Maoni ya wadau wa JamiiForums juu ya kusitishwa kwa Bima ya TOTO AFYA KADI

Kwa ubinafsi wao wameona bima hiyo ibaki kwa watoto wa wafanyakazi wa serikalini tu, watoto wa wengine wameona walikuwa wanaifaidi
 
Km nilivyoelewa mtoto unaweza kumsajili km tegemezi naona imekaa vzr maana ilitolewa hii
 
Jamani sasa mbona kama ni mateso makubwa kwa wasiokuwa na uwezo??
 
Kabla ya kuja na ushauri wangekuja kwa wadau, wanachama nini kifanyike. Kwani kinachowasibu wananchi au wateja wenu baada ya kuwazuia huduma toto afya hamkijui? Vaeni viatu vya wengine.
 
Ni vitu vilivyowahitaji fikra nyepesi tu. Dunia inakabiliana kupunguza vifo vya watoto wao Wana entertain kuondoa tiba ya mtoto, Tena anayelindwa na sera ya matibabu bure. Hivi waliikaa kikao na kufikiri? Au sababu wao Wana uhakika na matibabu muogopeni Mungu. Mtoto ni malaika, alikuja duniani kwa mapenzi ya watu wazima si kwa yeye kupenda, naungana nawe mtoto apewe haki yake. Kwanza Serikali ilipaswa imtibu huyo mtoto kutoka day 1 Hadi 5 yrs, wananchi wameisaidia kwa kujilipia bima
 
Hii bima ilifanya watu wengi waweze kusaidia watoto wasiokuwa na uwezo na ambao hawapo vituoni.
Serikali inatengeneza mechanism ya watu kuchiti na wenye vituo kunufaika.
Sio hivyo, inaangamiza watoto ambapo duniani kote watoto wanalelewa ipasavyo.
 
mimi nimo katika wale wanaosubiria siku 90 za kupewa kadi yangu ya TOTO

Kwa ajili ya mwanangu

hivi sasa zimesalia siku 25 tu kupewa.
 
mimi nimo katika wale wanaosubiria siku 90 za kupewa kadi yangu ya TOTO

Kwa ajili ya mwanangu

hivi sasa zimesalia siku 25 tu kupewa.
kwa mujibu wa nhif, mtoto wako atakuwa covered mpaka bima yake itapoisha ndiyo ukitaka kumkatia tena utaratibu mpya utatumika.
 
HIYO INAYOKUWA ETI BIMA YA AFYA KWA WOTE...NI KICHAKA TU CHA KUPATA MAPATO KWA URAHISI...KODI YA KICHWA KWA MLANGO MWINGINE...

I DONT THINK THIS COUNTRY HAS A LEADER... EVERYTHING IS AUTOMATIVE ROUGHLY DRIVEN.

ALAFU KUNA MTU YUPO MAHALI FULANI...HAJATOSHEKA BILA USO WA HAAYA ANAPIGIA HESABU 2025-2030...No mara waa...
 
Sina uhakika kama huu ndio uwezo wa kufikiri uwa viongozi wetu ulipofikia,halafu siku Rais akitumbua mtu utasikia kuna udini,mara ohh kuna upendeleo...
 
Watanzania na kujikusanya mitandaoni kulalamika kila siku sijui itaishia wapi!
Serikali kila siku itaamka na kufanya itakacho kwasababu vitu vidogo mnasahau ya msingi.
Hili ni jambo la ngapi la msingi kulalamikiwa mwaka huu?
 
Wanalazimisha wazazi kujiunga na mfuko kwa mgongo wa watoto.

Hapa ni kama kubet tu maana sio kila anayemlipia mtoto atamudu gharama za bima yake inayombeba mtoto.

Wangeongeza bei ya bima na sio kuifuta kabisa.
 
Kwa kweli. Kwanza walianza na kuondoa utaratibu va zile fomu za bima za njano za kuchukulia dawa nje ya hospitali kwa zile dawa ambazo hospitali hakuna, utaratibu huo unatutesa hadi sasa maana inabidi utoe pesa cash ukanunue. Wameona haitoshi wamekuja na wanayodai maboresho ya mfuko wa bima, haya siyo maboresho bali ni ukatili kwa mtoto kama ukatili mwingine tu.
 
Na kuna kipindi walitaka kuwaondoa wazee tegemezi kwenye matibabu ya bima mbona palichimbika ndiyo wakajidai ooh siyo kweli tulikuwa tunafanya maboresho. Naona sasa wamehamia kwa watoto. Huu ni ukatili kwa watoto ni kinyume na sheria ya mtoto kila mtoto ana haki ya kupata matibabu ili aisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…