utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,813
[h=5]Kitila Mkumbo
[/h]Haya mambo mimi ndio yananishinda. Nimeshasema hili jambo la Katiba ni la jamii. Ni la kitaifa. Ni kwamba hatuwezi kwenda wote Dodoma kuiandika hiyo katiba na ndio maana inabidi waende wenzetu wachache. Ili tujue kwamba wanafanya kazi yetu hakuna siri mle. Kama mtu anapenda sana mambo ya siri pale sio mahala pake. Aombe kazi serikalini huko ndiko kila kitu ni siri.
Sasa hii habari kwamba waandishi wa habari hawaruhusiwi kwenye Kamati inatoka wapi? Yaani tusubiri mtuambieni tu mlichoamua tusijue mliamuaje? Muhimu sana katika jambo hili ni mchakato, sio hitimisho. Tunahitaji tujue kila hatua. Sasa mie nashangaa kabisa. Namshukuru Mwalimu Ulouch, Halima Mdee na wengine kwa jinsi walivyojenga hoja vizuri kwa sababu kidogo Simbachawene awashawishi wajumbe kukubaliana na hoja ya Kamati ya Kanuni kuzuia waandishi. Hawa jamaa wanabishana muda mrefu kwa mambo ambayo ni common sense kabisa sijui wakifika kwenye mambo substantive itakuwaje. Na mimi nashangaa ilikuwaje Kamati ya Kanuni ikapendekeza jambo la ajabu lile la kuzuia waandishi kuingia katika Kamati. Na ukimsikiliza Simbachawane ni kama vile wanaona waandishi ni wajinga. Haikubaliki.
Jambo lingine ni kuhusu huu mteremko aliyoupata Samwel Sitta. Bila shaka nami namuunga mkono Samwel Sitta kwa sababu angalau mara chache chache huwa anauvua uCCM. Lakini kinachoogopesha ni kwamba huyu mtu alishatoa msimamo wake waziwazi kabisa kwamba yeye hakubaliani na serikali tatu na anataka serikali mbili ziendelee. Halafu yeye ni sehemu ya cabinet ambayo nayo msimamo wake unajulikana. Sasa kuwa na mwenyekiti ambaye anajulikana msimamo wake katika mambo magumu na ya msingi kama muundo wa muungano ni hatari sana. Anaweza akafika mahala akatengeneza mazingira ili msimamo wake uwe ndiwe. Kinachonitisha zaidi ni kwamba amapendekezwa na caucus ya CCM. Hii maana yake ni kwamba hayupo huru. Huwezi kupendekezwa na caucus ya CCM bila maelekezo maalumu. Yaani hadi CCM wampendekeze tutakuwa very naive kudhani kwamba hakuna kitu au namna nyuma ya pazia. Ndio kusema CCM wanaendelea kuwa na total control of this bunge, which is a pity. Ningeelewa na kumkubali zaidi kama angegombea kama yeye bila kupendekezwa na chama chake. Angeweza angalau kuwa huru. Kwa sasa hayupo na hatokuwa.
Kilichonisikitisha zaidi baada ya yote haya kutokea ni kwamba ni kama vile tupo katika nchi ya mfumo wa chama kimoja. Tunaenda kwenye uchaguzi na mgombea mmoja aliyependekezwa na chama kimoja. Tena viongozi wa upinzani wanamshabikia na kumchekea kabisa mtu ambaye amependekekzwa na chama tawala, mshindani wao katika kila jambo la kisiasa. Wanachotuambia akina Lipumba na Lissu ni kwamba inapokuja kwenye mambo makubwa kama uongozi katika taasisi serious kama Bunge la Katiba ni CCM pekee wanaoweza kutoa kiongozi. Yaani upinzani wameridhika kabisa na uongozi wa Sitta ambaye ndiye aliyemnyanyasa Dk Slaa kwa kukataa nyaraka zake akisema ni feki kabisa na hazifai hata kuingia katika ukumbi wa bunge. Halafu baadaye hizo nyaraka alizomnyanyasa nazo Dk Slaa ndiyo hizo zimepeleka watu jela katika kesi ya EPA na zilimpoteza kabisa Gavana wa Benki Kuu? Halafu upinzani una imani naye 100%? Huyu si ndiye aliyemfukuza Zitto bungeni katika mazingira tatanishi kabisa halafu Zitto naye ana imani naye, kweli? Halafu baadaye muanze kuliakulia atakapokuwa anashinikiza mamisimamo yao ikiwemo serikali 2?
Nilifundishwe siku nyingi na mwalimu wangu wa filosofia kwamba katika maisha jifunze kutilia shaka kila kitu, na hiyo ndiyo shaka yangu kuhusu Sitta!! We shouldn't be too comfortable with him. He is CCM by the way and you know birds of the same...! Asubuhini njema.
source; ukurasa wake wa facebook