Habari wakuu,
Nimejaribu kufikiri sana juu ya wema alionao rais magufuli kwa wananchi wake na watanzania kwa ujumla, nikawaza pia na najua ipo siku rais magufuli na awamu yake wata staafu pia kama ilivyo taratibu za nchi yetu.
Mh Rais inawezekanaje mbunge kapigwa risasi waliompiga hawajulikani hadi leo?, kama haitoshi pesa ya matibabu kanyimwa kwa hoja za ajabu ajabu na zilizojaa dharau na kiburi cha madaraka, amejaribu kupambana na stahiki zake amenyimwa sasa.
Ni Mungu yupi mnaye mwabudu?, ni mioyo ipi mlionayo?, ni watanzania wapi manohubiri kuwatumikia??, mnadhani watanzania upole wao ni ujinga wao??, Lisu amefanya nini hadi mumtende hivi?
Ingilia kati mh rais , maliza hili swala kwa busara na kumwogopa Mungu mnayeenda makanisani kila siku kumwabudu, dhambi hii haitawaacha salama kamwe, hata kama siyo leo hata miaka ya badaye mtajutia unyama huu, hata kama siyo nyinyi hata vizazi vyenu vya nne vitajutia.
Najiuliza mnapoudhuria misiba huwa mnajifunza nini au mnawaza nini? , hamtakuwa waheshimiwa milele ipo siku mtaitwa marehemu na vyoote mtaviacha.
Inauma sana kuona binadamu mwenzio anonewa kiasi hiki . Limalizeni hili swala waheshimiwa maana ipo siku mtatakiwa kujibu kwa lazima.