Uchaguzi 2020 Maoni yangu juu ya mchakato wa mgombea urais CHADEMA

Siku moja tu baada ya Lisu kutumia masaa 4 akiwahutubia watanzania na kuwapa sababu za kwa nini anatangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania, huku nyuma Mbowe akaibuka na igizo la kuvamiwa na watu wasiojulikana, kisha kukanyagwa kanyagwa na kuvunjwa mguu wa kulia bila mtoto wake James aliyekuwa ndani kusikia chochote ,badala yake akasikia Joyce Mkuya aliyekuwa umbali wa kilomita
5!!
Lengo la hili igizo ilikuwa ni kufunika habari ya Lisu kuandikwa na vyombo vya habari.

Kana kwamba haitoshi Mbowe baada tu ya kuruhusiwa kutoka hospitali ,huku akichechemea akatangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania!
Yani watanzania wakiwa na hamu ya kusikia report kutoka kwa Mbowe mwenyewe kwamba alivamiwaje, ilikuwaje ,badala ya kujibu hizo hoja ,yeye akaja na igizo jingine la kwamba kuna wazee wameenda nyumbani kwake kumshawishi awanie urais wa Tanzania!!.

Hivi Lisu unataka ufanyiwe nini ndiyo ujue kwa sasa hauhitajiki Chadema?
Haya maigizo ya mwenyekiti wako wa chama kufunika utangazaji wako nia hayajakuamsha tu?.

Shituka
 
Mpaka sasa CHADEMA ina watia nia watano kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwenye ushindani huu; namuona Tundu Lissu akishindana kwa ukaribu zaidi na Mwenyekiti wa chama ndungu Aikaeli Freeman Mbowe ukiachilia wagombea wengine watatu. Hii ni kwa sababu ya ushwawishi walionao ndani na nje ya chama chao.

Je, mchakato wa mwaka huu wa kumpata mpeperusha bendara ya CHADEMA unaharibiwa kwa Mwenyekiti kutia nia? Hasa ikizingatiwa kwamba wapenzi na wanachama wa CHADEMA walikuwa wameishafanya hitimisho juu ya uteuzi wa ndugu Tundu Lissu? Ambae kwa mtizamo na imani yao ndiye pekee anayeonekana anaweza kumkabili mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)?

La hasha, CHADEMA kama chama kinachojipambanua kuishi na kuienzi Demokrasia; kinapaswa kuwa mfano. Matendo yana kishindo kuliko maneno. Hivyo basi, CHADEMA inataka kuiambia jamii ya wapenda siasa zenye kufuata Demokrasia kwamba, kinaishi kwa matendo yale wanayoyahubiri. Hili ni jambo jema sana kama vyombo vinavyosimamia mchakato wa maamuzi vitatenda kazi yake kwa uwazi, bila upendeleo au msukumo wowote usiokua na dalili za kuienzi Demokrasia ndani ya CHADEMA . Historia itajengeka na heshima itatamalaki kwenye duru za siasa hizo. Vilevile, CHADEMA itakua inasahihisha makosa ya michakato kama hii ya huko nyuma. Kila mpenda Demokrasia ataimba mapambao ya ushindi kwamba DEMOKRASIA imeamua.

Kupata upinzani ndani ya mchakato wa CHADEMA kwa ndugu Tundu Lissu kuna faida nyingi. Mosi, kwa kawaida kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Pili, ushindi bila ushindani mgumu hauna hamasa. Watoto wa mjini wanasema, "atachukulia poa." Tatu, mchakato mgumu ndani ya CHADEMA unamuandaa mshindi vyema kwenda kukabiliana na hatua ya kushindana na CCM akiwa ameiva. Kwa mfano; wanamasumbwi hujiandaa sawa sawa na mpinzani atakayepambana nae. Hivyo basi, mchakato mgumu ndani ya CHADEMA ni maandalizi mazuri ya kumfanya mshindi awe ameiva kupambana na CCM.

