Kwa kasi ya kuongeza kodi kwenye maeneo yaleyale na kuwajengea wawekezaji kutoka nje mianya ya kutolipa kodi ili wawahonge viongozi wa kitaifa tunasema ndani ya miaka 20 hivi kodi zitafikia 70% ya mapato ya raia na za wageni zitakuwa 5%
Hela hiyo itaishia kuliwa na watendaji serikalini na wakati mwingine kuhamishiwa maeneo mengine ya ulaji na hao wanyonge wanatumika tu kuhalalisha ufisadi serikalini
Hakuna makisio yoyote yaliyofanyika kukadiria wangapi hawatakuwa na uwezo na hivyo wahudumiwe na hiyo mifuko hata kuelewa gharama halisi na matokeo yake sera yake haina tija
Tunarudia sheria ya mafao ya wenza wa viongozi wa kitaifa imeleta ubaguzi kinyume na matakwa ya kikatiba na imetumika kutengua haki za kikatiba walizopewa wenza
Tunasema bunge na serikali yote inakwepa kurekebisha katiba kwenye maeneo ya uteuzi wa tume ya uchaguzi na jinsi inavyofanya kazi lakini inatumia sheria za kawaida kutengua ibara za katiba ambazo hawazitaki
Tunasema hili bunge 95% ya maboresho ya masilahi yamelinufaisha lenyewe na viongozi wa kitaifa kwa hiyo limepoteza sifa ya kuwa bunge la nchi bali sasa tutaliita ni bunge la masilahi ya viongozi
Hili bunge kimya kimya limejiongezea mishahara kutoka milioni 9 kwa mwezi hadi milioni 16 kwa mwezi. Hili ni ongezeko la 75% na wafanyakazi wa kawaida wameachwa kwenye mataa kwa ahadi hewa za masuala yao kushughulikiwa
Ongezeko la gharama za kuwalisha hawa viongozi ni ongezeko la umasikini kwa watu wa kawaida ambao hubebeshwa mizigo ambayo hawastahiki kubeba kupitia kupanda kiholela kwa kodi