PostGE2025 Maoni ya Mwananchi akimjibu Dkt Rioba, tunatokaje hapa kama taifa? Haya yafanyike

PostGE2025 Maoni ya Mwananchi akimjibu Dkt Rioba, tunatokaje hapa kama taifa? Haya yafanyike

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
1. Achia watu waliotekwa.

2. Achia watu waliofunguliwa kesi za kijinga.

3. Weka katiba mpya yenye matakwa ya sasa.

4. Acha kulilia mali kuliko uhai wa watu.

5. Ongea lugha ya kuridhiana sio lugha ya kutishiana ubabe na kujiona kuwa wewe ni wewe.

6. Ruhusu uhuru wa vyombo vya habari. Nashangaa unasema eti mlishindwa kutangaza yaliyotokea kwa sababu ya vitisho vya kuchoma vituo. Mke akikutishia kukupiga unagoma kula na kuleta matumizi nyumbani? Utahukumiwa kwa wajibu wako sio kwa nini kilikuzuia kutimiza wajibu. Ni hoja mfu.

Soma Dkt. Rioba wa TBC: Hatukuripoti matukio ya Oktoba 29, wachochezi walikuwa wakihamasisha vijana kuja kuchoma vituo vya Shirika na hata kutuua sisi

7. Ruhusu uhuru wa kuabudu. Acha watu wahubiri neno sio kuwawekea remoti.

8. Mihimili iwe na nguvu. Acha kujaza uchawa uchawa sio.

9. Acha ufisadi. Yaani watoto wa viongozi ndo wanauwezo wa kuwa viongozi na kupata kazi nzuri. Watoto wa maskini wao ni kukosa elimu, HESLB na ajira ni interview interview ambazo hazina weledi wala vigezo. Vigezo ni una nini.

Dr. Kemea maovu yakiachwa mambo yatakuwa mazuri
 
wanajifanya wanauliza maswali,
lkn ukweli wanaujus, cha kufanya wanakijua ila hawataki kwasababu wanazozijua wao
 
Back
Top Bottom