MKWEPA KODI
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 28,701
- 71,056
Alikwisha Sema hataki ushauri wa aina yeyote ndiyo maana anasema tumechezewa kwa miaka hamsini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ashauliwe na nani wakat ataki kupangiwa... alafu washauri wake ndo polepole na bashite unategemea nini
Sitaki kuamini kuwa hashauriki
Ni wakati sasa aachane na washauri wa namna iyo ikiwemo pia waliokuwa washauri wa Nyerere kwa kuwa kusema kweli hawakumshauri vizuri mwalimu kupelekea nci kuanguka vibaya sana kiuchumiAshauliwe na nani wakat ataki kupangiwa... alafu washauri wake ndo polepole na bashite unategemea nini
Hajafikia kuwa wa ovyo. Ana nia nzuri, anahitaji washauri wazuri kumpa approach nzuriTuna Rais wa hovyohovyo mno
Acheni limuangukie si anavunga superhuman sanaNi wakati sasa aachane na washauri wa namna iyo ikiwemo pia waliokuwa washauri wa Nyerere kwa kuwa kusema kweli hawakumshauri vizuri mwalimu kupelekea nci kuanguka vibaya sana kiuchumi
Ni vizuri awe makini. Duniani ukitaka upate lazima utoe kikubwa ni kutumia akili na busara zaidi. Tanzania sio kisiwa.Alikwisha Sema hataki ushauri wa aina yeyote ndiyo maana anasema tumechezewa kwa miaka hamsini
Amani iwe nanyi wadau.
Natumaini mu wazima na mnaendelea vizuri na majukumu yenu Ni vizuri pia kabla ya yote nikatoa pole kwa watanzania wote walioguswa na tukio la kinyama dhidi ya kiongozi wa upinzani Bw Tundu Lissu.
Nikiwa sijaonekana kitambo sana kwenye jukwaa hili leo napenda kusema kuwa kwa yanayoendelea nchini Tanzania kwa sasa, imebidi niamue kujitokeza tu na labda niamue kutoa mchango wangu wa mawazo hata kama hayatasikilzwa lakini nikiwa na Imani kuwa haya mawazo kwa kuwa ni mazuri na yanajenga basi yatasikilizwa na kufanyiwa kazi.
Sipendi kwenda kwenye hili la Lissu ila kwa kuwa nia yangu ni ya kumsaidia Mh Raisi naona kwa hili la Lissu linaweza kupata utatuzi wake humuhumu.
Kwanza nianze na maana halisi ya wasaidizi wa Mh. Raisi ni kina nani hasa- Kama hamjui kwa Tanzania hawa wanaanzia na baraza la mawaziri ambalo kisheria na kikatiba ndicho chombo kilichopewa mamlaka ya kumshauri Mh. Raisi juu ya mambo yote ya nchi. Kwa hapa Tanzania washauri wengine ni mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wasaidizi wengine wa Mh Raisi.Wengine ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa nini leo nimeamua kuwaelezea hawa watu na kuongea na hawa watu????
Hawa ndo watu wa kumsaidia kumwambia ukweli Mh.Raisi, ukweli wa kiuchumi, ukweli wa kisiasa hata kijamii. Bila shaka kwa hali ilivyo sasa napenda kusema kuwa wasaidizi wa raisi hamfanyi wajibu wenu ipasavyo na inapoelekea nchi itaenda kuanguka chini ya raisi Magufuli. Naomba nielezee kwa mifano hili suala.
KIUCHUMI.
Pamoja na Mh Magufuli kuwa na nia njema kwa nchi hii kiuchumi napenda kusema kuwa mmekuwa mnapotosha vibaya sana Mh. Raisi kiuchumi kiasi kwamba nchi imekuwa ikipata matokeo hasi zaidi kiuchumi zaidi ya chanya.Swali langu kwenu ni kwa nini mmeshindwa kumshauri Mh Raisi juu ya kuanza na njia ya kupiga marufuku vitu wakati mlishaona hili lilianza kuleta matokeo hasi???
Kwenye sukari wasaidizi wa raisi mlipaswa kujifunza sana kwenye suala hili kwa sababu tangu Mh.Raisi apige marufuku uingizaji wa sukari bei ya sukari haijaweza kushuka kuwa kawaida hadi leo hii. Swali langu kwenu hamkujifunza kitu kwenye suala hili???? Hamjui kuwa bei ya sukari hadi leo haijawa kawaida na hili limepelekea nia nzuri ya Mh Raisi ishindwe kuonekana hapa???
Sio tu kwenye sukari, mlishindwa kumshauri Mh Raisi vizuri kwenye pesa kuondolewa kwenye benki za biashara na hadi leo hali ya kifedha imekuwa mbaya sana nchini hasa kwenye mzunguko na upatikanaji wa mikopo.
Kubwa zaidi mliloshindwa kumshauri Mh. Raisi ni hili la Acasia. Hivi ni nani aliwaambia kuwa wazungu unapambana nao kwa mabavu na sio akili? Hamjaona hili suala la Acasia linamuweka Raisi na nchi sehemu mbaya sana kiuchumi? Hivi hamkuona haja ya kumshauri Mh Raisi angeanza na kubadili sheria tena at least kwa kujifanya anawashirikisha hao wawekezaji wa madini alafu badae kunatokea maoni ya wadau ndo tunafikia kurekebisha sheria kwa muktadha tunaoona sie??? Hamkuona hi indo ilikuwa njia sahihi ya kudeal na suala la madini bila kucreate tension kwa dunia juu ya hali ya uwekezaji Tanzania???
