Nimezungumzia suala la kupendwa au suala la watu kuonekana kufurahia na kuombea rais akutwe na umauti?! Hata JK watu walikuwa hawampendi lakini hatukuwahi kushuhudia haya!! Hizi kauli za kwamba sijui "mtenda haki", sijui nini na nini ni kujaribu kufanya ujanja wa mbuni, kuficha kichwa chini wakati kiwili kiwili kinaonekana!!!
Tumeshuhudia majumba yakibomolewa hovyo hovyo kule Kilwa Rd... ndo utendaji haki wa wapi huo?!
Tumeshuhudia watu wakipotea, akina Saanane, Azory Gwanda, na wengine kuokotwa kwenye viriba, n.k... mnataka kusema huko ndo kutenda haki?!
Kwanini msifikrie hiyo ndiyo sababu iliyowafanya watu wapige shangwe badala ya hizi kauli mbiu za kutenda haki?! Kawatendea haki nani dhidi ya akina nani, ili tujiridhishe hao "dhidi ya..." ndiyo waliokuwa wanafurahia?!
Unafiki na kujidanganya ndio kawaida yetu. Nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, sheria lazima ifuatwe. Hata Yesu alikataa nyumba ya baba yake kuwa gulio la walowezi.
Watu walikufa kwa migomo ya madaktari, walimu waligoma mpaka elimu ikaporomoka, madudu lukuki ya aibu yamefanyika, usijisahaulishe. Watu walifikia hatua ya kuwekeana sumu na kuuwana waziwazi. Soma kuhusu sekretari wa Mwakyembe, watu walimwagiwa tindikali, ujambazi kila kona, hakuna wa kumuamini kati ya askari na jambazi au wewe hukuwepo nchini?
Nafsi yako inafahamu ukweli, iulize itakwambia, tulia, usiulize hasira zako. Watu wamesaidiwa kutenda haki, waliofoji vyeti watapata nafuu, sasa angalau watazikwa na majina yao halisi, watu waliishi wakifahamu kuwa hayo wanayoishi nayo si majina yao, fikiria uchungu kiasi gani? Mnamzika ndugu yenu kwa jina tofauti, anazaa inabidi watoto wake nae wawe na majina yasiyo yake, yasiyo ya ukoo yake.
Angalau ametusaidia sisi watenda maovu angalau kupata nafuu kwa kuadhibiwa kwa makosa ambayo tunafahamu fika tuliyatenda kutokana na nguvu ya mfumo ilivyotupeleka.
Watu wanakufa kila siku, ndio asili ya binadamu, amekufa Chacha Wangwe, amekufa Amina Chifupa, amekufa Mtikila. Kufa ni lazima kwa binadamu.
Kama hujaifahamu dunia rejea maandiko yanavyosemwa toka dunia iumbwe, wajinga, wapumbavu na wasiopenda haki ndio wameijaza dunia.
Pia, japo ukweli mchungu, popote duniani, uongozi bora ni ule unaohakikisha maslahi ya wengi lazima yatamalaki dhidi ya maslahi ya wachache by any means possible.
Ongea na nafsi yako, hakikisha unajiuliza hivi hili jambo ninalolisema kuhusu Azory Gwanda, kuhusu Ben Saanane, kuhusu voroba vya maiti ninalifahamu kwa hakika au hisia zangu tu? Nafsi yako itakuambia, kamwe nafsi haitakudanganya. Itakuambia pia kama wewe ni mtenda na mpenda haki au wewe ni dhulmati na mpenda dhulma. Wewe iulize tu, itakuambia!