Maoni ya wadau wa JamiiForums juu ya kusitishwa kwa Bima ya TOTO AFYA KADI

Maoni ya wadau wa JamiiForums juu ya kusitishwa kwa Bima ya TOTO AFYA KADI

Kama 50,400 ilikuwa ni bei rahisi basi wangeongeza gharama kuliko kuifuta kabisa.

Serikali imeshindwa kuangalia jambo la msingi na kuhakikisha wananchi Wanapata uhakika wa matibabu.
Afya ndio Kila kitu.

Ni lini viongozi wetu watakaa na kutunga Sheria na maamuzi ya kuwanufaisha wananchi? Pamoja na makato ya miamala na luku Kila mwezi ila Bado waneshindwa kuhudumia bima za watoto.

Hao wanasiasa wa majukwaani wanaongea mambo Gani? Hivi ndio vitu vya kuongelea

Mwisho, Serikali msije sema kuwa kabla ya kufuta bima kwa watoto mliomba maoni kwa wananchi wakakubali ufutwe utakuwa ni uongo kama mlivyosema kwenye tozo.
 
Kuondoa Bima kwa watoto huku wakijinasibu huduma bure kwa under 5 years ni uzushi.
Let's be really, tuwaache watoto. Bora yaongezewe makundi wengine. These are the most vulnerable group.
 
Kwa kweli. Kwanza walianza na kuondoa utaratibu va zile fomu za bima za njano za kuchukulia dawa nje ya hospitali kwa zile dawa ambazo hospitali hakuna...
Ummy hamna kitu pale. Mh Rais aache kupambwa na maneno ampe mtu mwenye uelewa aongoze wizara.
 
Makadirio ya idadi ya watoto chini ya miaka 18 ambao ni asilimia 31 ya watanzania wote

Idadi ya watoto = idadi ya watanzania X 31%

= 60,000,000 X 31%
Idadi. = 18,600,000

Tutoe watoto wa waajiriwa

Makadilio waajiriwa rasmi sekta binafsi na serikali ni 1,000,000.

Kila muajiriwa maximum watoto 4, so hapo ni sawa na watoto milion 4 wapo kwenye bima za wazazi wao waajiriwa.

Kwaiyo kupata idadi ya watoto wasio na wazazi waajiri ni sawa sawa na

= 18,600,000 - 4,000,000
= 14,600,000

Kwaiyo katika watoto 14,600,000 walikatiwa bima ya TOTO AFYA ni 217,000 tu ambayo ni sawa na asilimia 1.4 ya watoto wasio na wazazi waajiriwa.

Kwaiyo kuamishwa kwa mnufaika ambaye ni mtoto kwenda kwenye vifurushi vingine vya bima,

je itasaidia idadi ya watoto wanufaika kuongezaka?

Au ni mpango wamajaribio, ambao unaonesha dhahiri kwenda kugonga mwamba.
 
Na kuna kipindi walitaka kuwaondoa wazee tegemezi kwenye matibabu ya bima mbona palichimbika ndiyo wakajidai ooh siyo kweli tulikuwa tunafanya maboresho. Naona sasa wamehamia kwa watoto. Huu ni ukatili kwa watoto ni kinyume na sheria ya mtoto kila mtoto ana haki ya kupata matibabu ili aisha.
Wizara imeingiliwa na makatili.
Wanaona kama vile bima ni anasa
 
Yan kati ya watoto million 30 waliosajiliwa na bima ya afya n laki mbili lakin serikali imeshindwa kuwahudumia....hii serikali haiwezi kuwa serious...wakat kuna viongozi wanaenda kutibiwa nje gharama inawezafika ata million 100+..kwa mtu mmoja.
Umasikini mpaya sana.
 
Nafikiri kwa mapana kama hawa viongozi wa hii bima ya taifa walikaa chini kufikiri, walikuja na mpango mzuri kabisa wa bima kwa watoto chini ya miaka 5 ambao umeleta matokeo mazuri kwa wananchi wa hali ya chini.

Leo tena wanakuja na hoja ya kufuta huo mpango na kusema watoto wote wasajiliwe kama wategemezi kwa wazazi wao, swali je ni wangapi wanafanya kazi Serikalini hadi wawasajili watoto wao kama tegemezi mi nafikiri ili walifikirie tena upya warudishe utaratibu wa zamani.
 
Mpango tajwa haujafutwa bali umefanyiwa nabadiliko. Badala ya kulipa 50,400/- watoto watakuwa wanalipiwa 120,000/-.

Hio no taarifa ambayo haijathibitishwa rasmi na NHIF.
 
Professor Janabi angekuwa Waziri wa Afya tens ateuliwe msisumbue mambo yenu ya kugombea ubunge anapewa eneo dogo la Muhimbiri huku maeneo muhimu wakipewa wabahatishaji ...
 
Nafikiri wanalenga Bima ya wote japo nafikiri wangeiweka kwa phase pengine tatu;

1st year, 2nd year and 3rd year

Kimsingi wanachi wanahitaji zaidi Elimu, Elimu, Elimu.... mfano;

1. Bima ya familia itachajiwa kiasi gani kwa mwaka pamoja na watoto wao/wangapi?

2. Watoto wanaosoma wakiandikishwa mashuleni, Bima itakuwa kiasi gani?

3. Kile kigezo cha aliye ajiriwa kuandikisha familia yake pekee kitaendelea kuwepo AU mtu ataruhusiwa kuandikisha pengine mtoto wa dada yake/kaka yake (ili tuwe na Bima inayoendana na mazingira ya Kiafrika na sio vinginevo?).
 
Mpango tajwa haujafutwa bali umefanyiwa nabadiliko. Badala ya kulipa 50,400/- watoto watakuwa wanalipiwa 120,000/-.
Hio no taarifa ambayo haijathibitishwa rasmi na NHIF.
Hakuna bima ya mtoto, mtoto anatakiwa ajumuishwe kwenye familia.

Toto Afya imefutwa sababu wengi waliokuwa wanakatiwa walikuwa wagonjwa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hili swala lina baraka za Ikulu, hivyo kwa sasa tutaongea ila ndio imepitishwa hivyo. Lengo kubwa ni watu wasajiliwe kwa wingi

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kabla ya kufanya jambo lolote inatakiwa wawashirikishe wadua siyo wanakurupuka na kuja na ideas zao kutoka google search.
 
Back
Top Bottom