Mmemuacha Mh Raisi ametumia nguvu kubwa kudeal na issue ya madini kwa kuzuia usafirishwaji wa makinikia kiasi ambacho kimeleta picha mbaya sana kiuwekezaji hapa kwetu. Kusema kweli mmeiweka Tanzania sehemu mbaya sana kiuwekezaji na pia hata hifadhi yetu ya pesa za kigeni itaathilika sana kwa kuwa kuondoka kwa Acasia msidhani itakuwa raisi kwa muwekezaji mwingine kuja Tanzania kama amefikiria vizuri kwenye kucalculate risk za kuinvest Tanzania. Kwa nchi yenye miaka mingi ya uhuru hii haikuwa approach tuliyotakiwa kuitumia kwenye kudeal na hawa ngozi nyeupe.
Mnamuacha raisi atamke juu ya vita vya uchumi hadharani. Hivi mmeshindwa kumshauri Mh Raisi juu ya madhara ya nchi kutangaza hadharani vita dhidi ya maslahi yao kiuchumi?? Au mnataka siku ya mwisho nchi itapata nini??? Mnadhani kama nchi itafaidika chochote kwenye vita dhidi ya maslahi ya kiuchumi ya wanamagharibi au wanamashariki??? Hamuoni Zimbabwe?? Hamuoni Venezuela??? Hamuoni Libya na Syria???? Mnataka Magufuli aje kukumbukwa kwa sifa mbaya zaidi????
KISIASA.
Mmeshindwa kumshauri Mh Raisi vizuri kiuchumi na mbaya zaidi hadi kisiasa mnaharibu kwenye kumshauri Mh. Raisi vizuri kiasi ambacho leo adui akitumia siasa kutuvuruga anatumaliza kesho asubuhi tu. Hivi kulikuwa na haja gani ya kumshauri raisi kuwafungulia mashtaka wapinzani kila wanapomsema??? Hamuoni hili linawatengenezea huruma kwa wananchi na siku ya mwisho wananchi kuwasikiliza na kuwaamini wao zaidi kuliko wanavyoiamini serikali au Raisi wao???? Mmeshindwa nini kumshauri Mh. Raisi kuimalisha kitengo cha propaganda na uenezi cha chama chake ili kiweze kujibu kila shutuma dhidi ya Mh.Raisi na siku ya mwisho kuanzia wananchi hadi wageni waone kuwa ni game za kisiasa tu????? Hamuoni kutumia vyombo vya dola kujibu hoja za kisiasa zinamuharibia raisi kimataifa n ahata kuharibu taswira ya nchi kimataifa????
Kwako Mh. Raisi, bado nakuamini sana, kama nilivokupigania kwenye uchaguzi sitaacha kukuigania kwa nia ya kutaka uongoze vizuri. Ila naomba uchague wasaidizi wa uhakika wanaojua dunia inavyoenda na figisu zake na mwisho wape uhuru wa kukushauri kwa weredi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Hizo ni allegations/assumptions nzito sana ndugu. Kikubwa asikilize washauri wake na washauri wake wamwambie ukweli.Ukweli ni kuwa, ukitaka asikie ushauri basi huu ujumbe mpelekee Kagame, Museveni, Nkurunziza, au Odinga. wakikaa nae chini wiki tu anaelewa
Sent using Jamii Forums mobile app
Sitaki kuamini kuwa hashauriki. Tumuombe aanze kuwasikiliza washauri wake na pia washauri wake watumie weredi katika kumshauri vizuri.Huyu mtu hashauriki hata kwa sekunde moja. Ni one man show na anajiona yeye ndiye yeye hakuna mwingine ajuaye zaidi yake ndiyo sababu kukurupuka kila mara na kuingiza nchi kwenye matatizo chungu nzima.
Kawatisha kwa kuwatumbua hata kama hawajatenda kosa lolote lile! Kumbuka yaliyompata Nape dhidi ya kutimiza wajibu wake kama Waziri kufuatia uvamizi wa Clouds Studio.
Kama ndo ivo wafanyavo wanakosea sana. Ni wajibu wao sio tu kumshauri bali pia kumshauri katika ukweli kwa mustakaabali mpana wa maslahi ya taifa.Washauri wake wote wanasubiri aseme halafu wao ndio wacheze na hiyo hisia yake. Washauri wake wote wanajali maisha mazuri kwa nafasi alizowapa, wanaogopa kumshauri asichopenda vitumbua vyao vikaungia mchanga. Simply hamuamini yoyote kutoka hao wasaidizi wake na hasa tabia yake ya kuwapa maelekezo kwa kufoka ndio anawanyamazisha kabisa.
Kibaya zaidi hao wasaidizi wake ni wanafiki wa kutupwa, wanajifanya wanamsupport lakini akitoka madarakani ndio utaona rangi zao. Huoni washauri wa JK nao siku hizi wanasema nchi ilikuwa imeoza?