Maoni ya baadhi ya watu juu ya njia ya kupambana na #corona kwa nchi za Afrika

Maoni ya baadhi ya watu juu ya njia ya kupambana na #corona kwa nchi za Afrika

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Ameandika mmoja wa wasomi wa falsafa, Castor Mduda, aliyejikita kwenye maadili na siasa ameandika, #CoronaVirus ni Hatari sana lakini Kuvizuia kwa kuwatesa wananchi kwa kuchukua hatua ngumu na tatanishi kwa watu ni hatari pia

Ni vyema Busara ikazingatiwa na Viongozi wa Afrika katika kuchukua hatua za tahadhari. Lazima tuelewe kuwa mazingira yetu sio sawa na ya Mataifa makubwa. Tunaweza kupambana na #Covid19 na tukamudu halafu watu wetu wakafa kwa kupigwa na Polisi na njaa. Wengi wetu ni wajasiriamali/ wamachinga zaidi.

Mwishowe tukawa na tathmini kuwa #CoronaVirus haijaua hata mmoja halafu Njaa imeua maelfu au #CoronaVirus imeua mamia na Njaa imeua Maelfu. Lazima kupiga mahesabu ya fikra vizuri tukizingatia Uhalisia wetu.

Alimalizia kwa kusema ‘Busara iwaongoze zaidi Viongozi wetu Afrika’, ameandika haya baada ya uvunjifu wa haki za binaadamu unaoendelea kwa baadhi ya nchi za Afrika baada ya kuweka zuio la kubaki ndani.

Aidha nchi kama India umasikini wake unaendana kiasi na nchi nyingi za Afrika kumekuwa na uvunjifu wa haki za binaadamu baada ya zuio hilo. Hii inaonyesha ni muhimu kuwa na zuio lakini tuangalie uhalisia wa mazingira yetu.
 
Hao wanaospray huko Kariakoo wanapoteza fedha za walipa kodi na hawana ujuzi wa magonjwa ambukizi wanatafuta sifa za kisiasa tu.
 
Mimi nafikiri tuanze na dhana kubwa iliyojikita sasa hivi ya kuwa mtu mweusi haathiriwi sana na Corona, Tuanze kwa kuwafuatilia wagonjwa wote waliougua kwa siku za karibuni tuone waliathirika kwa kiasi gani na iliwachukua muda gani kupona, mfano mdogo ni huu:

Familia ya Mbowe ambayo mtu mmoja aliugua lakini Familia yote haikuugua kwanini? ni body resistance? au tahadhari kubwa au dhana yetu ya kutoathiriwa sana, Pia tuangalie kwa jinsi gani watu waliokuwa karibu na Isabela Mwampamba wameathirika kwa kiasi gani?

Hii itatusaidia kujua uhalisia wa tatizo tulilonalo, mfano kama watu wote waliokaribiana na Isabela hawakuugua je ni body resistance au ni lucky?

Kwa tathmini ya waathirika wawili na yule wa Tatu wa Zanzibar tunaweza kujua hatari ya Ugonjwa huu.
 
Self isolation inafanikiwa Uingereza, idadi ya wagonjwa wapya inapungua.
 
.
Screenshot_20200330-144149.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom