Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Hatujui bandari kavu zitaathiri makazi ya watu kwa kiwango gani
 

View: https://youtu.be/kp7qB49Sc84?si=yWVRo6o5Qpru8lVF

Maoni yetu.

Khoja hapa ni kuwa kwa kupitia TPA, serikali imekuwa ikipata 10% ya mapato yote ya bandari ya Dar sasa kwa kupitia DP WORLD mapato ya serikali yatakuwa 60% ya mapato ya bandari.

Tunaambiwa tija itakuwa babu kubwa.

Kama haya ni kweli mwaka 2025, tutarajie mapato ya serikali yasipungue 42 Trilioni ambayo ni mara 6 ya mapato ya 7 T tunayoyapata kwa sasa.

Ukokotoaji huu umetokana na kugawa 10% tunayoyapata sasa na 60% tutakayoipata. Uwiano huo ni mapato yatapaa kwa mara 6.

Tutarajie trilioni 42 zisipungue 2025 maana hata hizo ni kiduchu kwa ufanisi mdogo wa sasa kwa ahadi za ufanisi tulizopewa hatuna sababu ya kusubiri miaka 10 kama wanavyotuhadaa tusubiri hadi mapato yawe mara mbili.


Ukiona mapato ya serikali yako chini ya Trilioni 42 mwaka 2025 ujue takwimu zote walizotupa leo no UTAPELI.


Lakini mapato ya serikali yakiwa Trilioni 42 au juu ya hapo basi inabidi SSH apewe maua yake.
 
Back
Top Bottom