Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila nyerere nae bwana, anawaita majina watoto, Makongoro, Maharage??Kwanza Shikamoo mheshimiwa Rais!
Mheshimiwa Rais, haya ninayokuandikia naomba uyasome kwa utulivu, uyazingatie na uyafanyie kazi maramoja kwa faida ya nchi.
Rais Magufuli, kama utaendelea kutawala kwa mtindo huu, awamu ya tano haitakumbukwa kwa idadi ya ndege mpya zilizonunuliwa, wala idadi ya ‘flyovers’ zilizojengwa, wala idadi ya viwanda vipya vilivyojengwa bali itakumbukwa kwa idadi ya maiti zilizookotwa katika fukwe, idadi ya watu waliopotea, idadi ya risasi alizomiminiwa mheshimiwa Tundu Lissu na kikundi cha watu wasiojulikana, itakumbukwa kwa idadi ya wapinzani waliotupwa jela, idadi ya wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani waliohongwa na kuhamia CCM. Awamu ya 5 itakumbukwa kwa kuua na kubomoa!
Ndugu Rais ushauri wangu kwako ni huu:
1.Acha kuwaridhisha CCM kwa kuua upinzani na kudhoofisha demokrasia nchini. Soma tena kiapo chako, uliapa kuilinda, kuitetea na kuihifdhi Katiba ya Jamhuri na ukamuomba Mungu akusaidie! Mfumo wa vyama vingi upo kwa mujibu wa Katiba uliyoapa kuitetea na kuilinda! Kujaribu kubomoa, kudhoofisha au kuua vyama vya upinzani ni kuvunja Katiba na kumkejeli mwenyezi Mungu! Ndugu Rais, Mungu hajaribiwi wala hakejeliwi! Hawahawa wanaokuchekea na kujipendekeza kwako leo na wewe unawapa vyeo na madaraka makubwa katika chama na serikali, ndiyo haohao watakuita ZIRO siku utakapoachia madaraka!
2.Mheshimiwa Rais, sehemu ya ibara ya 3 ya Katiba ya Jamhuri inasema hivi: ‘Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa’ . Hii ina maana kuwa, vyama vya upinzani ni mguu wa pili wa nchi, mguu mmoja unao wewe na serikali yako, mguu wa pili ni wa upinzani. Bila mguu wa pili kutembea hatuendi popote ndugu Rais! Viache vyama vya upinzani vifanye kazi yake kwa mujibu wa Katiba ili nchi itembee kwa miguu miwili!
Waite viongozi wa kambi ya upinzani kama ulivyowaita viongozi wa dini, mjadiliane, mpatane nchi itembee kwa miguu miwili!
3.Mwisho ndugu Rais, saluti ni ishara ya heshima na utii anayoitoa askari kwa ofisa aliye mkubwa kwake au kiongozi mkuu wa kitaifa anayemwakilisha Rais nk. Unapoteua mtu asiye na maadili mema katika jamii na kumpa mamlaka makubwa na hadhi ya kupigiwa saluti, unawadhalilisha sana maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaompigia saluti mtu huyo na pia unaidhalilisha sana hadhi ya Ikulu na haiba ya nchi kitaifa na kimataifa! Hakikisha wateule wako wanakidhi viwango vya maadili na hadhi ya kupigiwa saluti.
Ndugu Rais ikikupendeza waweza kuniandikia barua pepe kupitia nyereremaharage@yahoo.com
Ndimi Maharage Burito Wa Nyerere!
Mi naona wewe si mwanademokrasia. Maana ya demokrasia ni hiyo unayoiona. Watu wanahama kutoka huku kwenda kule muda watakao. Au kwako mkuu demokrasia ni Lema kutoka TLP na kujiunga na CDM tu lakini kina Waitara wakifanya the same ishakuwa kuua vyama vya siasa? Mi naona wewe ujitafakari upya. Hayo mambo ya hama hama unayoyaona Hiyo ndiyo Demokrasia.Kwanza Shikamoo mheshimiwa Rais!
Mheshimiwa Rais, haya ninayokuandikia naomba uyasome kwa utulivu, uyazingatie na uyafanyie kazi maramoja kwa faida ya nchi.
Rais Magufuli, kama utaendelea kutawala kwa mtindo huu, awamu ya tano haitakumbukwa kwa idadi ya ndege mpya zilizonunuliwa, wala idadi ya ‘flyovers’ zilizojengwa, wala idadi ya viwanda vipya vilivyojengwa bali itakumbukwa kwa idadi ya maiti zilizookotwa katika fukwe, idadi ya watu waliopotea, idadi ya risasi alizomiminiwa mheshimiwa Tundu Lissu na kikundi cha watu wasiojulikana, itakumbukwa kwa idadi ya wapinzani waliotupwa jela, idadi ya wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani waliohongwa na kuhamia CCM. Awamu ya 5 itakumbukwa kwa kuua na kubomoa!
Ndugu Rais ushauri wangu kwako ni huu:
1.Acha kuwaridhisha CCM kwa kuua upinzani na kudhoofisha demokrasia nchini. Soma tena kiapo chako, uliapa kuilinda, kuitetea na kuihifdhi Katiba ya Jamhuri na ukamuomba Mungu akusaidie! Mfumo wa vyama vingi upo kwa mujibu wa Katiba uliyoapa kuitetea na kuilinda! Kujaribu kubomoa, kudhoofisha au kuua vyama vya upinzani ni kuvunja Katiba na kumkejeli mwenyezi Mungu! Ndugu Rais, Mungu hajaribiwi wala hakejeliwi! Hawahawa wanaokuchekea na kujipendekeza kwako leo na wewe unawapa vyeo na madaraka makubwa katika chama na serikali, ndiyo haohao watakuita ZIRO siku utakapoachia madaraka!
2.Mheshimiwa Rais, sehemu ya ibara ya 3 ya Katiba ya Jamhuri inasema hivi: ‘Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa’ . Hii ina maana kuwa, vyama vya upinzani ni mguu wa pili wa nchi, mguu mmoja unao wewe na serikali yako, mguu wa pili ni wa upinzani. Bila mguu wa pili kutembea hatuendi popote ndugu Rais! Viache vyama vya upinzani vifanye kazi yake kwa mujibu wa Katiba ili nchi itembee kwa miguu miwili!
Waite viongozi wa kambi ya upinzani kama ulivyowaita viongozi wa dini, mjadiliane, mpatane nchi itembee kwa miguu miwili!
3.Mwisho ndugu Rais, saluti ni ishara ya heshima na utii anayoitoa askari kwa ofisa aliye mkubwa kwake au kiongozi mkuu wa kitaifa anayemwakilisha Rais nk. Unapoteua mtu asiye na maadili mema katika jamii na kumpa mamlaka makubwa na hadhi ya kupigiwa saluti, unawadhalilisha sana maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaompigia saluti mtu huyo na pia unaidhalilisha sana hadhi ya Ikulu na haiba ya nchi kitaifa na kimataifa! Hakikisha wateule wako wanakidhi viwango vya maadili na hadhi ya kupigiwa saluti.
Ndugu Rais ikikupendeza waweza kuniandikia barua pepe kupitia nyereremaharage@yahoo.com
Ndimi Maharage Burito Wa Nyerere!
Wewe ndiyo unawaza na kukumbuka hayo maana mliyatengeneza wenyewe lakini sisi bado tunatambua mchango mkubwa wa Mh. Rais katika kutransform Nchi hii na hatutausahau ng'oo.Yeye anadhani atakumbukwa kwa kununua ndege anasahau mpaka sasa watu wameshasahau kuwa alinunua Bombadier bali wanakumbukumbu zaidi matukio ya Lissu kupigwa risasi, Aqulina kuuwawa kwa risasi,wanasiasa kununuliwa na mengine yanayoendelea.
Ukweli unaochoma.[/QUOTE