maoni ya DR kitila mkumbo juu ya kura ya wazi/siri na uchaguzi wa mwenyekiti wa bunge la katiba

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,813
[h=5]Kitila Mkumbo
[/h]Haya mambo mimi ndio yananishinda. Nimeshasema hili jambo la Katiba ni la jamii. Ni la kitaifa. Ni kwamba hatuwezi kwenda wote Dodoma kuiandika hiyo katiba na ndio maana inabidi waende wenzetu wachache. Ili tujue kwamba wanafanya kazi yetu hakuna siri mle. Kama mtu anapenda sana mambo ya siri pale sio mahala pake. Aombe kazi serikalini huko ndiko kila kitu ni siri.

Sasa hii habari kwamba waandishi wa habari hawaruhusiwi kwenye Kamati inatoka wapi? Yaani tusubiri mtuambieni tu mlichoamua tusijue mliamuaje? Muhimu sana katika jambo hili ni mchakato, sio hitimisho. Tunahitaji tujue kila hatua. Sasa mie nashangaa kabisa. Namshukuru Mwalimu Ulouch, Halima Mdee na wengine kwa jinsi walivyojenga hoja vizuri kwa sababu kidogo Simbachawene awashawishi wajumbe kukubaliana na hoja ya Kamati ya Kanuni kuzuia waandishi. Hawa jamaa wanabishana muda mrefu kwa mambo ambayo ni common sense kabisa sijui wakifika kwenye mambo substantive itakuwaje. Na mimi nashangaa ilikuwaje Kamati ya Kanuni ikapendekeza jambo la ajabu lile la kuzuia waandishi kuingia katika Kamati. Na ukimsikiliza Simbachawane ni kama vile wanaona waandishi ni wajinga. Haikubaliki.

Jambo lingine ni kuhusu huu mteremko aliyoupata Samwel Sitta. Bila shaka nami namuunga mkono Samwel Sitta kwa sababu angalau mara chache chache huwa anauvua uCCM. Lakini kinachoogopesha ni kwamba huyu mtu alishatoa msimamo wake waziwazi kabisa kwamba yeye hakubaliani na serikali tatu na anataka serikali mbili ziendelee. Halafu yeye ni sehemu ya cabinet ambayo nayo msimamo wake unajulikana. Sasa kuwa na mwenyekiti ambaye anajulikana msimamo wake katika mambo magumu na ya msingi kama muundo wa muungano ni hatari sana. Anaweza akafika mahala akatengeneza mazingira ili msimamo wake uwe ndiwe. Kinachonitisha zaidi ni kwamba amapendekezwa na caucus ya CCM. Hii maana yake ni kwamba hayupo huru. Huwezi kupendekezwa na caucus ya CCM bila maelekezo maalumu. Yaani hadi CCM wampendekeze tutakuwa very naive kudhani kwamba hakuna kitu au namna nyuma ya pazia. Ndio kusema CCM wanaendelea kuwa na total control of this bunge, which is a pity. Ningeelewa na kumkubali zaidi kama angegombea kama yeye bila kupendekezwa na chama chake. Angeweza angalau kuwa huru. Kwa sasa hayupo na hatokuwa.

Kilichonisikitisha zaidi baada ya yote haya kutokea ni kwamba ni kama vile tupo katika nchi ya mfumo wa chama kimoja. Tunaenda kwenye uchaguzi na mgombea mmoja aliyependekezwa na chama kimoja. Tena viongozi wa upinzani wanamshabikia na kumchekea kabisa mtu ambaye amependekekzwa na chama tawala, mshindani wao katika kila jambo la kisiasa. Wanachotuambia akina Lipumba na Lissu ni kwamba inapokuja kwenye mambo makubwa kama uongozi katika taasisi serious kama Bunge la Katiba ni CCM pekee wanaoweza kutoa kiongozi. Yaani upinzani wameridhika kabisa na uongozi wa Sitta ambaye ndiye aliyemnyanyasa Dk Slaa kwa kukataa nyaraka zake akisema ni feki kabisa na hazifai hata kuingia katika ukumbi wa bunge. Halafu baadaye hizo nyaraka alizomnyanyasa nazo Dk Slaa ndiyo hizo zimepeleka watu jela katika kesi ya EPA na zilimpoteza kabisa Gavana wa Benki Kuu? Halafu upinzani una imani naye 100%? Huyu si ndiye aliyemfukuza Zitto bungeni katika mazingira tatanishi kabisa halafu Zitto naye ana imani naye, kweli? Halafu baadaye muanze kuliakulia atakapokuwa anashinikiza mamisimamo yao ikiwemo serikali 2?

