Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Tunashindwa kuelewa kodi za wawekezaji ambao wametupora njia kuu za uchumi huwa analipwa nani?
 
Kwanini wananchi wabebeshwe mzigo mkubwa wa kodi na wageni wapete na kutokuwa na mchango wowote wa maana kwenye bajeti ya kila mwaka ya serikali
 
Kwa kasi ya kuongeza kodi kwenye maeneo yaleyale na kuwajengea wawekezaji kutoka nje mianya ya kutolipa kodi ili wawahonge viongozi wa kitaifa tunasema ndani ya miaka 20 hivi kodi zitafikia 70% ya mapato ya raia na za wageni zitakuwa 5%
 
Misingi ya usawa iliyoko kwenye katiba inasiginwa kila siku
 
Kwa mfano kodi za mfuko wa bima za afya kusaidia wasiyojiweza ni ufisadi tu unaruzukiwa
 
Hela hiyo itaishia kuliwa na watendaji serikalini na wakati mwingine kuhamishiwa maeneo mengine ya ulaji na hao wanyonge wanatumika tu kuhalalisha ufisadi serikalini
 
Hakuna makisio yoyote yaliyofanyika kukadiria wangapi hawatakuwa na uwezo na hivyo wahudumiwe na hiyo mifuko hata kuelewa gharama halisi na matokeo yake sera yake haina tija
 
Hakuna makisio ya wanaochangia bima ni wangapi na kwanini wale ambao wana afya hela yao waliyochangia ndiyo itumike kuwagharimia wasiyojiweza
 
Huyu waziri wa afya Ummy ni mzigo hana tija na wala siyo mbunifu sasa sijui kwanini uteuzi wake hautenguliwi
 
Kulea mawaziri mizigo ni moja ya sababu kuu nchi inakazana kutoza kodi na kufifilisha soko la ajira kwa vijana
 
Tunarudia kukumbusha kuna uhusiano wa moja kwa moja wa kuruzuku ufisadi, kasi ya kupanda kwa kodi na ukosefu wa ajira
 
Zaidi ya theluthi mbili ya kodi tunazolipa hutumika kuruzuku ufisadi na wala hazielekezwi kwenye maeneo yaliyokusudiwa
 
Tunarudia sheria ya mafao ya wenza wa viongozi wa kitaifa imeleta ubaguzi kinyume na matakwa ya kikatiba na imetumika kutengua haki za kikatiba walizopewa wenza
 
Tunasema bunge na serikali yote inakwepa kurekebisha katiba kwenye maeneo ya uteuzi wa tume ya uchaguzi na jinsi inavyofanya kazi lakini inatumia sheria za kawaida kutengua ibara za katiba ambazo hawazitaki
 
Tunasema hili bunge 95% ya maboresho ya masilahi yamelinufaisha lenyewe na viongozi wa kitaifa kwa hiyo limepoteza sifa ya kuwa bunge la nchi bali sasa tutaliita ni bunge la masilahi ya viongozi
 
Hili bunge kimya kimya limejiongezea mishahara kutoka milioni 9 kwa mwezi hadi milioni 16 kwa mwezi. Hili ni ongezeko la 75% na wafanyakazi wa kawaida wameachwa kwenye mataa kwa ahadi hewa za masuala yao kushughulikiwa
 
Ongezeko la gharama za kuwalisha hawa viongozi ni ongezeko la umasikini kwa watu wa kawaida ambao hubebeshwa mizigo ambayo hawastahiki kubeba kupitia kupanda kiholela kwa kodi
 
Kwanini naksi ya wachangiaji wa bima ya afya isitumike kubeba gharama za wasiojiweza?
 
Back
Top Bottom