Kiukweli ukitoa protokali za urais za mh Magufuli yeye binafsi ni mwana Sana Tena msela kabisa ila sijui atajinasua vipi na kifungo Cha Ben sanane na Azory Gwanda ila jpm ni mwana Sana Tena msela Sana Mungu amlinde!
Alianza vibaya sana, kwa kutaka watu wote wamuogope yeye.
Unakumbuka akina Lema walivyowekwa mahabusu miezi kadhaa?
Na "Dikteta Uchwara" ilivyomtia ukichaa, huku makesi yote Lissu akiyapangua?
Alipotoka huko, akaona atengeneze masheria ya kikandamizi, ya kunyima watu uhuru na haki zao; na kama hiyo haikutosha akaona kwamba wapinzani kuendelea kufanya siasa kutamnyima alichokitamani sana...'sifa' .
Akapiga marufuku mikutano ya siasa ili abaki yeye peke yake akitamba na kufanya kampeni miaka minne yote. Kabinafsisha TBC, kila akigeuka huku anasikika yeye pekee.
Kaweka magenge kila sehemu waimbe nyimbo zake tu, lakini wapi, bado haridhiki na haoni kama waTanzania wamekogwa roho zao.
Kaanza kujitangaza mwenyewe, kwamba hakuna aliyefanya kazi kubwa kama yeye, waTanzania wanamsikiliza tu hawasemi kitu.
Kwa hiyo ana hofu kubwa hapo alipo. Anajua akiruhusu uchaguzi ulio huru kabisa, ataangukia mchanga licha ya kufanya mambo mengi ambayo waTanzania wengi wanayaona kuwa ni mambo mazuri kwa taifa. Lakini wengi hawaoni maana ya kuuza haki zao kwa gharama ya miradi hiyo inayofanyika, pamoja na uzuri wake.
Aliponyakua Mahakama na Bunge, vyote viwe mfukoni mwake, hapo katimiza kabisa kuwakatisha tamaa waliokuwa wakisubiri kwamba atarekebisha aliyokwisha haribu.
Rekodi yake imekwishaganda. Watu hawatekwi na hawapotei ovyo tena, lakini kumbukumbu zipo na hofu zinaendelea kwamba huenda ni mapumziko tu ya muda.
Mengi ya haya asingeruhusu yamchafue, kwa hakika msimamo wake wa kulinda mali za taifa hili na hii miradi mikubwa ingemfanya awe kiongozi wa kuheshimiwa na kukumbukwa. Kwa hakika, asingehangaika kamwe kupiga kampeni kwenye chaguzi zinazokuja..
Sasa hivi ni lazima awategemee polisi na wasimamizi wa uchaguzi kuwa na hakika ya kuchaguliwa ngwe nyingine.