Mkuu pole Sana wakili. Nafikiri hapa umeropoka na umeamua kuonyesha ni kwa jinsi gani umevamia hii taaluma.
Kazi ya wakili ni nyingi na moja wapo ipo katika kesi ya mohamed katindi v Republic inayosema kuwa "an advocate is an officer of the court, his main function is to make a research, analysis, reading journals, books, in order to help the court to reach into the justice"
Sasa niulize kwa Hilo, je wakili msomi, umefanya research na analysis kuhusu ishu nzima ya wimbo wa diamond? Au tu kwa sababu ya media na wewe unafikia maamuzi hayo?
Pia kuna kitu kinaitwa "corrupt of public moral" je ni kweli diamond kafanya hivyo?
Nafikiri kuwa basata wako sahihi na pia wameamua sio kuufungia wimbo Bali waweze kuufanyia editing ili kuondoa maneno ambayo yanaonekan ni matusi na wakiridhika, unaruhusiwa kupigwa kwani maneno yaliyotumika ni matusi.
Je wakili msomi, kutukana kwa njia ya wimbo ni kosa au sio kosa? Sasa kuambiwa watoe maneno ya matusi basata wanawez laumiwa? Au wamshtaki kwa kutoa lugha za matusi kwa njia ya nyimbo unafikir diamond atabaki Bila kufungwa?
Lay man wataelewaje kuhusu ishu kama hizi za kisheria?
Nadhani wakili inaonekana huna experience katika kazi yako hvyo comments zako uwe kidogo unafanya research na si kwa mhemko