Mkuu, kama nilivyosema pale mwanzo ni kuwa toyota nyingi hazijatulia. Ila miongoni mwa chache zilizotulia ni kama hizo vx na v8.
Ngoja nikupe uzoefu wangu kidogo, nilikuwa nimezoea kuendesha SUV nissan ambayo kwa kawaida nimezoea kulala nayo katika kona hata nikiwa above 140, sasa siku moja nikaombwa kuwatoa watu Tanga niwapeleke Dar kwa harrier yao yaani nilijuta. Gari haishiki barabara kabisaaaa katika kona nikahisi kabisa inaweza kutuangusha basi nikawa mpole.
Pamoja na hayo yote, lipo jambo la msingi unapaswa kujua unapotaka kununua gari, je mahitaji yako ni yapi??? Ukijibu swali hili vzr ni rahisi kupata ushauri mzuri wa gari nzuri inayoweza kukufaa.
Mf: Kuna mtu anataka gari yenye hadhi - huyu malengo yake yatakuwa gari mfano v8, vx etc
Mwingine anahitaji gari ambayo ni fuel efficient atachukua gari ya cc ndogo au ambayo ni ya umeme zaidi
Mwingine yeye anajali brand ambayo ni unique
Mwingine anataka gari ambayo ni durable ili aitumie muda mrefu sana
Sasa basi ukiwa unajua unataka nini then unalinganisha na mfuko wako basi unapata kitu roho inapenda.