Nilifundishwe siku nyingi na mwalimu wangu wa filosofia kwamba katika maisha jifunze kutilia shaka kila kitu, na hiyo ndiyo shaka yangu kuhusu Sitta!! We shouldn't be too comfortable with him. He is CCM by the way and you know birds of the same...! Asubuhini njema.
source; ukurasa wake wa facebook
 
Dokezo zuri Kitila,ulifundishwa kutilia shaka kila jambo,kwenye saga lenu la usaliti wewe Kitila,Zitto na Mwigamba mlipotiliwa shaka kwa umamluki na uhaini kwa na ushahidi ukatolewa na mkaomba kujiuzulu,Mbona hukusema ni sawia kutiliwa shaka na baadala yake mkaanza kutapa tapa na matamko kwa hisani ya CCM,makala kwenye magazeti na hadi Mahakama??!! Ulituhumiwa kupewa posho na Zitto na Zitto alianikwa anahongwa na TISS na CCM na hadi namba ba a/cs zlianikwa na majina pia akiwemo Andrea,hampaswi kutiliwa shaka??!!

Maneno na matendo yako yana mashaka makubwa kuliko mashaka,labda now una jaribu kuijenga image yako baada ya kubomolewa na utatu tata wako na Zitto & Co.!!
 
Nami namuunga mkono Mwl Dr Mkumbo kwa 90%.
Hoja nyingi ni kweli kabisa,vyama vya siasa vya upinzani wanaweza kuwa wamemisi point kumtrust namna hii Sitta.
10% ambayo si Muungi mkono Kitila ni benefit of daught,anaweza asisimame na msimamo wake,akafanya kama Judge Warioba ambaye naye alikuwa muumini wa serikali 2 ila kaleta rasimu ya serikali 3
 
Mbona sijaona suala la kura ya siri au laa?kaandika waandishi wa habari waruhusiwe
 
Mpaka mchakato ulipofikia ni kumuachia Mungu ndiye atakaye amua juu ya udhalimu huu wote kwa sababu kama aliweza kuruhusu maoni ya wananchi yachukulie badi hivyo hivyo Mungu atatia mkono wake tutapa katiba mpya na yente kukidhi matakwa ya wananchi
 
Sijaona muunganiko wa Kichwa cha habari na maelezo,lakini kuna baadhi ya mambo naweza kuungana nae ni hii Imani kuwa wajumbe waliyoijenga kwa mhe Sita!!siamini kuwa Sita ni zaidi ya Hao wajumbe wote waliopo Kwenye hilo bunge,Mara nyingi mtu akipambwa sana mwisho wake ujaa Kiburi na matokeo yake ni kufanya vituko!!!sita asipokaa vizuri kuna hatari kubwa ya kuingia Kwenye anguko!!

kuhusu kuwa tayari alishaonyesha msimamo wake Kwenye Suala la serikali mbili kwangu binafsi sina tatizo nalo sana kwani naamini kuwa licha ya kuwa wengine hawajaonyesha misimamo yao kuhusu muungano,ukweli unabaki pale pale kuwa wote wana upande,tukumbuke kuwa hata sita anamapungufu yake Kama mwanadamu lakini ni bora yeye kuliko baadhi ya waliokuwa wanaonyesha nia ya kugombea toka ccm.

Maelezo kuwa tunarudi Kwenye mfumo wa chama kimoja kwa kuruhusu mgombea mmoja,mhe anatakiwa aelewe kuwa mchakato huu ulishahodhiwa na ccm toka mwanzo,kitendo cha kugeuza wabunge wa bunge la jamhuri na wajumbe wa bara za la wawakilishi kuwa wajumbe wa bunge maalum la katiba ulikuwa ni upuuzi wa makusudi ili kutawala mchakato mazima,hivyo piga ua mwenyekiti lazima atatoka ccm,Suala hapa ni kuangalia nani ni afadhali ndani ya ccm,binafsi Sita ni bora kuliko hao wengine waliokuwa na nia ya kugombea.
 
