Maoni ya Director General wa WHO kuhusu lockdown kwa nchi masikini kama Tanzania

Maoni ya Director General wa WHO kuhusu lockdown kwa nchi masikini kama Tanzania

Nilidhani Total Lockdown kwa nchi masikini haiwezekani.., ila niliyoyaona India yalinibadilisha mawazo..., Ushauri usingoje nani atasema au atafanya nini wewe na familia yako mjitayarishe kama ambayo hayawezi kufanyika yakifanyika...

Uhalisia ndio utadetermine maamuzi, na kama maamuzi yatatoka kwa panic na bila kujiandaa kweli wengi watakufa (always prepare for the worse)
 
Hapa ndipo unafikia hatua ya kusema Mungu aliwaumba weupe kwanza then akawaumba watu weusi baada ya miaka millions ...... wametuacha mbali mno...why

Ni kweli kabisa umaskini wa Africa sasa upo wazi kabisa - hii COVID 19 imeuweka wazi wazi - kwamba 80% ya watu wake hawana akiba ya chakula hata cha masaa 48.... Lockdown Africa haiwezekani.....watu watakufa... Serikali zetu choka mbaya haziwezi kuwalisha watu hawa hata kwa siku 30.

Mbaya zaidi viongozi wa Africa huwa hawasemi ukweli kuhusu umaskini wa bara hili lenye raslimali lukuki - ni aibu.....
 
Hata Mimi siungi mkono hoja..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi mkuu mfano wale jamaa daywaka anaeamka asubuhi hana kitu.anaingia kariakoo anapiga mishe akipata elf 3 ndio anakula ..hizi wale watu wanaweza kukaa hata siku 5 ndani? Hata kama ukiweka vifari nje??
Lockdown is the best way of controlling Corona. Lakini kwa hapa kwetu total lockdown ni shida kwa kweli kwa sababu ya umaskini na hata serikali siamino kama itaweda kumudu kulisha familia zote maskini zikiwa lockdown all in all tuombe mungu balaa hili liishe

Sent using Jamii Forums mobile app
Walianza kubisha kuzuia ndege... baada ya hali kuwa tete wakazuia.

Sasa wewe endelea kupinga tu siku ikiingia kwenye familia yako ndio utajua umuhimu wa lockdown.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown si rahisi kwa nchi zetu,watakufa wengi kwa njaa. Hakuna anayelazimishwa kutoka,wanaotaka lockdown wajifungie wao. Labda tuzuie mikusanyiko,mf nyumba za ibada,minada,mikutano nk
 
Kwa hiyo ni bora ufe kwa korona?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuangalie measures zingine,maana hiyo lockdown ni ngumu kwetu. Tusisitize social distancing kwa kuepuka mikusanyiko, kila mtu kuvaa barakoa(zipatikane za bei nafuu,tutengeneze za kwetu kwa vitambaa vya pamba), kuhimiza usafi... Lockdown iwe mwishoni kabisa. Huwezi kumfungia mwenye njaa,ngumu. Hata hivyo mitaani watu wanapungua sana(wamejifungia),wanatafuta elimu ya corona kwa kila namna,tunafuatilia taarifa mbalimbali bila kulazimishwa. Hiari yashinda utumwa
 
Uzuri wa hilo gonjwa huwa haliangalii nani ni nani. Linaua wote, rais, waziri, mlalahoi nk.

Viongozi ni zaidi kwa vile wana umri mkubwa, na wengine wana vibetri kwenye moyo.

Hivi punde watajua umuhimu wa lockdown, mara yatakapowafika

Sent using Jamii Forums mobile app
Itafikia kipindi mtu anachagua kati ya corona au njaa. Ambapo mimi bora corona inakupiga hata week 2.. lakini njaa siku 3 tu hinyanyuki.
 
Kwakweli saga likichanganyia watu watapotea mtaani wenyew kwa sasa tuendelee na maandaliz ya lockdown yajayo yanasikitisha
carcinoma,
Dunia nzima HAKUNA. Narudia tena HAKUNA anaependa LOCKDOWN.

Ila wamelazimishwa na HALI ILIVYO TETE.

Hata hapa kwetu huu UBISHI wa kuanza kujadiliana kuhusu kuwepo na LOCKDOWN au ISIWEPO ni MBWEMBWE tu za UZIMA kwa kuwa ZAGA haijachanganyia.

Siku wakianza kukata MOTO watu 2000 kwa siku huku NEW CASES zikiwa 3000 kwa siku. Hapo hakutakuwa na MJADALA TENA wala MABISHANO.

Hata Trump anatamani watu warudi kazini hata sasa ila ndio hivyo HALI TETE, Hairuhusu. Tena alitamani wamarekani warudi kazini kabla ya PASAKA ila imeshindikana, amebaki tu kuwa MOTIVATIONALA SPEAKER Twitter maana mafanikio yake yote ya miaka 4 ( JOBS +STOCKS MARKET ) yameliwa na COVID-19.

