Maoni yangu kuhusu Sensa 2022

Maoni yangu kuhusu Sensa 2022

Tengeneza Njia

Senior Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
121
Reaction score
205
Wadau, hivi Serikali haikuona umuhimu wa kuunganisha masuala ya postal code na mifumo hii ya sensa?

Kama tayari anuani za makazi zipo kwenye system, huyu karani anayekuja kwenye makazi yetu alitakiwa kwanza akifika aingize ile anuani anayoikuta (kwenye milango yetu) au vibao vile walivyoweka kisha ku-pin (kama mtu unavyoweza kufanya kwenye google map etc.) hususani huku mjini - nafahamu kwamba vijijini inaweza kuwa ni changamoto kutokana na issue ya network.

Akisha-pin si zile details za awali zitatokea ndipo anakuwa ana uwezo wa kuendelea na kuuliza maswali mengine. Lakini ninachokiona mimi, bado tunasua sua na kama vile serikali haina uhakika na mifumo inayojitengenezea na mambo kama haya yanatengeneza mwanya wa watendaji kubuni miradi mingi yenye matumizi ya pesa yasiyo na tija.
 
Ngoja waje wachambuzi wa sensa mie nipo tu hapa
 
Back
Top Bottom