Hivi anategemea kuna mgombea gani wa CHADEMA anaweza akashinda kwenye nafasi yoyote pale!!! CCM wako tayari kuchagua jiwe dhidi ya mgombea yoyote wa CHADEMA...mm nadhani n wakati mwingine ukampa shetan mtoto wako akulele... Na hapa sasa ni kuangalia yupi n shetani bora miongoni mwa maccm. Lakin kama dr. Mkumbo hawajaridhika si kuna mwasisi wa chama chao cha ACT mule ndg ZZK achukue fomu agombee,, si alikuwa a nataka uenyekiti CHADEMA,,,!
 
Mkuu, kwani kuna mahala Kitila ameitaja chadema? Yeye ametaja upinzani kwa ujumla na anawalaumu akina Lipumba na Lissu kwa kumuunga mkono Sitta
 
Kitila Mkumbo

Haya mambo mimi ndio yananishinda. Nimeshasema hili jambo la Katiba ni la jamii. Ni la kitaifa. Ni kwamba hatuwezi kwenda wote Dodoma kuiandika hiyo katiba na ndio maana inabidi waende wenzetu wachache. Ili tujue kwamba wanafanya kazi yetu hakuna siri mle. Kama mtu anapenda sana mambo ya siri pale sio mahala pake. Aombe kazi serikalini huko ndiko kila kitu ni siri.

Sasa hii habari kwamba waandishi wa habari hawaruhusiwi kwenye Kamati inatoka wapi? Yaani tusubiri mtuambieni tu mlichoamua tusijue mliamuaje? Muhimu sana katika jambo hili ni mchakato, sio hitimisho. Tunahitaji tujue kila hatua. Sasa mie nashangaa kabisa. Namshukuru Mwalimu Ulouch, Halima Mdee na wengine kwa jinsi walivyojenga hoja vizuri kwa sababu kidogo Simbachawene awashawishi wajumbe kukubaliana na hoja ya Kamati ya Kanuni kuzuia waandishi. Hawa jamaa wanabishana muda mrefu kwa mambo ambayo ni common sense kabisa sijui wakifika kwenye mambo substantive itakuwaje. Na mimi nashangaa ilikuwaje Kamati ya Kanuni ikapendekeza jambo la ajabu lile la kuzuia waandishi kuingia katika Kamati. Na ukimsikiliza Simbachawane ni kama vile wanaona waandishi ni wajinga. Haikubaliki.

Jambo lingine ni kuhusu huu mteremko aliyoupata Samwel Sitta. Bila shaka nami namuunga mkono Samwel Sitta kwa sababu angalau mara chache chache huwa anauvua uCCM. Lakini kinachoogopesha ni kwamba huyu mtu alishatoa msimamo wake waziwazi kabisa kwamba yeye hakubaliani na serikali tatu na anataka serikali mbili ziendelee. Halafu yeye ni sehemu ya cabinet ambayo nayo msimamo wake unajulikana. Sasa kuwa na mwenyekiti ambaye anajulikana msimamo wake katika mambo magumu na ya msingi kama muundo wa muungano ni hatari sana. Anaweza akafika mahala akatengeneza mazingira ili msimamo wake uwe ndiwe. Kinachonitisha zaidi ni kwamba amapendekezwa na caucus ya CCM. Hii maana yake ni kwamba hayupo huru. Huwezi kupendekezwa na caucus ya CCM bila maelekezo maalumu. Yaani hadi CCM wampendekeze tutakuwa very naive kudhani kwamba hakuna kitu au namna nyuma ya pazia. Ndio kusema CCM wanaendelea kuwa na total control of this bunge, which is a pity. Ningeelewa na kumkubali zaidi kama angegombea kama yeye bila kupendekezwa na chama chake. Angeweza angalau kuwa huru. Kwa sasa hayupo na hatokuwa.

Kilichonisikitisha zaidi baada ya yote haya kutokea ni kwamba ni kama vile tupo katika nchi ya mfumo wa chama kimoja. Tunaenda kwenye uchaguzi na mgombea mmoja aliyependekezwa na chama kimoja. Tena viongozi wa upinzani wanamshabikia na kumchekea kabisa mtu ambaye amependekekzwa na chama tawala, mshindani wao katika kila jambo la kisiasa. Wanachotuambia akina Lipumba na Lissu ni kwamba inapokuja kwenye mambo makubwa kama uongozi katika taasisi serious kama Bunge la Katiba ni CCM pekee wanaoweza kutoa kiongozi. Yaani upinzani wameridhika kabisa na uongozi wa Sitta ambaye ndiye aliyemnyanyasa Dk Slaa kwa kukataa nyaraka zake akisema ni feki kabisa na hazifai hata kuingia katika ukumbi wa bunge. Halafu baadaye hizo nyaraka alizomnyanyasa nazo Dk Slaa ndiyo hizo zimepeleka watu jela katika kesi ya EPA na zilimpoteza kabisa Gavana wa Benki Kuu? Halafu upinzani una imani naye 100%? Huyu si ndiye aliyemfukuza Zitto bungeni katika mazingira tatanishi kabisa halafu Zitto naye ana imani naye, kweli? Halafu baadaye muanze kuliakulia atakapokuwa anashinikiza mamisimamo yao ikiwemo serikali 2?

Nilifundishwe siku nyingi na mwalimu wangu wa filosofia kwamba katika maisha jifunze kutilia shaka kila kitu, na hiyo ndiyo shaka yangu kuhusu Sitta!! We shouldn't be too comfortable with him. He is CCM by the way and you know birds of the same...! Asubuhini njema.
source; ukurasa wake wa facebook

Mkuu
utaifakwanza nafikiri hii nyaraka umeiiba katika ofisi ya ZZK kule fb!!?
 
Nami namuunga mkono Mwl Dr Mkumbo kwa 90%.
Hoja nyingi ni kweli kabisa,vyama vya siasa vya upinzani wanaweza kuwa wamemisi point kumtrust namna hii Sitta.
10% ambayo si Muungi mkono Kitila ni benefit of daught,anaweza asisimame na msimamo wake,akafanya kama Judge Warioba ambaye naye alikuwa muumini wa serikali 2 ila kaleta rasimu ya serikali 3
MA-CCM ni zaidi ya 70% ulidhani mpinzani gani angepigiwa kura na maccm? Au unaunga mkono tu bila kutilia shaka uwezo wa kuchambua mambo wa kitila.
 
Sishangai Dr. kuwa na mawazo kama ya watu walioko kariakoo, issue ya 6 kuwa na upunzi wa kuwa muundo wa serikari 2 au 3 hauwezi kukwepeka. Si italetwa wa watanzania tupige kura? wengi wape. Hivi mnaweza kuafikiana vipi kuwa atakaye kuwa mwenyekiti wa Bunge awe na itikadi ya serikali 3 sio issue
 
Dr Kitila Mkumbo ameathirika kisaikolojia, Samwel sita anakubalika kwa uwezo wake wa kufanya kazi na pia kwa misimamo yake, hapa ushabiki tunaweka pembeni, penye ukweli tuseme kweli, sio kwa sababu sisi ni wapinzani, basi tupinge hata kila kitu hata vinavyoonekana kuwa ni sahihi, sisi tulipinga vikali kuhusu Chenge, sauti zimesikika Chenge wamemtoa, hatusemi ni mzuri asilimia mia moja, anaweza fanya tofauti, lakini hatutarajii hilo, na hii haiwezi kuwa sababu ya kumkataa, Kitila akumbuke kuwa, mle ndani wajumbe wengi ni ccm, hivyo upinzani hata tusimamishe mgombea hawezi pita, Kitila kasahau ccm walivyombeba makinda na kumuacha Mabele Marando, ukiachana na hilo la njama za ccm, Samwel Sita ni mzuri anauwezo wa kuendesha bunge, kama yeye Kitila anaona kila kitu ni kubishania au kupinga, huo ni mtazamo wake, lakini upinzani hauko hivyo.
 
[h=5]Kitila Mkumbo
[/h]Haya mambo mimi ndio yananishinda. Nimeshasema hili jambo la Katiba ni la jamii. Ni la kitaifa. Ni kwamba hatuwezi kwenda wote Dodoma kuiandika hiyo katiba na ndio maana inabidi waende wenzetu wachache. Ili tujue kwamba wanafanya kazi yetu hakuna siri mle. Kama mtu anapenda sana mambo ya siri pale sio mahala pake. Aombe kazi serikalini huko ndiko kila kitu ni siri.

Sasa hii habari kwamba waandishi wa habari hawaruhusiwi kwenye Kamati inatoka wapi? Yaani tusubiri mtuambieni tu mlichoamua tusijue mliamuaje? Muhimu sana katika jambo hili ni mchakato, sio hitimisho. Tunahitaji tujue kila hatua. Sasa mie nashangaa kabisa. Namshukuru Mwalimu Ulouch, Halima Mdee na wengine kwa jinsi walivyojenga hoja vizuri kwa sababu kidogo Simbachawene awashawishi wajumbe kukubaliana na hoja ya Kamati ya Kanuni kuzuia waandishi. Hawa jamaa wanabishana muda mrefu kwa mambo ambayo ni common sense kabisa sijui wakifika kwenye mambo substantive itakuwaje. Na mimi nashangaa ilikuwaje Kamati ya Kanuni ikapendekeza jambo la ajabu lile la kuzuia waandishi kuingia katika Kamati. Na ukimsikiliza Simbachawane ni kama vile wanaona waandishi ni wajinga. Haikubaliki.

Jambo lingine ni kuhusu huu mteremko aliyoupata Samwel Sitta. Bila shaka nami namuunga mkono Samwel Sitta kwa sababu angalau mara chache chache huwa anauvua uCCM. Lakini kinachoogopesha ni kwamba huyu mtu alishatoa msimamo wake waziwazi kabisa kwamba yeye hakubaliani na serikali tatu na anataka serikali mbili ziendelee. Halafu yeye ni sehemu ya cabinet ambayo nayo msimamo wake unajulikana. Sasa kuwa na mwenyekiti ambaye anajulikana msimamo wake katika mambo magumu na ya msingi kama muundo wa muungano ni hatari sana. Anaweza akafika mahala akatengeneza mazingira ili msimamo wake uwe ndiwe. Kinachonitisha zaidi ni kwamba amapendekezwa na caucus ya CCM. Hii maana yake ni kwamba hayupo huru. Huwezi kupendekezwa na caucus ya CCM bila maelekezo maalumu. Yaani hadi CCM wampendekeze tutakuwa very naive kudhani kwamba hakuna kitu au namna nyuma ya pazia. Ndio kusema CCM wanaendelea kuwa na total control of this bunge, which is a pity. Ningeelewa na kumkubali zaidi kama angegombea kama yeye bila kupendekezwa na chama chake. Angeweza angalau kuwa huru. Kwa sasa hayupo na hatokuwa.

Kilichonisikitisha zaidi baada ya yote haya kutokea ni kwamba ni kama vile tupo katika nchi ya mfumo wa chama kimoja. Tunaenda kwenye uchaguzi na mgombea mmoja aliyependekezwa na chama kimoja. Tena viongozi wa upinzani wanamshabikia na kumchekea kabisa mtu ambaye amependekekzwa na chama tawala, mshindani wao katika kila jambo la kisiasa. Wanachotuambia akina Lipumba na Lissu ni kwamba inapokuja kwenye mambo makubwa kama uongozi katika taasisi serious kama Bunge la Katiba ni CCM pekee wanaoweza kutoa kiongozi. Yaani upinzani wameridhika kabisa na uongozi wa Sitta ambaye ndiye aliyemnyanyasa Dk Slaa kwa kukataa nyaraka zake akisema ni feki kabisa na hazifai hata kuingia katika ukumbi wa bunge. Halafu baadaye hizo nyaraka alizomnyanyasa nazo Dk Slaa ndiyo hizo zimepeleka watu jela katika kesi ya EPA na zilimpoteza kabisa Gavana wa Benki Kuu? Halafu upinzani una imani naye 100%? Huyu si ndiye aliyemfukuza Zitto bungeni katika mazingira tatanishi kabisa halafu Zitto naye ana imani naye, kweli? Halafu baadaye muanze kuliakulia atakapokuwa anashinikiza mamisimamo yao ikiwemo serikali 2?

Nilifundishwe siku nyingi na mwalimu wangu wa filosofia kwamba katika maisha jifunze kutilia shaka kila kitu, na hiyo ndiyo shaka yangu kuhusu Sitta!! We shouldn't be too comfortable with him. He is CCM by the way and you know birds of the same...! Asubuhini njema.
source; ukurasa wake wa facebook

Kura ya siri ni kujaza kila mjumbe anapendelea kitu gani bila kutamka. Wakati wa kupiga kura, zoezi linafanyika kila mtu akiona, kuhesabu kura kila mmoja akiona.
 
Back
Top Bottom