Refer: Trump, despite virus warnings, wants US back at work by April 12

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown hatuhitaji.. kinacho hitajika ni kufunga mipaka, wananchi wapewe mask, lab za kupimia walau kila mkoa, mikoa iliyo adhiriwa ijitenge
Habari za mida hii wakuu.
Kufuatana na janga hili la ugonjwa wa COVID 19 unaosababishwa na kirusi cha corona,
Kumekuwa na mjadala kuhusu lockdown ya nchi nzima ambapo baadhi ya watu wanamtaka Rais wa nchi aidhinishe total lockdown.
Na wengine wakitaka hali iwe hivi hivi ilivyo.

Ninadeclear interest kwamba mimi ni mmoja wa watu ambao hawaungi mkono jambo la total lockdown sababu ikiwa ni kwamba nchi kama yetu ambapo kipato cha watu wengi kinategemea kufanya kazi kula siku ndio wapate ridhiki zao.. sasa ukifanya total lockdown kuna watu watu watakufa kwa njaa.

DG wa WHO amesema ili kufanya lockdown inabidi upime uzito wa athari za watu kukaa ndani na kutoka nje..

Chini hapa ni screenshot ya press ya DG wa WHO ambapo ameongelea kuhusu lockdown kwa developing countries View attachment 1418364View attachment 1418365

Nini maoni yako..

#carcinoma01

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown si mchezo,spain leo wameanza kurudi makazini mdogo mdogo,na huku kasi ya maambukizi ikiwa haijapungua kihivyo
 
Mpaka sasa tulipaswa kuwa na formal modal ya maisha inayoonyesha jitihada za dhati kudhibiti/kupunnhuza maambukizi.
Hiyo ya WHO haiwezi kutusaidia.
 
Tanzania ilivyo kataa lockdown nchi zingine zilisema sisi WAKAIDI, leo hii wameona nani alikuwa sahihi.

Sehemu ambazo watanzania wanakutana na kuchanganyika na raia wengi wa mataifa ya mbali ni Zanzibar, Dar, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza. Ni rahisi kudhibiti hayo maeneo na kuhakikisha raia wengine wanajikinga kwa kuwa wasafi, kuvaa mask na kuzuia mikusanyiko.
Sema nini hapo haujagusia ukweli kwamba sasa kitu inatembea local host to another local host.
 
Huyu muethiopia DG ana akili sana. Kuna manyang'au yanatamani lockdown. Wewe kama maisha yako mazuri jifungie ndani na mkeo. Wengine tunaogopa njaa kuliko hiyo corona.

Kuna lingine hapo juu limeandika mwezi mmoja au miwili watu hawawezi kufa njaa. Yaani linaongea rahisi tu. Ukiwa mtoto wa mama au maisha mazuri huwezi jua siri ya kambi ya maisha ya watu wa chini.
 
Mkuu carcinoma mifano ya kujifunza mbona tayari iko Kenya, Uganda na Rwanda? Lockdown kule inafanywaje? Kafa mtu njaa au hapana? Inasaidia au haisaidii?
 
Mkuu carcinoma mifano ya kujifunza mbona tayari iko Kenya, Uganda na Rwanda? Lockdown kule inafanywaje? Kafa mtu njaa au hapana? Inasaidia au haisaidii?
Kenya watu waliuawa na polisi wanazidi waliouawa na corona (source ni aljazeera).
Hata hivyo kenya lockdown iko usiku tu.. mchana ni free kutembea..

Hata uganda hawajafanya total lockdown watu bado wanatembea mchana tu ndio maana hakuna aliyekufa njaa..

Rwanda sina data.

Kubali kataa kwa nchi zetu total lockdown HAIWEZEKANI!!
 
Huyu muethiopia DG ana akili sana. Kuna manyang'au yanatamani lockdown. Wewe kama maisha yako mazuri jifungie ndani na mkeo. Wengine tunaogopa njaa kuliko hiyo corona.

Kuna lingine hapo juu limeandika mwezi mmoja au miwili watu hawawezi kufa njaa. Yaani linaongea rahisi tu. Ukiwa mtoto wa mama au maisha mazuri huwezi jua siri ya kambi ya maisha ya watu wa chini.

Mimi nawaamboa watu sana hawanielewi..
Njaa vs corona bora corona kuna chance ya kusurvive lakini ukipigwa na njaa bila msosi mortality ni 100%
 
Lockdown hatuhitaji.. kinacho hitajika ni kufunga mipaka, wananchi wapewe mask, lab za kupimia walau kila mkoa, mikoa iliyo adhiriwa ijitenge

Sent using Jamii Forums mobile app
Sure.. kitu cha kwanza wangelimit movement ya kutoka na kuingia dar.. yatoke magari ya mizigo na yanayobeba vitu muhimu tu.
 
Back
Top Bottom