Hapa ndipo 'shida' iliko -- kwenye 'vina vya tafsiri' juu ya 'Akili' na 'Utashi'.
Hauhitaji kusema 'mimi ninatambua...' kama vile haya ni mambo ya hoja ya ubishani--kama vile 'maoni'; Maoni si 'Maarifa'--vivyo hivyo sayansi si 'maoni'. Kadiri yoyote ya hata sayansi kuwa ni 'Maoni' ni nyumba iliyojengwa kwenye mchanga ama tuseme jumba la makuti kwenye nyika; huweza kusambaratikia mbali pepo kali za kuvuma wakati mmoja hata mwingine...
Haya ni mambo ya kiufundi kabisa... Hayana cha 'Unafsi' labda tu 'Mazoea' ya tabia ya utu wa kujitafsiri hivi ama vile kwa kuwa 'unapenda'--ama kufikiria kama wengine wengi. Nasibu ya kujua ilivyobora huhitaji nidhamu ya kuwa tayari kuikana nafsi na basi 'uono wako uwe fasaha' na wenye kujitegemea wenyewe.
...
Tazama hiyo picha ya 'Trizania'--ruhusu 'akili yako ya ndani itafsiri'; achana na akili ya nyama kwenye hiyo itakutoa kapa!
Hizo alama nne zina ufunguo kwa ajili ya 'ufunuo' kuhusiana 'Utashi' wa 'ndani na nje' ya mtu.
Alama ya juu ni alama ya 'Mboni ya Jicho', ni hiyo mboni ya jicho ipo kwenye fraktali tunayoweza kuiita 'Mpango Mzima'. Kwa kuwa hiyo ndiyo fraktali ya 'Uono'--uono ulio ni hatma ya kubangua utatusho wa 'Mtenda-Kitendo-Matokeo'.
Fraktali ya Kushoto-chini, hiyo unayoiona ni picha-gramu ya 'Utaasisi' ambavyo kiufundi ni alama mbili katika moja; MSALABA na MKASI. Alama hizi mbili ni akitipu ya 'Imani' na 'NIa' katika moja. Msalaba ni alama ya 'Imani' inayoshikilia 'Mbingu na Nchi'. Kwa hivyo pande nne za msalaba huwakilisha 'Ardhi', 'Maji', 'Upepo' na 'Moto'. Mkasi ni alama ya 'Ulinzi wa Malango'--ni alama ya uaminifu kwa ajili ya 'Shika Neno, Tenda Neno'. Kwa hivyo zao la Msalaba na Mkasi kiufundi ni 'UTASHI'.