Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Kwa kutumia takwimu za mapato ya TPA June 2022 Trilioni 7.1 ambacho Serikali hupata kwa mwaka ni 53.79% ya mapato yote kwa mwaka ya TPA ambayo ni takribani 13. 2 Trilioni
Do your math!

7.1/13.2 × 100 = 53.79%

Hiyo 10% wanayodai hupata kutoka TPA ni UONGO!

Wao hupata zaidi ya 54% kwa mwaka ya mapato yote ya TPA.
 
Kwa hiyo serikali hupata wastani wa 54% ya mapato yote ya TPA ambayo hayatofautiani na kodi ya pango ambalo watawakodisha DP WORLD ambayo ni 60% ya mapato yote!


Tofauti ya 6% siyo sababu ya kuikodisha bandari yetu kwa mamluki lakini la kusikitisha ni kwanini uongope ili ufanikishe uovu wako?

Hamjui mwongo baba yake ni shetani kwa sababu shetani alikuwa mwongo tangia mwanzo?
 
Jingine la kuumiza moyo wa kila mtanzania ni ahadi yao ya mapato kuongezeka mara 3 ndani ya miaka 10
 
Kitakachoongezeka siyo mapato ya bandari bali ni viwango vya tozo kutokana na mfumuko wa bei na mapato (inflation) na kuporomoka thamani ya shilingi yetu.

Tutatoa mifano hai
 
Mwaka 1972 nauli ya basi la shirika la umma la TRC ilikuwa Tshs 14.10 kwa mtu mzima na Tshs 7.05 kwa mtoto kutoka Dodoma kwenda Iringa.
 
Miaka 10 baadaye yaani mwaka 1982, nauli ilipaa na kuwa Tshs 100 kwa mtu mzima na Tshs 50 kwa mtoto.

Hivi ni sahihi kwa TRC kujigamba mapato yalipaa kwa vile nauli waliongeza au sifuri zimeongezeka kwenye bajeti yao kutokana na mfumuko wa bei na mapato pamoja na kuporomoka kwa thamani ya shilingi yetu?
 
Watawala hawa wanayo masilahi binafsi kwenye huu uwekezaji wa DP WORLD
 
Wote ambao wanashabikia huu uwekezaji aidha kwa kutofahamu au kwa makusudi mazima wajue fika wameyakana na kuyachukia maisha yao wenyewe na siku zao za kuishi wamezipunguza wenyewe kwa kuyakataa maarifa.


Utetezi wa kutokujua siyo utetezi adhabu yako iko pale pale.
 
Kwa vile, watawala wamejikita zaidi kwenye khoja ya mapato ya serikali kupaa sasa tunawatabiria mapato ya serikali kutokana na bandari ya Dar yatashuka hadi kufikia sifuri.

Bwana atatenda na jina lake lihidimiwe. Hivyo, hata hiyo Trilioni 7.1 mnayoidhihaki leo mtaitafuta kwa tochi ya Nokia na kamwe hamtaiona.

Kuanzia hapo mtajua yuko Mfalme wa wafalme na Mungu wa miungu.

Hamuwezi kumsulubu Mwenyezi Mungu kiasi hiki mkabaki salama.

Kwani nyie ni akina nani?
 
CCM is DOOMED!

Yaani haiendi mahali.

Waendelee kuongopa halafu wasubiri kivuno chake.
 

Attachments

  • IMG-20231023-WA0004.jpg
    IMG-20231023-WA0004.jpg
    62.5 KB · Views: 3
CCM is finito!
 

Attachments

  • PSX_20231023_175913.jpg
    PSX_20231023_175913.jpg
    212.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom