Maoni: Vunjabei apokonywe dili la Jezi - Simba

Nasema Uongo Ndugu Zangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
279
Reaction score
779
Hakuna ubishi kuwa club ya Simba ndiyo club yenye heshima kubwa kimataifa iliyopo hapa nchini.

Kuna jambo halipo sawa katika club yetu, mwaka jana na mwaka huu kuna mambo mawili yametokea ambayo kwa maoni yangu hayakupaswa kutokea.

Ukiyachunguza ni kana kwamba tuna hujumiwa na aliyepewa dhamana.

1. Kuvuja kwa jezi kabla ya siku ya uzinduzi, sote tuliona kilichotokea mwaka jana, jezi zilivuja kabla ya wakati tena zilivuja siku zaidi ya 5 kabla ya siku ya uzinduzi na hili likafanya uzinduzi rasmi usiwepo.

2. Mwonekano wa jezi, kiukweli mwaka jana jezi hazikuwa na hadhi inayo endana na timu yetu, watani walituchapa kwa upande huo.

Mwaka huu tena tumeanza kuona jezi inayo sadikiwa kuwa ni ya Simba kwa msimu huu, kwa maoni yangu nadhani tumshukuru bwana Freddy na tutafute mtu mwingine maana hii ya mwaka huu ni kama mapazia ya chumba cha kuhifadhia maiti.

Tatizo liko wapi? Tunazo rangi nzuri sana nyekundu na nyeupe, tunakwama wapi? inamaana tumeshindwa kupata mbunifu ?
 
Hakuna ubishi kuwa club ya Simba ndiyo club yenye heshima kubwa kimataifa iliyopo hapa nchini.

Kuna jambo halipo sawa katika club yetu, mwaka jana na mwaka huu kuna mambo mawili yametokea ambayo kwa maoni yangu hayakupaswa kutokea.
...
Hivi umbea unalipa sana?
 
Mbona nzuri tatizo ni ile MO Foundation imekaa sehemu mbaya kama sio makalioni basi ipo kiunoni kama shanga.
 
Haya mambo ya kumpa mtu tenda ya jezi matokeo yake ndy hayo jezi haina mpangilio mzuri wa rangi,bora wangekuwa wanatangaza wazabuni wanaoweza kudesign jezi then wanaangalia nani kadesign uzi mkali kuliko mwingine basi anapewa tenda
Ila kwa staili hii hapana hiyo jez haijakaa poa
 
Naunga mkono hoja.
Haiwezekani ronya unalivaa mara moja tu malalamiko kwa vunja bei ..
Halifai hata kuwa tambara tuwaige yanga.
 
Yan vijitu vingine bana kisa una bando basi unapost ujinga...hivi ulichoandika hapa mbona kama umekatwa vidole gumba...ww tunaweza kupa tenda ya jez ya watu kumi tuu na ukashindwa...acha kijana afanye kazi ..,,
 
Utopolo achane wivu ,vunjeni mkataba na huyo wa kwenu aliyeweka magofu ya kaole kwenye jezi
 
Yan vijitu vingine bana kisa una bando basi unapost ujinga...hivi ulichoandika hapa mbona kama umekatwa vidole gumba...ww tunaweza kupa tenda ya jez ya watu kumi tuu na ukashindwa...acha kijana afanye kazi ..,,
Hakuna ujinga wake hapo kasema ukweli
 
1. Kuvuja kwa jezi kabla ya siku ya uzinduzi, sote tuliona kilichotokea mwaka jana, jezi zilivuja kabla ya wakati tena zilivuja siku zaidi ya 5 kabla ya siku ya uzinduzi na hili likafanya uzinduzi rasmi usiwepo.
Kuvuja kwa jezi kunaathiri kitu gani?
NB: Simba ilishachukua B zake kwa Vunjabei, iliyobaki ni yeye kuzirudisha kwa kuuza jezi
 
Yan vijitu vingine bana kisa una bando basi unapost ujinga...hivi ulichoandika hapa mbona kama umekatwa vidole gumba...ww tunaweza kupa tenda ya jez ya watu kumi tuu na ukashindwa...acha kijana afanye kazi ..,,
Simba sio ya kudhalilika hivi
 
jezi kama hii ilivuja pia mwaka jana. Kinachomuuma mleta mada ni jezi ya Simba kutovuja. namshauri afiche upumbavu wake
Wewe lofa kilichofanya mwakajana tusifanye uzinduzi si jezi zilivuja zikapostiwa mpaka na akina Manara badae uzinduzi uka ahirishwa? Mwaka huu tena ndiyo hivyo wanatuletea mapazia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…