Maoni yangu kitalaamu kuelekea "fainali" dhidi ya Horoya

Maoni yangu kitalaamu kuelekea "fainali" dhidi ya Horoya

Wakubwa wenzangu tuache kujadili ulimbukeni wa jamaa zetu kwenye mashindano ya CAF, tujadili mambo ya msingi.

Clatous Chama amekuwa akipangwa winga huku Saido Ntibazonkiza akitumika kama kiungo wa kushambulia nyuma ya mshambuliaji wa kati.

Chama amekuwa akionyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho (assists) kulinganisha na Saido ambaye ameonyesha uwezo wa kufumania nyavu pindi anapopata fursa.

Kitendo cha kumpanga Chama pembeni kinaonekana kuipunguzia Simba idadi ya pasi za mwisho jambo linaloonekana kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa kati ambao wamekuwa wakipangwa, hivyo pengine Robertinho angejaribu kumtumia Saido winga na kumrudisha Chama acheze namba 10.

Maoni yangu ya kitaalamu ni hayo kuelekea Jumamosi kwenye fainali yetu. Wewe maoni yako ni yapi.
Galasa la yanga Leo hii ndio injini la Simba pale kwenye kushambulia,hahaaaa.[emoji23]
 
Chama na saido hawatakiwi kuanza wote,ni aidha aanze chama saido aanzie benchi nafasi yake aanze kibu.
 
Ww una utaalam upi!!?? Hujawahi kukochi hata timu za chandimu. Punguzeni midomo yenu mirefu na dharau. Tz sasa hv kuna timu moja tu Jangwani. Na kwa taarifa yako huu ni mwanzo tu.
Hiyo timu iko kwa walioshindwa,kweli kinyesi fc ni vilaza sana
 
Mleta mada amesema tujadili kitaalamu wewe unamshambulia mleta mada,hii ni haki kweli au hujaelewa uzi unataka nini?
Amesema ni maoni yake,wewe maoni yako ni yapi?
Hayanaga akili hayo myazoee
 
Back
Top Bottom