Marekebisho ya sheria za uchaguzi na muundo wa Tume ya uchaguzi zinalenga kuwadhulumu wapigakura haki yao ya kikatiba ya kujichagulia viongozi wao wanaowaamini
Jaji mkuu ndiye mwenyekiti wa kamati ya uteuzi wa makamishina wa Tume ya uchaguzi sasa ikija kesi ya kupinga zoezi zima la uteuzi wa hao makamishina atatoa wapi uhalali wa kuunda jopo la majaji wamchunguze yeye mwenyewe kama hakuhongwa wakati alipokuwa akiyatelekeza majukumu yake.
Atajifunga kengele mwenyewe au atateua jopo analojua litamsafisha.
Swali la msingi kuliko yote ni sahihi kwa majaji kuwa mahakimu kwenye kesi yao yenyewe?
Pia, je ni sahihi kwa wateule wa Rais kuwa wajumbe wa Tume ya uchaguzi kama lengo siyo kuijaza Tume ya uchaguzi na makada wa CCM ili watangaze matokeo ya uchaguzi bila kuhesabu kura?
Ieleweke tuliyoyashuhudia kwa macho yetu wenyewe uchaguzi wa 2020 ndiyo yanatusukuma tuoni kama tunavyooni.
Hatuna imani na wateule wote wa Rais kujihusisha na Tume ya Uchaguzi kwa sababu wanayo masilahi binafsi ya kuhakikisha CCM inaendelea kutawala hata kama wapigakura wameikataa kwenye masanduku ya kura
Si sahihi kwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi kuwa jaji kwani kuhesabu kura tuna kesi ya kuamua? Jaji na kuhesabu kura wapi na wapi?
Sifa ya ujaji ni unafiki mtupu wa kuipa Tume ya uchaguzi sifa ya haki wakati haina bali ni kijiwe na kichinjio dhidi wa wagombea wa vyama vya siasa vya upinzani
Halafu bado tunajigamba tuna Mwanasheria Mkuu mbavu zangu hoi
Tunatamka rasmi uwepo wa majaji kwenye kamati ya uteuzi au mteule yeyote wa Rais kwaajili ya majukumu mengine kama Mwanasheria mkuu kuna haramisha tume ya uchaguzi na inapoteza uhuru wake na kuiita jina tume huru huku Rais mwenye chama cha siasa chenye masilahi mapana ya kuiba kura ndiye anaiunda kupitia wateule wake sisi hatukubali kudanganyika na tambo za kuibatiza tume ya uchaguzi kilemba cha ukoka ya kujigamba ni tume huru wakati ni tume ya mgombea Urais wa CCM
Tatizo kubwa kuliko yote tulilonalo ni ukapa wa uongozi bora na haya marekebisho ya sheria za uchaguzi kamwe hayatatua haya matatizo bali zitayakoleza.
Uwakilishi haramu ndilo chimbuko la umasikini hapa nchini hasa ukiona hata Bashite anaonekana ni jembe la wezi wa kura ujue tumefikia pabaya mno
Malengo ni kuwahadaa watanzania na wapigakura kuna uchaguzi hufanyika lakini kinachoendelea ni kuwachagulia wananchi viongozi wasiwataka na kwa haya marekebisho yasiyo na dhamira ya kuwawezesha wapigakura kuwachagua viongozi wanawaamini tutarajie uwakilishi haramu kutawala na kuwa kichocheo cha wizi, ubadhirifu na rushwa kukithiri
Kamati ya uteuzi tajwa inapaswa iwe na wajumbe walioteuliwa na mikutano mikuu ya vyama vya siasa kwa kazi hiyo tu na wasiwe na nyadhifa zozote serikalini au kwenye vyama vya siasa.
Yaani wawe watu wa kawaida siyo viongozi kwenye ngazi yoyote ile na wasiwe watumishi wa umma
La maana tuliloliona kamati ya uteuzi haina sura ya utaifa ila wale wale wanaotuongezea umasikini ndiyo wanakaza buti kutuchagulia viongozi yaani kuhakikisha business as usual wakati mustakabali wa nchi uko njia panda
Hii jitihada ya marekebisho ya sheria inalenga kulinda mfumo wa kiutawala tuliorithi kutoka kwa mkoloni zaidi ya miaka 60 iliyopita sasa utuambie nchi hii tuna wasomi.
Tunao wenye makabrasha lakini wabunifu hatunao huu ndiyo ukweli wetu
Tunahitimisha kwa kusema marekebisho ya sheria za chaguzi yamegubikwa na hila, unafiki na tunasisitiza yeyote anayeshabikia huu upotolo ajue mbinguni ataziona lakini hatakwenda huko atabaki hapahapa Jahanamu na Lucifer mungu wake maana hii ndiyo mbingu yake na hana nyingine ya kuwapa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.