Mimi nafikiri tuanze na dhana kubwa iliyojikita sasa hivi ya kuwa mtu mweusi haathiriwi sana na Corona, Tuanze kwa kuwafuatilia wagonjwa wote waliougua kwa siku za karibuni tuone waliathirika kwa kiasi gani na iliwachukua muda gani kupona, mfano mdogo ni huu:
Familia ya Mbowe ambayo mtu mmoja aliugua lakini Familia yote haikuugua kwanini? ni body resistance? au tahadhari kubwa au dhana yetu ya kutoathiriwa sana, Pia tuangalie kwa jinsi gani watu waliokuwa karibu na Isabela Mwampamba wameathirika kwa kiasi gani?
Hii itatusaidia kujua uhalisia wa tatizo tulilonalo, mfano kama watu wote waliokaribiana na Isabela hawakuugua je ni body resistance au ni lucky?
Kwa tathmini ya waathirika wawili na yule wa Tatu wa Zanzibar tunaweza kujua hatari ya Ugonjwa huu.