Katika hawa mawaziri watatu Profesa Kitilya Mkumbo ndiye aliyetia fora kwa kukosa upeo, kujitutumua kama ni mjuaji na kukosoa maeneo aliyopaswa kuufyata
Mbunge Salome Makamba aliibua hoja nzito ya kuonyesha taarifa za CAG zinaonyesha maovu yanaongezeka na hivyo kuonyesha watendaji waandamizi wameshindwa kuthibiti hali hiyo
Watendaji wamekuwa magwiji wa kufuata taratibu za kiuhasibu ili kulinda wizi na ubadhirifu wa mali ya umma!
Profesa Kitilya Mkumbo katika harakati zisizo na mashiko akainua mkono na kudai Salome alisema uongo maana yeye aliisoma taarifa yote ya CAG yenye kurasa 800+ hajaona tuhuma zilizoibuliwa na Salome Makamba
Nayo ilikuwa kuutaja ukurasa ambao taarifa ya CAG imeonyesha hati safi kupungua huku zenye utata zikipaa na hivyo kuthibitisha mtazamo ya kuwa profesa Kitilya Mkumbo aidha hajaisoma taarifa ya CAG au hata kama aliisoma hakuielewa
Alipoombwa na spika aipokee taarifa ya Salome Makamba Nape Nnauye aliyekuwa akitetea utendaji wa serikali na kuibeza taarifa ya CAG Nape Nnauye kwa kiburi alikataa kuikubali na hakutaja sababu ya maana kwanini haikubali zaidi ya kuwakumbusha wabunge muda wa utumishi wake bungeni ni wa kitambo hoja ambayo haikuwa na uhusiano na sababu alizotakiwa kutoa kuelezea kinagaubaga kwanini ameikataa taarifa ya Salome
Mwigulu Nchemba alitumia muda mwingi kutamba yeye na Rais walivyoboresha utendaji wa ofisi ya CAG hadi ikaibua yale madudu yaliyoibuliwa lakini hakuwa na mkakati wowote ule wa jinsi atakavyomsaidia Rais kuthibiti wizi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka kama taarifa ya CAG ilivyobainisha.
Mwigulu Nchemba alilitumia jina na cheo cha urais kama kinga ya yeye asiadhibiwe kwa kushindwa kuthibiti hasara kubwa nchi inapata kwa yeye kuendelea kuwa waziri wa fedha mzigo
Tulichojifunza Nape Nnauye, Profesa Kitilya Mkumbo na Mwigulu Nchemba wamepoteza imani ya wabunge na vyema bunge likatoa azimio la kuwapigia kura ya kukosa imani nao
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.