao ndio watakuwa maamuma hata kutuliko.

Inasikitisha hii nch chin ya hik chama aina dira.

The only solushen ni Individual development baas!
Ndiyo Zimbabwe iliharibika, Napenda sana Jeuri ya Mugabe, Lakini alichukua Ardhi bila Kutumia Utaratibu Mzuri, Angeweza Kuchukua Nusu ya Mashamba akawaachia Wakulima Wakubwa Nusu. Na Pia Kuwawezesha Wazalendo na Kuwapa Utaalamu wa Kuendesha Nusu au sehemu ya Nusu Nyingine. Na Kiasi Kingine akawagawia Wananchi wa kawaida Ekari moja au Mbili nao walime chakula. Lakini Akakurupuka na Matokeo ndio haya. Na Baadaye Imegundulika Kuwa Mugabe naye Ni Fisadi mkubwa tu Kama Mobutu, Ni huo Mdomo tu!

Ila Naweza Kuapa Kuwa Pamoja na Madhaifu ya Magufuli, sio Fisadi hata Chembe!
 
Ndiyo Zimbabwe iliharibika, Napenda sana Jeuri ya Mugabe, Lakini alichukua Ardhi bila Kutumia Utaratibu Mzuri, Angeweza Kuchukua Nusu ya Mashamba akawaachia Wakulima Wakubwa Nusu. Na Pia Kuwawezesha Wazalendo na Kuwapa Utaalamu wa Kuendesha Nusu au sehemu ya Nusu Nyingine. Na Kiasi Kingine akawagawia Wananchi wa kawaida Ekari moja au Mbili nao walime chakula. Lakini Akakurupuka na Matokeo ndio haya. Na Baadaye Imegundulika Kuwa Mugabe naye Ni Fisadi mkubwa tu Kama Mobutu, Ni huo Mdomo tu!

Ila Naweza Kuapa Kuwa Pamoja na Madhaifu ya Magufuli, sio Fisadi hata Chembe!
Mugabe aliathirika na vikwazo vya uchumi alivyowekewa na Western. Na Sio kunyang'anya mashamba.
The policy was pure cool.
Ndio maana nchi zA Africa zilishindwa kumkosoa.
 
Mm namuomba rais magufuli akimaliza msako walioficha sukari aje na msako waliyo ficha pesa uku mtaani pesa ni adimu afadhali na sukari walio ficha pesa awana niya njema na rais wetu na wakikamata hizo pesa tugaiwe wananchi bure
 
Sometimes Maamuzi ya JF ya Kutumbukiza Mada Katika Mada Nyingine, Inaweza Kuwa Nzuri Lakini Mara nyingi Inazipoteza na Kama Zilikuwa na Swala la Maana Linapotea. Nimefuatilia Mara Nyingi Kichwa cha habari Kikifanana tu Mada Zinaunganishwa. Moja inakuwa tu Kama changizo na inapotea baada ya Dakika chache!
 
Mugabe aliathirika na vikwazo vya uchumi alivyowekewa na Western. Na Sio kunyang'anya mashamba.
The policy was pure cool.
Ndio maana nchi zA Africa zilishindwa kumkosoa.
Hilo najua, Lakini aliwapa Kisingizio cha Mashamba, Na Uzalishaji wa Chakula Ulishuka kwa sababu hiyo. Uingereza Walichukia sana Kwa Kuwa walikuwa Wanaingiza Chakula Kingi hasa Mboga kutoka Zimbabwe kwa Bei nzuri.
 
Hilo najua, Lakini aliwapa Kisingizio cha Mashamba, Na Uzalishaji wa Chakula Ulishuka kwa sababu hiyo. Uingereza Walichukia sana Kwa Kuwa walikuwa Wanaingiza Chakula Kingi hasa Mboga kutoka Zimbabwe kwa Bei nzuri.

Unajua mkuu, hakuna nchi ya kiafrika Ambayo iko huru kwa asilimia 100% .
Hata Tanzania haiko huru. Ile wanasema ni sovereignity ni myth kuliko reality.

Huwa tuna mipaka ya kujiamulia mambo yetu. Kuna invisible hand unao operate juu ya sheria zA nchi zetu.

Pia kuna ukweli kua Malengo ya Mugabe yalilenga kumuongezea power or influence kwa wananchi kuliko ukombozi wa kweli, kama ilivyokua kwa Sadam Hussein alipoivamia Kuwait na kusababisha vita ya ghuba ile ya miaka ya 90s.(operation desert storm).
Mugabe alikaza akawa amefeli.

Kitu cha Msingi may be Baada ya somo kusomeka..nadhani angewaPa uraia wale watasha. Kuliko kuwatambua kama wageni.kwa miaka mingi waliyokaa.
Kama hapa tized Nyerere aliwapa utaifa wahindi.
 
Mh Rais umekuja na falsafa mpya mpya ya Hapa Kazi tu ukiwa unataka kuongeza ufanisi kwenye serikali yako. Kosa moja umeanza kulifanya ni kuteua watu ambao aidha wamekaa serikalini muda mrefu wamelemazwa na mazoea (wengine tangu enzi za nyerere hadi Mkapa wamehudumu).

Ukweli ni ngumu sana kuwabadilisha watu hawa kuendana na kasi yako unayotaka watakuangusha tu.

Kundi la pili ni la watu wenye umri mkubwa zaidi ya 60 uwezo wa kufikiri unakua mkubwa lakini uwezo wa kutenda mdogo ni natural phenomena soma Life cycle hypothesis inaelezea kwa kina. Kundi hili litumie zaidi kwenye maswala ya ushauri tu nafasi za utendaji wame vijana.

Kuwabadili hawa wenye umri mkubwa ni ngumu kwani wengine wanaamini wanajua kuliko wewe kwa sababu wamekuzidi umri, wengine wanasema wamekuwa wakitenda hivyo siku za nyuma ndio mana wanaonekana watendaji wazuri.

Kubwa zaidi ni kwamba mazingira ya kiutendaji yanabadilika kwa kasi kutokana na mabadiliko ya teknolojia n.k hivyo young generation inauwezo wa kubadilika kwa haraka kuliko makundi hayo mawili.


Sababu ya tatu ni kwamba kuna kundi kubwa la wasomi wasio na kazi mtaani na moja ya mtoa ajira mkuu nchini ni serikali. Teuzi mbali mbali ni sehemu ya kuongeza ajira nchini, Mh Rais, teuzi mbali mbali za board, wakuu wa wilaya, mikoa, mashirika ya umma, balozi, etc ni vyema ukawateua vijana. Sio lazima umchukue kutoka mtaani unaweza teua ambao tayari ni watumishi kisha nafasi zao kujazwa na wapya na vingine.

Ni mategemeo yangu kuona serikali ufanisi iliosheheni vijana wenye weledi mkubwa, usiofanya kazi kwa mazoea au hofu bali proffessionalism

Nawakilisha
 
Yapo maeneo vijana wanafaa zaidi kuliko "wazee wa miaka" 60. Kwa kazi za kutoa maamuzi ajira mpya si mahali pao hadi uwapime utendaji wao.

Wapo wenye umri mdogo wana utendaji dhaifu kuliko hao wanaoitwa wazee.Serikalini miaka 60 ni ukomo wa kuajiriwa,lakini vyuo vikuu makini Dunia nzima hawa hawaondolewi.
 
Chief,
suala la utendaji mmbovu kama mtu halina umri (anaweza kuwa kijana au mzee) lakini mtendaji mzuri akizeeka ufanisi wake unapungua. Ndio maana kwenye vyuo vikuu mhadhiri kufundisha hadi 70 sio shida ukilinganisha na kuwa na mkurugenzi katika shirika kama NSSF, SIDO, TBS, TFDA ambao kila kukicha kuna mambo mapya ya kuyafanyia kazi.

Ndio maana pia sio wote tunaweza kuteuliwa bali wale wenye uwezo mkubwa watateuliwa sisi wenye uwezo wa kati na wachini tutaendelea kuajiriwa
 
Rais ameteua kwa kubalance. Wazoefu (tunawaita wazee) wamo. Damu changa wamo.
Wateule wasituangushe.
 
Kuna wimbo wa bendi ya zamani hapa Tanzania usemao,mwanadamu hharidhiki hata ukimpa nini,milele hatoridhika....aaah,ni baadhi ya maneno ndiani ya wimbo.Kabla ya kuingia JPM watu walikaririwa wakisema wana kiu ya kumpata rais ayethubutu,kaingia JPM wengine mara hana subira n.k,huyo rais mliyemtaka ni yupi?mbona hamna shukran kwa Mungu,mie ningedhani kwa sasa ingelikuwa ni kumsaidia ayakamue vipi si kusema aache kukamua,du mwanadamu upewe nini,majirani wanataman angelikuwa wao,sasa nauliza yule wenye uthubutu tuliyeomba aingie siyo huyu?
 
Kama sipo sahihi naomba kuelimishwa....

Sikusoma uchumi...ila nakumbuka kwenye jiografia Viwanda vya chuma vilijulikana kama mama wa viwanda vyote..

Tunakimbizana kuelekea Tanzania ya viwanda lakini habari ya ujenzi wa angalau kiwanda cha chuma hakuna...

Tutafika kweli Tanzania ya viwanda bila viwanda vya chuma.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom