Maoni ya Katiba Mpya: Kama madaraka yanatokana na wananchi, kwanini Rais Samia aseme kuwa mapendekezo ya Kikosi Kazi siyo amri kwa Serikali?

Tunajua kuwa serikali hii ya CCM hawapendi kabisa kuibadilisha Katiba hii, kwa kuwa wao ndiyo wanufaika kwa kiasi kikubwa na Katiba hii ya Sasa tuliyonayo.
Watawala wa ccm wanaona wao wana hati miliki ya Nchi hii!
Bila wananchi 'kuja juu' haya manyanyaso kwa vyama vingine hayatakoma!
Tufike mahali tuiambie ccm hapana na inatosha!
 
Mada Bora kabisa kwa Wenye akili. Siku hizi naona ugonjwa wa viongozi wa serikali kutoheshimu madaraka ya Wananchi umeenea Hadi ngazi za Kata.
Bila bila
Hivi huyu Rais wetu anadhani kuwa atayipitisha yale tu anayoyapenda yeye?

Cha ajabu zaidi hao kina Profesa Mkandala, kawaahidi "kuwazawadia" handshake!

Hebu tujiulize hiyo handshake inatokana na nini, wakati hao akina Profesa Mkandala walikuwa wanalipwa posho nono, kipindi chote walichokuwa wakikuasanya hayo maoni?

Hiyo handshake, naichukulia kama aina fulani ya Rushwa🥺
 
Unaunda kikosi kazi cha mchongo kisha kinakuambia kuwa katiba mpya ni lazima🐒🐒🐒
Your browser is not able to display this video.
 
Mara nyingi tunashindwa kutenganisha umma na serikali na vyama. Umma ndo unatawala hawa watu yaani serikali na vyama. Tunafikia wakati chama kikikiwa madarakani basi chenyewe ndo mungu mtu na kila kitu tunashindwa kutambua kuwa kuna nchi za wenzetu watu wanatawala week 3 tu wanang'atuka na chama kinakuwa nje ya utawala kwa miaka zaidi ya 60 na kinakuja kutawala kama Italy. Tumeamua kuiga demokrasi ya wenzetu basi tuifuate. Kama mnataka tuwe kama nchi zinazotuzunguka usiihusishe Kenya basi tukae kimya na kusema ndiyo bwana ndiyo bwana.
 
Je unaulizia ile Government of the people by the people for the people ?? Bado tunaenda mdogo mdogo sana lakini tutafika !!
 
Mkuu Mystery nakuelewa ila bado nabaki palepale aliye pale juu anaweza kuja na nia thabiti kutaka kuleta mabadiriko ya kikatiba ila akiwa pale anakutana na wenye nguvu kuliko yeye hao ndiyo wanaompa direction ya nini asimamie na nini aache.

Hivi unadhani legendary asingegusa issues za watu na kuzuia madini wangemuondoa?.
 
Nnje ya Tume ya Warioba mavikosi mengine ni Kanjanja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…