Natambua hamu, matamanio na imani waliyonayo wale wanaosema Tundu Lissu apewe kijiti kwa kuwa anatosha. Hata hivyo, njia hii si sahihi sana. Inafanya uchaguzi kukosa hamasa. CCM mara nyingi wamefanya maajabu kwenye michakato yao ya kumsaka mgombea wa kiti cha Urais. Kwa mfano, hakuna aliyetegemea kwamba John Pombe Magufuli angelikua mgombea wa urais kupitia CCM mwaka 2015. Mchakato wao ndani ya chama uliitikisa nchi, macho yote yalihamia Dodoma. Kila mpenzi na mfuatiliaji wa siasa za Tanzania hakupenda kupitwa na tukio lolote. Hii ni nafasi nzuri ya CHADEMA kuboresha pale CCM wanapokosea, hasa pale wanapobaki makundi kinzani baada ya kuisha kwa mchakato wa ndani. Ni fursa kwa CHADEMA kuanzisha safari mpya ya matumaini na siasa zenye kulenga kujisahihisha na kuwa mfano wa kuigwa.

Mwisho, nawatakia CHADEMA mchakato mwema. Mchakato wenye uwazi, usiopendelea mtu kwa ubaguzi wowote ule, na wenye kuboresha umoja kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020.
Mchakato wa kumpata mgombea Chadema una mvuto sana, na utavutia jamii ya watz na jumuiya ya kimataifa
 
Ndio uzuri na ubaya wa Demokrasia. Lakini kama kweli wana nia, malengo na matamanio yanayofanana; basi watavuka salama.
Hawawezi kuvuka, kumbuka Nyalandu alisema 2015 kuwa wamarekani ndiyo wamemtuma awe Rais kama si Lahisi wa Tanzania. Ilipobuma akahamia CDM. Inaaminika Wachagga hawakutaka TL awe Mwenyekiti wa CDM na alipoanza vituko sasa yupo Ubeleji. Leo hii TL kaweka nia na Mbowe (kiboko yao) katangaza pia. Hapo unategemea nini? Huoni TL kapoa sasa? CDM ikubali kuwa underdog wa upinzani hapa TZ au siyo Sky Eclat
 
Rubbish

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Siku moja tu baada ya Lisu kutumia masaa 4 akiwahutubia watanzania na kuwapa sababu za kwa nini anatangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania, huku nyuma Mbowe akaibuka na igizo la kuvamiwa na watu wasiojulikana, kisha kukanyagwa kanyagwa na kuvunjwa mguu wa kulia bila mtoto wake James aliyekuwa ndani kusikia chochote ,badala yake akasikia Joyce Mkuya aliyekuwa umbali wa kilomita
5!!
Lengo la hili igizo ilikuwa ni kufunika habari ya Lisu kuandikwa na vyombo vya habari.

Kana kwamba haitoshi Mbowe baada tu ya kuruhusiwa kutoka hospitali ,huku akichechemea akatangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania!
Yani watanzania wakiwa na hamu ya kusikia report kutoka kwa Mbowe mwenyewe kwamba alivamiwaje, ilikuwaje ,badala ya kujibu hizo hoja ,yeye akaja na igizo jingine la kwamba kuna wazee wameenda nyumbani kwake kumshawishi awanie urais wa Tanzania!!.

Hivi Lisu unataka ufanyiwe nini ndiyo ujue kwa sasa hauhitajiki Chadema?
Haya maigizo ya mwenyekiti wako wa chama kufunika utangazaji wako nia hayajakuamsha tu?.

Shituka
Kusema ukweli hata mimi kidogo imenishangaza hii. Sio kawaida ya CDM kutotolea ufafanuzi wa tukio la kuvamiwa. Nilitegemea Mh. Mbowe asema anachokijua juu ya tukio lile. Anyway, tumpe muda. Naamini atatuambia nini kilimsibu.
 
Hawawezi kuvuka, kumbuka Nyalandu alisema 2015 kuwa wamarekani ndiyo wamemtuma awe Rais kama si Lahisi wa Tanzania. Ilipobuma akahamia CDM. Inaaminika Wachagga hawakutaka TL awe Mwenyekiti wa CDM na alipoanza vituko sasa yupo Ubeleji. Leo hii TL kaweka nia na Mbowe (kiboko yao) katangaza pia. Hapo unategemea nini? Huoni TL kapoa sasa? CDM ikubali kuwa underdog wa upinzani hapa TZ au siyo Sky Eclat
Kama nakuelewa hivi. Kuna hoja kwenye maandishi yako.
 
Yeyote kati ya hao watano waliojitokeza kutia nia, anao uwezo mzuri sana wa kumkabiri mtesi wao bila ya shaka yoyote, hata kama kila mmoja wao anazo sifa zake zinazomtofautisha.

Kujitokeza kwa hao watano sioni sababu ya kuwepo wasiwasi ndani ya chama chao.

Kila mmoja ajinadi kadri awezavyo, na mwisho wa yote, mmoja wao apatikane kwa haki, kutokana na watakavyompima watakaohusika katika kumpitisha.

Na kama haya hayafanywi kwa sababu za 'mkakati' maalum waujuao wao CHADEMA, kujitokeza kwao ni ishara nzuri na kuonyesha ukomavu wa chama chao.

Wamejiwekea utaratibu wa jinsi mgombea atakavyopatikana; na kama kazi hiyo itafanyika kwa ufanisi, kwa nini pawepo na sintofahamu kati yao!

Acha hawa wapiga debe walioko nje ya chama wahangaike, lakini mwisho wa siku, heshima itakuwa kwa CHADEMA.
Ni matumaini yangu mchakato utaisha bila kuacha mpasuko.
 
Kama nakuelewa hivi. Kuna hoja kwenye maandishi yako.
Kwa wajinga ambao wanajifanya kutukana hapa JF hawawezi kunielewa, ndugu yangu huu ndiyo ukweli na inaonesha intelligensia ya CDM ni weak ndo maana wachagga wakaanza kuwa na Plan B yaani kufufua NCCR Mageuzi ili kulipa kisasi kwa Mrundi Zitto. Nani asiyejua kuwa 2020-2025 urais ni wa Magufuli? Ni TL pekee ambaye akili zake anazijua ambaye ana imani anapendwa na watanzania kiasi wampe kura ili amng’oe JPM. Thubutu
 
Hawawezi kuvuka, kumbuka Nyalandu alisema 2015 kuwa wamarekani ndiyo wamemtuma awe Rais kama si Lahisi wa Tanzania. Ilipobuma akahamia CDM. Inaaminika Wachagga hawakutaka TL awe Mwenyekiti wa CDM na alipoanza vituko sasa yupo Ubeleji. Leo hii TL kaweka nia na Mbowe (kiboko yao) katangaza pia. Hapo unategemea nini? Huoni TL kapoa sasa? CDM ikubali kuwa underdog wa upinzani hapa TZ au siyo Sky Eclat
Speculations tupu
 
Kwa wajinga ambao wanajifanya kutukana hapa JF hawawezi kunielewa, ndugu yangu huu ndiyo ukweli na inaonesha intelligensia ya CDM ni weak ndo maana wachagga wakaanza kuwa na Plan B yaani kufufua NCCR Mageuzi ili kulipa kisasi kwa Mrundi Zitto. Nani asiyejua kuwa 2020-2025 urais ni wa Magufuli? Ni TL pekee ambaye akili zake anazijua ambaye ana imani anapendwa na watanzania kiasi wampe kura ili amng’oe JPM. Thubutu
Kolola,

Nashukuru sana kwa mchango wako. Watu kama mimi napenda sana kujifunza. Ukiona mtu anakimbilia kutukana; tambua kwamba amechagua upande wa kushirikiana na UJINGA wake.

Nitaendelea kufuatilia maandishi yako. Yana mambo ya msingi yanayotafakarisha.
 
Back
Top Bottom